Wanafunzi wawili wa Asili wa Australia wapokea Udhamini wa Francis Xavier Conaci
Na Kielce Gussie – Vatican
Kwa miaka 50 iliyopita, Juma kamili la kwanza la mwezi Julai kila mwaka limekuwa likitengwa kwa ajili ya kusherehekea sauti, tamaduni na mila za jamii za Asili ya Australia yote, ambazo zimekuwa sehemu ya historia ya nchi hiyo kwa makumi ya maelfu ya miaka. Juma hili linajulikana kama Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Watu wa Asili na Visiwa (NAIDOC). Kila mwaka, wanafunzi wawili wa Asili husafiri kuja Roma kusoma kama sehemu ya Mfuko wa Udhamini wa Francis Xavier Conaci, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Katoliki cha Australia (ACU) na Ubalozi wa Australia unaowakilisha nchi yake katika Kiti Kitakatifu kuwakilisha tamaduni zao duniani. Mwaka huu 2026, wanafunzi wawili waliopokea udhamini ni Hayden Atkins, miaka 24, na Tanisha Julie Sonter, miaka 20 wote wawili ni kutoka lugha ya kale ya Dharug huko New South Wales, Australia. Hii ni mara ya kwanza kwa wanafunzi kutoka eneo moja la watu wa asili kupokea udhamini huo katika mwaka mmoja.
Pande mbili za sarafu moja
“Juma la NAIDOC, kwa muonekano wa sasa ni hafla ya mafanikio ya watu wa Asili na kuakisi ukuaji wa utamaduni wa Watu wa Asili nchini Australia katika kipindi cha miaka 50 iliyopita,” Hayden alielezea. Kwake, kupokea udhamini huu na kuwa Roma kunawakilisha "mafanikio ya Watu wa Asili yanavyoonekana leo hii katika utamaduni na historia ya Australia.” Watu wa asili wa lugha ya Dharug huko Sydney wanatambuliwa kama Waaustralia wa Kwanza na utamaduni wa zamani zaidi unaoendelea kuishi duniani wenye historia ya miaka 60,000.
Mila na Tamaduni na historia yao ndiyo Hayden na Tanisha wanataka kushirikisha ulimwengu. "Ni jambo kubwa sana kuwakilisha utamaduni wetu nje ya nchi kwa sababu si utamaduni unaojulikana sana au kueleweka," Tanisha alielezea. "Ninahisi kama mapinduzi sana." Zaidi ya hayo, alisisitiza athari ambayo yeye na Hayden wanaweza kuwa nayo kwa vizazi vijavyo baada yao, akibainisha kuwa wanaweza kuwa mifano ya kile ambacho watoto wachanga wa Watu Asilia wanaweza kufikia na kile kinachowezekana.
Hili ni muhimu kwao kuliona, Tanisha alisisitiza, kwa sababu linavunja vikwazo. "Ni muhimu kuonesha kwamba unaweza kuvunja mipaka, na kwenda hata maeneo, mapya, na bado kudumisha nafsi yako na utamaduni wako ndani yake." Kuelewa umuhimu wa kushiriki utamaduni wa Dharug na watu wengine, si nje ya Sydney tu bali ulimwenguni, ni jambo ambalo Tanisha anashirikisha na Hayden. Alibainisha kuwa Juma la NAIDOC na udhamini huo unamwezesha yeye na watu wengine wa Watu wa Asilia kuakisi "upande wao wa Kiingereza, lakini pia upande wetu wa Asili na jinsi wanavyofungamana na jinsi hilo linavyowakilishwa katika ulimwengu wa leo hii."
Australia na Roma: Uhusiano wa karne nyingi
Ingawa udhamini wa Conaci umetolewa kwa miongo mitano iliyopita, uhusiano wa Watu wa Asili wa Australia na Vatican ni wa kiutamaduni. Katika safari iliyoandaliwa na Ubalozi wa Australia Vatican, Hayden na Tanisha waligundua jinsi ambavyo Basilika ya Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta ilivyo mahali penye makaburi ya waseminari wawili wa Asili, Dioram (au Dirimera) na Francis Xavier Conaci, wa mwisho akiwa jina la udhamini uliowaleta wanafunzi hao wawili Roma. Wavulana hao wawili wadogo wa asili waliletwa Italia katikati ya miaka ya 1800 na Askofu Rosendo Salvado wa Monasteri ya New Norcia huko Australia Magharibi. Hata hivyo, wote wawili waliugua na kufariki kabla ya kukamilisha masomo yao ya Seminari. Hayden alikiri jinsi ilivyokuwa vigumu kwa wote wawili hao kuacha kila kitu na kila mtu waliyemjua na kuja Italia. "Kuwa wa kwanza wa kufanya chochote, kuondoka katika eneo lako, kuondoka bara lako na kutafuta kitu kikubwa kuliko wewe mwenyewe, nadhani hiyo ni ya ajabu sana na inatia moyo," alielezea.
Nusu karne
Hayden na Tanisha, wote wawili walisisitiza jinsi ilivyokuwa shukrani na maana kupokea udhamini huo, si kwa ajili yao wenyewe tu bali kwa jamii yao yote ya watu wa Asili huko Australia. Tanisha alisisitiza jinsi ilivyo muhimu kuwa na udhamini unaohusishwa na Juma la NAIDOC. "Kiukweli tunaonesha jinsi tumefikia hatua gani kama watu wa asili na fursa tulizonazo sasa, na jinsi tulivyoendelea kwa muda, na ni dalili wazi. Mada ya hatua hii muhimu ya nusu karne ni Miaka Hamsini ya ufufuko. Inawakumbuka watu waliounda mpango huu na ambao walianzisha nafasi kwa watu wa leo, kama Tanisha na Hayden, kuelezea utamaduni na mila zao katika kila kona ya dunia.
Imesasishwa tarehe 8 Julai 2026 saa 4.00 kamili na Sr Christine Masivo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.