Tafuta

2026.07.15:Mwanzilishi wa Shirika la Mabinti wa Kanisa. 2026.07.15:Mwanzilishi wa Shirika la Mabinti wa Kanisa. 

Mkutano katika ishara ya Mama Oliva,Mwanzilishi wa Mabinti wa Kanisa

Mkutano wa kumkumbuka Mama Oliva,mwanzilishi wa Mabinti wa Kanisa,lilikuwa ni tukio la siku mbili kwa kuongozwa na mada:"Nilifanya uzoefu wa Upendo,"Julai 10-11, jijini Roma ili kufanya kumbukizi ya mtawa huyo miaka 50 baada ya kifo chake.Ulikuwa wakati wa"kuthibitisha umuhimu wa karama yake,ambayo inabaki kuwa mwaliko wa kutafakari na kuwa mitume walio wazi katika ulimwengu."

Vatican News

Safari ya kina kupitia Taalimungu, mambo ya kiroho, na historia  za maisha zilizoakisi umuhimu wa karama ya Mama Maria Oliva Bonaldo, mwanzilishi wa Mabinti wa Kanisa, ambaye aliyekuwa na uwezo wa kutambua Mtaguso wa Pili wa Vatican kupitia maono yake ya fumbo la Kanisa. Hili lilishuhudiwa wakati wa tukio la siku mbili la tarehe 10-11 Julai 2026, jijini Roma kwa kuongozwa na mada: "Nilifanya uzoefu wa Upendo," ambalo liliadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 tangu kifo cha Mama Bonaldo kilichotokea tarehe 10 Julai 1976. Mama huyo amekuwa Mtumishi wa Mungu tangu 2013.

L'apertura dell'incontro “Ho sperimentato l'amore”

Ufunguzi wa Mkutano: Nilifanya uzoefu wa upendo" 

Ufunguzi wa tukio hilo, ulifanyika tehe 10 Julai 2026 katika Nyumba ya Mtakatifu Maria jijini Roma ambayo ni makao Makuu ya Shirika hilo, uliokabidhiwa kwa Padre Ambroise Atapka, ambaye alichambua: "Vipeperushi 33" (maandishi ya mwanzilishi ya 1934) kwa kuzingatia majisterio ya sasa. Padre Ambroise aliita maandishi hayo kama "kito" kinachomweka Mungu katikati ya mambo ya Kanisa. Kulingana na mzungumzaji, maono ya Mama Oliva, yaliashiria katiba kuu za Mtaguso wa Pili wa Vatican: kutoka kuabudu kama ukuu (Sacrosanctum Concilium) wa Kanisa, hadi kama fumbo la Utatu (Lumen Gentium), kwa Neno la Mungu linaloakisi njia ya Kanisa(Dei Verbum) ya kuzungumza na ulimwengu(Gaudium et Spes). Kilichovutia zaidi ilikuwa kurudi kwenye mada ya (Ecclesia Mater,) yaani Mama wa Kanisa,  ambalo, kama Kristo, linakuwa "Mama" wa kuzaa watoto katika ubatizo. Siku ya ufunguzi ilifikia kilele chake cha  maadhimisho ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu Mkuu Filippo Ciampanelli, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

Sanaa ya Kuwazaa Watoto katika Imani

Siku ya Jumamosi, tarehe 11 Julai 2026, katika kituo cha kiroho cha Domus Aurea, shughuli zilifunguliwa kwa Misa iliyoongozwa na Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, ambaye aliwasihi waliokuwepo kuwa "walinzi wa tamaduni hai" na kukuza sanaa ya "kuzaa watoto katika imani." Mjadala uliofuata wa meza ya duara ulichunguza vipengele mbalimbali vya upendo aliouishi Mama huyo.

Filomena Sacco, profesa wa Taalimungu ya maadili katika vyuo vikuu kadhaa vya kipapa, alitafakari kuhusu uhusiano kati ya utii na utambuzi, akimtaja Augustino, ambaye kwake upendo ni "uzito wa roho" unaobadilisha utii kutoka kizuizi hadi uhuru. Pia umuhimu ulikuwa marejeo ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola na Mtakatifu Alphonsus Maria de' Liguori, ambao kwao uliakisiwa  uhusiano mkubwa na Mama Maria Oliva 

La celebrazione con le Figlie della Chiesa

Maadhumishi ya Misa na Mabinti wa Kanisa

Wafumaji wa muungano

Padre Ambrogio Giuffrida, Padre wa Siracusa, aliwasilisha wasifu wa upadre, "Mwana wa Kanisa," aliyeitwa kupenda Mwili wa Fumbo kwa kujitolea sawa kwa mwenzi kama Kristo. Sr Giulia Iuso, Binti wa Kanisa, alichunguza upendo wa Mama Oliva kwa maskini, akiuona si kama kundi la kijumuiya bali kama "mahali pa ufunuo" na "mwili wa Kristo." Paolo Zagami, wa Jumuiya ya Mabinti wa Kanisa huko Mtakatifu Stefano Briga, katika Wilaya ya Messina, alielezea upendo unaohitaji "mioyo mikubwa kama dunia," yenye uwezo wa huruma ya kibinadamu na kuwa "wafumaji wa ushirika" katika maisha ya kila siku.

Mwali wa moto unaoishi leo hii

Alasiri hiyo ilitolewa kwa sauti za "familia yenye karama." Kupitia historia zenye kugusa moyo, iliibuka jinsi gani karama ya Mama Oliva inavyoendelea kufanya kazi katika miktadha mbalimbali: kutoka katika kujitolea kwa ajili ya kiekumene kulikosimuliwa na Padre wa Kiorthodox, Padre Vladimir, ambaye alikumbuka huduma yao ya pamoja kwa maskini katika mitaa ya Roma, hadi ugunduzi mpya wa Anna na Rossella wa imani yao na "ubinti" wa kikanisa katika jumuiya za Calabria,  Nicotera, hadi Stefano, na ambaye aliwasili kutoka Mestre ya Sabina ya Nuoro, na Elena, ambaye aliwasili kutoka Barcelona, ​​​​Hispania. 

Ushuhuda wa Sr Eterna unaogusa moyo ulikumbusha kukutana kwake kibinafsi na Mwanzilishi na uwezo wake wa kusikiliza kama mama. Siku zilimalizika kwa wakati wa kuabudu na ahadi ya kuendelea kutembea "kwa mwendo wa Kanisa." Kama Mkuu wa Shirika Mama María Santos García alivyosisitiza, kuwa "maadhimisho haya hayakuwa ukumbusho wa kumbukumbu, bali fursa ya "kuanza upya kutoka moyoni mwa Kristo kuelekea njia panda ya ubinadamu." Urithi wa Maria Oliva Bonaldo unabaki kuwa mwali unaoishi leo: mwaliko wa kuwa "wa kutafakari, kuungana naye kila wakati; na mitume, daima wakiwa wazi kwa wote."

Foto di gruppo

Picha ya kundi  la ushiriki wa siku mbili.

Imesasishwa tarehe 15 Julai 2026 saa 10.00 jioni na Angella Rwezaula.

MAMA OLIVA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

15 Julai 2026, 16:00