Tafuta

2021.09.22 Mkutano wa  Papa Makardinali kwa njia ya Mtandao. 2021.09.22 Mkutano wa Papa Makardinali kwa njia ya Mtandao. 

Mchakato wa Sinodi kiini cha Mkutano na Papa na Makardinali washauri

Papa Francisko na Makardinali washauri wamefanya mkutano wao kwa njia ya mtandao,kila mmoja na mahali pake.Hili ni Baraza la makardinali washauri wa Papa katika Kanisa la Ulimwengu ambao wanamsaidia kupyaisha katiba ya kitume'Pastor Bonus'.Wametumia muda mwingi kutazama mchakato wa Sinodi ijayo.Mkutano wao ujao utakuwa Desemba pamoja ikiwa hali halisi itaruhusu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Sinodi ambayo iko mbali na ukuhani na ugumu na ambayo inatoa nafasi ya kusikiliza na mtazamo wa kichungaji, ndiyo umakini na lengo la Papa, kwa ajili ya siku ya tarehe  9 na 10 Oktoba ijayo jijini Roma kuhusiana mchakato wa safari ya Sinodi. Na ndivyo Papa Francisko mwenyewe ametaka kusisitiza jana alasiri tarehe 21 Septemba 2021 wakati wa Mkutano wa Makardinali washauri. Kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Wanahabari ya Vatican saa 10.00  jioni, kupitia unganisho la mtandao katika Nyumba ya Mtakatifu  Marta, Vatican, Papa alifuatilia kazi ambazo walishiriki pamoja kwa kila mmoja akiunganishwa kutoka nchi yake anayoishi. Kardinali Óscar A. Rodríguez Maradiaga, S.D.B., Kardinali Reinhard Marx,  Kardinali Sean Patrick O’Malley, O.F.M. Cap., Kardinali Oswald Gracias na Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, O.F.M. Cap. Kutoka Vatican kinyume chake waliunganishwa Kardinali Pietro Parolin na Giuseppe Bertello, na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Monsinyo Marco Mellino.

Mkutano wa Papa na Makardinali washauri
Mkutano wa Papa na Makardinali washauri

Baada ya utangulizi mfupi kutoka kwa Kardinali Maradiaga ulifuatiwa na tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko juu ya ufunguzi wa kazi ya Sinodi mwezi Oktoba ijayo na ambayo itahitimishwa kama ilivyo andaliwa mjini Vatican mnamo 2023. Baada ya kupitia hotuba mbili zake ambazo zilibainishwa kama kitovu kweli cha wzo la Sinodi ujayo, ile ya mwaka 2015 katika kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu na ile ya hivi karibuni iliyoelekezwa kwa waamini wa Jimbo la  Roma Jumamosi iliyopita, Papa alifafanua jinsi ambavyo moyo wa tafakari ya kanisa, sio kuzidisha sana mada hii au mada hiyo na kwa maana hiyo ni kujifunza njia ya kuishi Kikanisa, iliyowekwa alama katika viwango vyote kwa kusikilizana na mtazamo wa kichungaji, hasa mbele ya vishawishi vya ukleri na ugumu.

Uteuzi ujao mnamo Desemba

Kwa upande wao, katika hatua za kibinafsi, taarifa kutoka Ofisi ya Wanahabari imethibitisha kuwa makadinali pia waligundua mambo kadhaa ambayo yanafanya safari ya sinodi kuwa muhimu sana katika nchi wanazotoka, ili kushinda udhehebu unaoibuka kila kuchao na masilahi ya vyama. Baada ya masaa mawili, mkutano ulimalizika na sasisho lingine linalotarajiwa kuhudhuriwa katika mkutano kwa uwepo wao wote ikiwa  hali itaruhusu, mnamo Desemba. 

22 September 2021, 17:42