Tafuta

2026.07.15 Watawa wa UISG wakutana Camilla. 2026.07.15 Watawa wa UISG wakutana Camilla.  (© BuckinghamPalace)

Uingereza,Muungano kati ya UISG na Camilla kwa ajili ya wanawake umeanzishwa

Katika makazi ya kibinafsi ya familia ya kifalme ya Uingereza,wawakilishi wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa mashirika (UISG)walikaribishwa na Malkia Camilla. Majadiliano hayo yalilenga katika usaidizi kwa wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi,mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu na kujitolea kwa ajili ya haki ya tabianchi.

Vatican News

Karibu mwaka mmoja baada ya mkutano wa kihistoria uliofanyika wakati wa ziara ya Wafalme wa Uingereza, kwa Baba Mtakatifu, wawakilishi wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa (UISG) waliweza kukutana na Malkia Camilla tena ili kushirikisha matunda ya kujitolea kwao kwa walio katika mazingira magumu zaidi. Mkutano huo ulithibitisha mazungumzo yaliyoanzishwa vizuri, yaliyotokana na wasiwasi wa pamoja kwa utu wa binadamu, ulinzi wa wanawake na wasichana, na utunzaji wa kazi ya uumbaji.

Pamoja na wanawake walio katika mazingira magumu zaidi,

Wakati wa mkutano huo, huduma ya kila siku ya takriban wanawake 600,000 Watawa waliopo katika mazingira magumu zaidi duniani iliakisiwa. Kuanzia waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu hadi watu waliolazimishwa kuhama, kuanzia jamii zilizoathiriwa na migogoro hadi idadi ya watu walio maskini kutokana na athari za mgogoro ya tabianchi ,  watawa hao wanaendelea kuwa uwepo imara na wa kutegemewa, mara nyingi ambapo taasisi zingine hazifikii. Malkia Camilla aliboresha uthamini wake kwa uwepo huo ulioenea na kwa kazi ya kuhamasisha hadhi ya wanawake na wasichana, akithibitisha tena kujitolea kwa Familia ya Kifalme ya Uingereza kwa juhudi hii.

Talitha Kum, mtandao wa kimataifa dhidi ya biashara haramu ya binadamu

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa, umakini maalum ulitolewa kwa kazi ya Talitha Kum, mtandao wa kimataifa wa watawa waliojitolea kuzuia na kupambana na biashara haramu ya binadamu, ambao kwa sasa upo katika nchi zaidi ya 110 kupitia mitandao 68 ya kitaifa na kikanda. Sr Abby Avelino alielezea maendeleo yaliyopatikana katika kuwasaidia waathiriwa na manusura wa unyonyaji, akizingatia mpango wa Mabalozi Vijana Dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu. Ukiwa umeanzishwa kwa usaidizi wa Serikali ya Uingereza na sasa unapanuka duniani kote, mpango huo unawashirikisha vijana katika kuzuia utumwa mamboleo, na kuwawezesha kuongeza uelewa katika jamii zao.

Kujali Uumbaji kama Haki ya Kijamii

Lengo lingine muhimu la mkutano huo lilikuwa kujitolea kwa UISG kwa haki ya haki ya tabia nchi. Sr  Maamalifar Poreku aliwasilisha mipango iliyochochewa na Mashirika ya kitawa  ili kusaidia jamii zilizo wazi zaidi kwa athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia mipango katika elimu ya mazingira, kilimo endelevu, upatikanaji wa maji, na kuimarisha ustahimilivu wa wenyeji. Tafakari hiyo ilionesha jinsi janga la tabianchi linavyoathiri hasa idadi ya watu walio katika mazingira magumu zaidi, hasa wanawake na wasichana, na kufanya ulinzi wa uumbaji, mapambano dhidi ya umaskini, na kuhamasisha haki ya kijamii.

Msaada Unaoimarisha utume

Mkutano huo ulithibitisha maelewano makubwa kati ya kazi ya masista Wakatoliki na umakini wa Familia ya Kifalme ya Uingereza kwa changamoto kubwa za kibinadamu za wakati wetu. Msaada huu unawakilisha utambuzi muhimu wa huduma ya kimya inayofanywa kila siku na watawa katika mabara matano na unahimiza ushirikiano wa karibu zaidi kati ya taasisi, asasi za kiraia, na jumuiya za kitawa. Kuanzia utetezi wa wanawake waathiriwa wa vurugu na unyonyaji hadi ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja, mazungumzo kati ya UISG na Malkia Camilla yanaonyesha jinsi kushiriki maadili na malengo kunaweza kutafsiri kuwa kujitolea kwa dhati kwa hadhi ya mtu na manufaa ya wote.

MTANDO WA UISG
16 Julai 2026, 09:31