Tafuta

Papa alipokutana na Wanashirika la Mateso(Wapasionisti). Papa alipokutana na Wanashirika la Mateso(Wapasionisti). 

Papa Francisko:msalaba ni kitovu cha wokovu wa binadamu

Kusaidia uinjilishaji aminifu katika mtindo wa Mungu na ukaribu wa watu,ndiyo matumaini na matashi mema ya Papa Francisko yaliyomo kwenye ujumbe alioutuma katika fursa Mkutano wa kitaalimungu kimataifa ulianza 21-24 Septemba katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Papa Francisko aliouelekeza kwa Mkuu wa Shirika la Mateso (Wapasionisiti), Padre Joachim Rego, umemfikia katika ufunguzi wa Mkutano ambao unaona ushiriki wa mamia ya wasomi na ambao si wa imani ya kikristo lakini madhehebu mengine ya kidini kama vile Uislamu kuanzia tarehe 21 hadi 24 Septemba 2021. Kiini ni msalaba wa wokovu wa Yesu ambao ameutoa kwa binadamu wote katika uhusiano na ulimwengu wa dini nyingi na utamaduni mwingi. Kwa maana hiyo kauli mbiu iliyochaguliwa kuongoza mkutano huo ni Hekima ya Msalaba katika ulimwengu wa wingi wa dini na utamaduni katika muktadha wa Jubilei ya miaka 300 tangu kuanzishwa kwa shirika hili

Papa Francisko akitoa salamu kwa washiriki, amekumbusha kile ambacho kilikuwa ni shauku ya miaka 300 iliyopita ya Mwanzilishi wa Shirika la Mateso, Mtakatifu Paulo wa Msalaba ambaye alijikita katika mtondo wa Fumbo la Kipasaka kiini cha imani ya kikristo na karama ya Familia ya shirika wa Mateso, ili iweze kuangaza na kuendelea kuwa kujibu la dhati la upendo wa Mungu na ili kuweza kukutana na  matarajio na matumaini ya ulimwengu.  Papa Francisko akizunguzmia juu ya upendo wa Kristo, amebainisha kwamba “kwa kutafakari kwa kina juu ya Msalaba, tunaona ukuu wa kibinadamu uliokumbatiwa na huruma ya Mungu. Upendo wake wa kenotico na huruma yake kuu, inagusa kwa njia ya Msalaba, katika misingi mikuu minne na kufikia ncha ya hali hasi yetu, ikiunganisha kwa namna ya ajabu uhusiano wa juu na Mungu na ule ulio chini na watu, katika udugu ambao kifo cha Yesu kilifanya kuwa cha ulimwengu wote”.

Papa Francisko amebainisha kuwa wokovu ulioletwa na Yesu kutoka msalabani, hasa kutokana na udhaifu wa msalaba ndiyo unafundisha taalimungu ya kuunganisha ukuu wa wazo la unyenyekevu wa moyo. Mbele ya Msalaba, unaalikwa kuutazama kwa hali halisi za walio dhaifu zaidi na kwa binadamu wa dhati, na kuachwa kungazwa nao.  Akikabiliana na maana ya Msalab, amewaalika kurejea katika hali dhaifu na thabiti ya mwanadamu na kukataa kila njia na nia mbaya, ili kushiriki kwa moyo wenye furaha juhudi ya kujifunza na kutafuta kwa ujasiri mbegu za thamani ambazo Neno huenea katika wingi na wakati mwingine unapingana na utamaduni.

Msalaba hufunua umuhimu wake na ufanisi hata katika hali, kama ile ya sasa inayojulikana na mabadiliko ya haraka na magumu, na kwa kile ambacho amependekeza katika mkutano huo ni muhimu, kuingiza hekima ya Msalaba katika mazingira mbali mbali ya kiutamaduni na kijamii ya leo hi ina   kuhamaisha  matukio mapya ya uinjilishaji ulio mwaminifu kwa mtindo wa Mungu na karibu na mwanadamu. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki wa mkutano huo uwe na matunda ya kitaalimungu, kiutamaduni na kichungaji chini ya ulinzi wa Bikira Maria na Mtakatifu Paulo wa Msalaba.

21 September 2021, 17:21