Tafuta

2026.07.14  Wanasheria Watawa Katoliki Barani Afrika watafanya Kongamano lao la Kwanza nchini Kenya. 2026.07.14 Wanasheria Watawa Katoliki Barani Afrika watafanya Kongamano lao la Kwanza nchini Kenya.  (Photos By CASILEP)

Wanasheria masista Katoliki barani Afrika wajenga mtandao wa kisheria kwa ajili ya haki

Kuanzia Julai 30-31,2026 jijini Nairobi Kenya litakaribisha Kongamano la Kwanza la Wanasheria Watawa Katoliki Barani Afrika.Wakitafuta kuimarisha ushirikiano,kujifunza na usaidizi wa kitaaluma miongoni mwa watawa huku wakihudumia mashirika ya watawa kupitia huduma ya kisheria.Watashughulikia changamoto muhimu katika maisha ya kitawa huku wakiendeleza haki, utu wa binadamu na manufaa ya wote.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Zaidi ya Watawa Katoliki 100  wa mashirika tofauti ambao ni wanasheria wa Kanuni za Sheria za  Kanisa na Sheria za Kiraia,(Lawyers of Canon Law and Civil Law,)watakusanyika jijini Nairobi kuanzia tarehe 30 - 31 Julai 2026 kwa ajili ya Kongamano la Kwanza la kihistoria lililoandaliwa na Masista Katoliki Wanasheria (CASILEP) nchini Kenya. Kongamano hilo litaongozwa na mada: “Ushahidi wa Kinabii wa Watawa Wakatoliki katika Masuala ya Sheria za Kanoni za Kanisa na Sheria za Kiraia,” wakihamasisha kujifunza, kushirikiana miongoni mwao katika taalamu ya kisheria kama wanasheria wanaohudumia Taasisi za Kanisa na maisha ya Utawa barani Afrika.

Kujenga mtandao wa haki katika maisha ya kitawa

Kongamano hilo litawaleta pamoja watawa wanasheria, ili kutoa usaidizi wa kitaalamu na kuhamasisha haki katika masuala yanayoathiri uwajibikaji unaoathiri maisha ya kitawa. Mpango huu mzuri unaungwa mkono na Umoja wa Masista wa Kenya (AOSK) na kufadhiliwa na Mfuko wa Conrad N. Hilton, ambao ulizinduliwa rasmi tarehe 10 Januari 2026, na Askofu Mkuu Philip Anyolo wa Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi. Sr. Teresiah Muthoni, LSOSF, ambaye ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya, Mchunguzi Mkuu na Sr. Eutropia Chao Mwakamba CPS,  Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Wanasheria Watawa Katoliki(CASILEP), wakizungumza na Vatican News walieleza  kwamba, malengo makuu ya Kongamano hilo ni “kukuza utamaduni wa ushirikiano na kuunda jukwaa la kuunganisha miongoni mwa watawa, ambao mara nyingi hutoa huduma za  ndani tofauti za Kanisa, nchi na mashirika. Ili kujifunza kutokana na uzoefu wa kila mmoja, kutambua wasiwasi wa kawaida na kuhamasisha njia za vitendo za kusaidiana katika huduma zao husika.”

CASILEP.Kenya
CASILEP.Kenya   (Photos By CASILEP)

Kujibu changamoto zinazoibuka katika maisha ya watawa

Kongamano hilo litakuwa la muhimu kwa sasa kwa mashirika mengi barani Afrika yanayokabiliwa na changamoto ngumu zaidi za kisheria, kichungaji na kiutawala. Masuala yaliyotambuliwa ni kuanzishwa kwa utume  mpya katika nchi tofauti, kufuata mifumo tofauti ya kisheria ya kiraia na uhusiano wa usimamizi kati ya majimbo na mashirika ya kitawa. Sr. Teresiah na Sr. Eutropia pia walibainisha kwamba, idadi inayoongezeka ya kesi zinazohusiana na ulinzi na usalama, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki na migogoro kati ya wanashirika na uongozi wa shirika. Suluhishi  na upatanishi vimekuwa zana muhimu katika kurejesha uhusiano na kuhamasisha mazungumzo kati ya wanashirika na miundo ngazi za uongozi. Kongamano hilo “litatoa nafasi ya kutafakari juu ya hali halisi na kutambua majibu madhubuti yanayotokana na haki na utunzaji wa kichungaji.”

Sinodi na hadhi ya binadamu

Sr. Teresiah alisema kwamba, “Kongamano hili  litaakisi wito wa Kanisa wa Sinodi kupitia kusikiliza, kushirikiana na utambuzi wa pamoja. Kupitia vikao vya jumla na majadiliano ya jopo, masista watachunguza jinsi ambavyo Kanuni na sheria za Kanisa na wanasheria wa kiraia yanavyoweza kufanya kazi pamoja katika kutumikia Kanisa na Utume. Msisisitizo  zaidi utakuwa katika ulinzi, uwajibikaji, utawala na ulinzi wa hadhi ya binadamu. “Kupitia mafunzo, masasisho ya sera, usaidizi wa kufuata sheria na utetezi, watachangia katika kuimarisha miundo ya utawala ndani ya mashirika huku wakihakikisha kwamba haki na hadhi ya watu wote inaheshimiwa,” alisisitiza Sr. Eutropia. Watachunguza jinsi ambavyo wataalamu wa sheria wanavyoweza kuwasaidia waathiriwa wa nyanyaso  na udhaifu wao huku wakilinda haki za pande zote zinazohusika. "Kulinda hadhi ya  binadamu bado ni muhimu kwa kila mchakato wa kisheria ndani ya Kanisa, Sr. Teresiah alibainisha.

Watawa nchini Kenya wanasheria wakitoa kiapo kwa Askofu
Watawa nchini Kenya wanasheria wakitoa kiapo kwa Askofu   (Photos By CASILEP)

Ushirikiano na upatikanaji wa haki

“Tunatumaini kwamba Kongamano hili litakuwa kichocheo cha kuundwa kwa mtandao wa wanasheria watawa katoliki wa Kitaifa na kikanda barani Afrika, na kuwawezesha kushirikiana kwa ufanisi zaidi na kuvuka mipaka,” Sr. Eutropia alisema. Na zaidi “ili kurahisisha mashirika yanayofanya kazi katika nchi nyingi kupata huduma ya kitaalam ya kisheria na kupokea msaada kutoka kwa watawa wanasheria ambao, wanelewa mktadha wa kitawa kutumia Kanoni za Sheria na Sheria za kiraia. Kwa upande wa Sr. Teresiah aliunga mkono pia kwamba, “Wanasheria Watawa watatoa mapendekezo yao na hati ya tafakari ya pamoja ambayo wawasilishaji na wajumbe watatoa. Maoni yao yatasaidia kuongoza huduma za kisheria za siku zijazo miongoni mwa watawa Wakatoliki na kuchangia katika malezi endelevu katika masuala yanayoathiri maisha ya kitawa.” Kwa kuongozwa na Injili  na utume wa pamoja, Masista Wakatoliki Wanasheria(CASILEP) nchini Kenya, wanafuta kuhakikisha kwamba “kila mtawa anasikilizwa, anathaminiwa, analindwa na kuwezeshwa kuishi wito wao kwa heshima na bidii katika kumtumikia Mungu na watu wake.”

WANASHERIA WATAWA WAKATOLIKI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

13 Julai 2026, 11:18