Tafuta

Papa Francisko:matumaini ya dunia yanajengwa kwa pamoja!

Katekesi ya Papa Francisko imejikita katika ziara ya kitume huko Budapest na Slovakia iliyotimishwa wiki moja iliyopita,akikumbusha mikutano ya makanisa ya kikristo,wayahudi,wasio waamini na dhaifu zaidi.Ziara yake ameiweka katika sehemu tatu:hija ya sala,katika mzizi ya imani na ya matumaini.Matumaini ya ulimwengu ujao utajengwa kwa pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatato tarehe 22 Septemba, Baba Mtakatifu Francisko amekuwa katika Ukumbi wa Papa Paulo VI  Vatican, katika  katekesi yake ambapo leo amejikita kuwalezea juu ya ziara yake ya kitume aliyokwenda  huko Budapest na Slovakia, ambayo ilihitimishwa wiki moja iliyopita, yaani Jumatano.  Kwa ufupi Papa Francisco ameifafanua kuwa kwamba ilikuwa  hija ya sala, hija katika mizizi na hija katika matumani, kwa maana hiyo katika mambo matatu sala, mizizi na matumaini. Hatua ya kwanza ni Budapest, kwa ajili ya kuhitimisha  Kongamano la Ekaristi kimataifa, ambalo lilikuwa limeahirishwa kutokana na janga. Ushiriki ulikuwa mkubwa katika sherehe hizo. Watu wa Mungu katika Siku ya Bwana waliunganika mbele ya mafumbo ya Ekaristi ambayo inaendelea kuzaa daima. Ilikuwa ni mkubatio wa Msalaba ambao ulikuwa umewekwa juu ya Altare kuonesha mwelekeo huo wa Ekarist, yaani njia ya upendo mnyenyekevu na usiojiependelea, upendo mkarimu na unaoheshimu wote, njia ya imani ambayo inatakata na maovu ya kidunia na kutufikisha katika yaliyo ya muhimu. Imani hii inataka daima na kutuepusha na malimwengu ambayo yanatuharibu wote, ni mnyoo unaotuharibu kwa ndani, Papa Francisko amesema.

Hija ya sala ni ile ambayo ilihitimishwa huko Slovakia katika Siku kuu ya Maria wa mateso. Hata huko Šaštín, katika Madhabahu ya Bikira  Maria wa Mateso Saba, wana wa Mungu walikuja kwenye siku kuu ya Mama na ambayo ni siku kuu ya kitaifa kipya. Hija yake ilikuwa ni ya sala katika moyo wa Ulaya, kwa kuanza na kuabudu na kuhitimisha na ibada za watu. Papa Francisko amesema  kwamba kusali ndiyo awali wanaitwa watu wa Mungu  hasa kuabuui, kusali, kutembea, hija, kitubio na katika yote hayo kuhisi amani, na furaha ambayo anatupatia Bwana. Maisha yetu lazima yawe hivyo kuabudu, kusali, kutembea, kufanya hija na kitubio. Ni kile ambacho kina umuhimu sana katika bara la Ulaya mahali ambapo uwepo wa Mungu umechakachuliwa, kwa kuwa inaonesha kila siku, kuanzia na  utumiaji  hovyo na kama vile mvuke wa wazo moja, jambo ambalo ni la kushangaza lakini la ukweli, ambalo ni matokeo ya mchanganyiko wa itikadi za zamani na mpya. Hii inatutenga mbali  na kumjua kwa karibu Bwana, kumjua Mungu kifamilia. Hata katika muktadha huu, majibu ya uponyaji yanatokana na sala, ushuhuda na upendo mnyenyekevu. Upendo mnyenyekevu unaohitajika. Papa Francisko ameomba ili wachukue wazo hili tena kwamba “mkristo ni kwa kutumikia”

