Tafuta

2023.01.18 Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya watu waoteseka kwa namna ya pekee, Congo DRC, Nigeria na Ukraine. 2023.01.18 Papa Francisko ameomba kusali kwa ajili ya watu waoteseka kwa namna ya pekee, Congo DRC, Nigeria na Ukraine.  (Vatican Media)

Papa:Kusali kwa ajili ya Pd.Isaac,waathirika wa Congo&Ukraine

Baada ya katekesi yake,Papa amekumbuka Padre wa Nigeria aliyeuwa Dominika iliyopita,baadaye wazo kwa Congo DRC atakayotembelae mwishoni mwa mwezi huu kuhusiana na shambulizi.Ameomba kusali kwa Mungu aweze kutufanya kuwa na moyo wa kichungaji unaoteseka na kujitahatisha kutoa ushuhuda.Hakusahau watu wa Ukraine.

Na Angella Rwezaula: - Vatican.

Miili ilichomwa ikiwa hai, watu waliopigwa risasi, mabomu Makanisani, na mateso ya watu wasio na hatia. Ukatili juu ya ukatili unachukua sura tofauti katika sehemu mbalimbali za Afrika, lakini maumivu daima yanafafana tu. Baba Mtakatifu Francisko ametoa sauti yake mara baada ya katekesi yake Jumatano tarehe 18 Januari 2023 katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, kwa waamini na mahujaji ambapo akikumbuka "mateso ya ulimwengu huu amesema yuko karibu na waathrika wa mashambulizi, ambayo mara nyingi ni asili ya mateso, ambayo yamekuwa yakiumiza uso wa Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa miezi au siku, kama sio miaka", amesema

Wazo kwa ajili ya Kuhani wa Jimbo la Minna, Nigeria

Wakati wa salamu, zake vile vile Baba Mtakatifu ameomba kusali pamoja naye kwa ajili ya Padre Isaac Achi, Padre wa Jimbo la Minna, Kaskazini mwa Nigeria, aliyeuawa alfajiri ya Dominika 15 Januari katika nyumba ya Parokia hiyo na kundi la majambazi na waliomjeruhi mshirika wake Padre Collins nyuma ya mgongo wakati akijaribu kutoroka. Baada ya kushambulia Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro na Paulo, huko Kafin-Koro, katika eneo la Paikor, washambuliaji, kabla ya kukimbia wakati vikosi vya usalama vikiwa vinakaribia, walichoma nyumba kwa moto, na hivyo kumuua padre aliyekuwamo ndani ya nyumba hiyo walioshindwa kuingia ndani. Papa Francisko ameuliza: “Je ni Wakristo wangapi wanateseka kwenye ngozi zao wenyewe: tuwaombee! Nawaombea ninyi nyote na familia zenu amani ya Bwana Yesu.”

Maombi kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC

Mtazamo wa Papa bado ulendelea kuelekeza barani Afrika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  ambayo ataitembelea kuanzia  kuanzia Januari 30 ijayo katika hija kubwa ambayo pia atakwenda nchini Sudan Kusini. Hata nchi hiyo imeona watu wasio na hatia wakifa, mnamo Dominika tarehe 15 Januariiliyopita, katika shambulio lililodaiwa na IS katika kanisa la Kipentekoste huko Kasindi. Papa Francisko ahata hivyo tarehe 17 Januari alionyesha huruma na ukaribu kwa familia za waathrika  kupitia telegramu kwa Mchungaji André Bokundoa-bo-Likabe, rais wa Kanisa la Kristo katika nchi hiyo, kwa njia hiyo akisalimia mahujaji kwa lugha ya kifaransa na hasa akikumbuka hija yake ya kitume inayokaribia, alisali kwamba: “Tumwombe Mungu atupe moyo wa kichungaji unaoteseka na kuhatarisha kushuhudia. Sio tu heshima bali pia ni wajibu wa kupeleka  Neno la Mungu kwa wale tuliokabidhiwa na wale tunaokutana nao katika maisha yetu ya kila siku.”

Faraja na amani kwa Ukraine

Papa Francisko  vile vile amegeuzoamawazo yake kwa nchi ya  Ukraine iliyopigwa, huku akitoa wito kwa kila mtu kuwakumbuka watu katika sala zao kwani wanahitaji sana ukaribu wetu, faraja, na zaidi ya yote amani. Pia alikumbuka shambulio la hivi karibuni la  kombora lililotokea Jumamosi iliyopita tarehe 14 Januari kwa kuua na kujeruhi raia wengi, miongoni mwao wakiwemo watoto. Picha na ushuhuda wa kipindi hiki cha kutisha ni wito wenye nguvu kwa dhamiri zetu. Hakuna anayeweza kubaki sintofahamu, amesisitiza. Hata hivyo ripoti za vyombo vya habari zinasema zaidi ya watu 40 walifariki na wengine 75 kujeruhiwa katika shambulizi la kombora la Urussi lililogonga jengo la ghorofa katika mji wa Dnipro nchini Ukraine siku ya Jumamosi 14 Januari 2023. Makumi ya watu hawajulikani waliko na juhudi za kuwatafuta zinaendelea.

Papa aombea Congo,Nigeria na Ukraine
18 January 2023, 16:04