Hayo ndiy aliyoona  Papa katika Mkutano na watu watakatifu wa Mungu, Je aliona nini. Papa ameongeza kuthibitishwa kuwa aliona watu waamini, ambao waliteseka katika kumkana Mungu. Aliona katika nyuso zao kaka na dada wayahudi walio wakumbuka katika kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari Shoah. Kwa kuwa hakuna sala bila kuwa na kumbu kumbu. Papa ameulioza mawasili “ Je ina maana gani hiyo? Sisi tunapokuwa tunasali, lazima kufanya kumbu kumbu ya maisha yetu, ya watu wetu, ya maisha ya watu wengi ambao walitusindikiza katika mji kwa kuzungatia historia yao ilikuwaje”. Papa Francisko ametoa mfano kuwa mmoja wa maaskofu wa Slovakia  ambaye ni mzee, wakati wa kumsalimia alisema: “nilifanya kazi ya  udreva wa bus ili kujificha dhidi ya wakomunisti”.  Amemsifu Askofu huyo, kwa sababu ameongeza: “wakati wa udiktetea, wa mateso yeye alikuwa ni dreva wa Bus na  wakati huo huo kwa siri aliendelea na  kazi yake kama Askofu na hakuna yoyote aliyekuwa anajua. Ndivyo ilivyo katika mateso. Hakuna sala bila kumbu kumbu. Kusali, kufanya kumbu kumbu ya maisha binafsi na ya watu binafsi kwa historia yao, ndiyo jambo jema na inasaidia kusali”, Papa Francisko amesisitiza.

Mantiki ya pili ambayo Papa Francisko katika safari hiyo aieleza ilikuwa ni mhujaji kwenye mizizi. Alikuwana na ndugu maaskofu wa Budapest na  Bratislava, ambapo aliweza kugusa kwa mkono wake  kumbu kumbu ya shukrani kwa chimbuko la imani hii na maisha ya kikristo, kwa mfano angavu wa shuhuda nyingi za imani kama vile Kardinali Mindszenty na  Korec, kwa mwenyejeri Askofu Pavel Peter Gojdič.  Mizizi hii inayosimikwa kwa kina hadi karne ya tisa, kufikia kazi ya uinjilishaji wa watakatifu Ndugu Cirilly na Metodius, ambao waliwasindikiza katika ziara hii kama uwepo wao halisi. Papa Francisko amethibitisha jinsi alivyohisi nguvu ya mizizi hiyo wakati wa maadhimisho ya Liturujia takatifu ya Kibizantina huko  Prešov, katika Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba. Katika nyimbo Papa alihisi mtikisiko wa moyo kwa watu watakatifu waaminifu wa Mungu ambao waliteseka sana kwa sababu ya imani yao. Mara nyingi  Papa amesema alisisitizia kuhusu mizizi hii ambayo daima ni  hai, iliyojaa kiini hai ambacho ni Roho Mtakatifu na kama ilivyo wanapaswa kuilinda, na si kama vifaa vilivyo kwenye makumbisho, sio itikadi na kunyonywa kwa ufahari na masilahi ya nguvu, kuimarisha kitambulisho kilichofungwa. Hapana. Hiyi amesema  ingemaanisha kuwadanganya na kuwa tasa! Cyrilly na Methodius sio wahusika kwa ajili yetu wa kuwakumbuka tu, lakini ni mifano ya kuigwa, waalimu ambao kila wakati tunajifunza kutoka kwao roho na njia ya uinjilishaji, na pia kukitoa kwa raia

Papa amesema wakati wa ziara yake katika moyo wa Ulaya alifikiria mara nyinyi Mababa wa Umoja wa Ulaya kama walivyoita si kama shirika kwa ajili ya kugawanya ukoloni wa kiitikadi uliopo kwenye mtindo mbalimbali, hapa, wao waliota ndoyo ya Ulaya. Kama jinsi ilivyosukwa na kuishi mizizi ndiyo uhakika wa wakati ujao, kutokana na hiyo ndipo matawi yenye nguvu na matumaini yanachomoza. Papa Francisko amesema, hata sisi tunayo mizizi, kila mmoja anayo mizizi yake. Lakini Je! tunaikumbuka mizizi yetu? Ya babu na bibi? Je sisi tunao uhusiano na bibi ba babu ambao ni tunu? Wengine watasema, lakini ni wazee, hapa wao wanatoa kiini, muhimu wewe kwenda kwao na kujifunza kutoka kwao uweze kuku ana kwenda na kuiendeleza mbele. Wakati mwingine hatusumi “nenda, kimbia kwenye mizizi, hapana. Urudi katika mizizi na kuchukua kiini na kuendelea mbele. Nenda katika nafasi yako” Papa Francisko amehimiza wasisahahu hilo. “Ninarudia kusema ambayo mara nyingi niliwambia kwa sababu ni nzuri: “Kila kitu ambacho mti huo umechanua maua hutoka kwa kile kilichozikwa chini”. Unaweza kukua kwa kiwango ambacho umeunganishwa na mizizi: nguvu hutoka hapo. Ukikata mizizi, kila kitu kipya, lakini itikadi mpya, hii haikupelekei chochote, haikukuzi badala yake  utakua na kuishia pabaya”.

Papa Francisko akijikita kuelezea mantiki ya tatu ya ziara yake ya kitume, ilikuwa ni hija ya tumaini. “Kama alivyoeleza tangu mwanzo mambo matatu ya safari yake kwa ajili ya sala, katika mzizi na matumaini. Niliona matumaini mengi machoni pa vijana, katika mkutano ambao hautasahaulika kwenye uwanja wa Košice. Hii pia ilinipa matumaini, kuona wanandoa wengi, vijana na watoto wengi. Na nilifikiria msimu wa kupungua kwa idadi ya watu, na nchi hizo zinastawi na wenzi wa ndoa na watoto ambayo ni ishara ya matumaini. Hasa wakati wa janga, wakati huu wa sherehe ilikuwa ishara muhimu na yenye kutia moyo, pia shukrani kwa uwepo wa wanandoa kadhaa vijana, na watoto wao. Ushuhuda wa Heri Anna Kolesárová, msichana wa Kislovakia ambaye kwa gharama ya maisha yake alitetea hadhi yake dhidi ya vurugu: ushuhuda ambao ni muhimu zaidi kuliko hapo awali, kwa bahati mbaya, kwa sababu unyanyasaji dhidi ya wanawake ni janga lililo wazi kila mahali”.

Papa akiendelea amesema aliona tumaini kwa watu wengi ambao hujali wengine kwa kimya. Amefikiria Masista Wamisionari wa Upendo wa Kituo cha Bethlehem huko Bratislava, watawa wazuri, ambao hupokea waliobaguliwa katika jamii; wao wanasali na kutumikia, wanasali na kusaidia, bila kujidai. Hao ndio mashujaa wa ustaarabu huu. “Ningependa sisi sote kuwa na shukrani kwa Mama Teresa na watawa hawa: wote kwa pamoja tunawapigia makofi watawa hawa wazuri!.... Watawa hawa wanawakaribisha watu wasio na makazi maalumu. Ninafikiria jumuiya ya Warom wale wanaojitolea kwao kwa safari ya undugu na ujumuishaji. Ilikuwa jambo la kugusa sana la kushirikishana sikuu ya Jumuiya ya Warom. Siku kuu rahisi ambayo ilitambua Injili. Warom ni ndugu zetu: lazima tuwakaribishe, lazima tuwe karibu kama vile Mababa wa Kisalesiani wanavyofanya huko Bratislava, walio karibu sana na Warom”.

Papa ameongeza kusema kuwa tumaini hili, la Injili ambalo ameweza kuona kwenye safari, limetimizwa, na linakuwa halisi ikiwa tu linaoneshwa na neno jingine: pamoja. Tumaini halikatishi tamaa kamwe, tumaini haliendi peke yake, lakini pamoja. Huko Budapest na Slovakia waliweza kukutana wakiwa pamoja na ibada tofauti za Kanisa Katoliki, pamoja na ndugu wa madhehebu mengine ya Kikristo, pamoja na ndugu wa Kiyahudi, pamoja na waamini wa dini zingine, pamoja na wadhaifu zaidi. Hii ndiyo njia, kwa sababu siku zijazo zitakuwa za matumaini ikiwa zitakuwa pamoja, sio peke yake: hii ni muhimu”.  Kwa kuhitimisha Papa amesema kuwa,  baada ya safari hii, kuna kuna asante kubwa moyoni mwake. Shukrani kwa Maaskofu, shukrani kwa viongozi wa serikali, shukrani kwa Rais wa Hungaria na Rais wa Slovakia; asante kwa washiriki wote katika mashirika; asante kwa watu wengi wa kujitolea, asante kwa kila mmoja wa wale walioomba kwa ajili ya ziara hiyo. “Tafadhali ongeza sala moja zaidi, ili mbegu zilizotawanyika wakati wa Safari zizae matunda mazuri. Tuombe kwa hili”.

KATEKESI YA PAPA 22 SEPTEMBA
22 September 2021, 16:35