Tafuta

2023.01.19 Papa amekutana na Ujumbe  wa Kiekumene kutoka Finland katika fursa ya Siku kuu ya Mtakatifu Enrico Msimamizi wao. 2023.01.19 Papa amekutana na Ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland katika fursa ya Siku kuu ya Mtakatifu Enrico Msimamizi wao.  (Vatican Media)

Papa na wajumbe wa Finland:Kwa Ubatizo mmoja unatuwajibisha

Papa Francisko akikutana na wajumbe wa Kiekumene kutoka Finland katika fursa ya Siku Kuu ya Msimamizi wao Mtakatifu Enrico,amesisitiza juu ya thamani ya Wakristo wawe wahudumu wa Upatanisho kwa waathrika wa vita na wanaokandamizwa.Vile vile kujikita kwa pamoja katika kuponesha majeraha ya wahitaji.Ni Ubatizo mmoja katika huduma ya haki na ukaribu wa waliodhaifu.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 19 Januari 2023 amekutana mjini Vatican na Wajumbe wa Kiekumene kutoka Finland. Amewashukuru kwa sababu mwaka huu wamekuja Roma kuadhiimsha siku kuu ya Mtakatifu Enrico ikiwa na kiini zaidi cha kiekumene. Kwa njia hiyo ni furaha ya kuwakaribisha wawakilishi si tu wa kiluteri na wakatoliki, lakini hata Waorthodox na wametodi. Akimgeukia mchungaji wa kiluteri amemshukuru kwa maneno ya hotuba yake na kushukuru salamu za rambi rambi alizopkea kufuatia na kifo cha mtangulizi wake Papa Benedikto XVI. Ana utambuzi hata kile ambacho kimeelezwa kwa njia ya picha ya Bahari ya Baltic, chanzo cha uhai unaotishiwa na matendo ya kibinadamu, mahali pa kukutania panapoathiriwa kwa uchungu na hali ya makabiliano inayosababishwa na upumbavu mkali wa vita, kwamba vita daima ni kushindwa.

Papa amekutana na Ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland
Papa amekutana na Ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland

Akigusia juu ya hotuba yake kufuatia na suala la maji, ambayo alisema Wakristo tunaitambua kama  zawadi ya upatanisho uliopokelewa na Ubatizo Papa amekumbusha jinsi ambavyo muda si mrefu umefanyika Ubatizo wa Bwana. Mwana wa Mungu kwa kuingia kwenye maji ya Yordani, ulikuwa ni mwanzoni waa huduma yake ya umma   na ambayo ilidhihirisha nia ya kuzama kabisa katika hali yetu ya kibinadamu. Na sisi tuliobatizwa katika Kristo, kwa neema takatifu tulizamishwa ndani yake; Baada ya kupokea Ubatizo wa pekee, kama waamini, kwa hiyo, tunaitwa kushukuru kwa sababu, kuanzia maji ya Ubatizo, uwepo wetu umepatanishwa na Mungu, pamoja na wengine, na uumbaji. Sisi ni watoto waliopatanishwa na kwa hiyo tunaitwa kupatanishwa zaidi na zaidi kati yetu, na kuwa waendeshaji wa upatanisho duniani.

Papa amekutana na ujumbe wa kiekumene kutoka Finland
Papa amekutana na ujumbe wa kiekumene kutoka Finland

Inapendeza kuona haya yote katika Juma la Kuombea Umoja wa Kikristo. Ndani yake, tunakiri Imani ya Nikea  ya Constantinopoli pamoja, tunakiri ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi, lakini mwaka huu pia tunatafakari juu ya baadhi ya maneno yaliyotolewa katika kitabu cha nabii Isaya: “Jifunzeni kutenda mema, tafuteni haki.” (Isa 1:17). Hivyo tunasikia mwangwi wa Ubatizo wetu ambao unatuita, kama tumehesabiwa haki kwa neema, tutende kazi za haki bila malipo, na kufanya ishara thabiti za ukaribu na wale ambao ni waathirika wa dhuluma, kukataliwa, na vile vile aina mbalimbali za ukandamizaji na zaidi ya yote vita. Kama shuhuda  wa imani katika Kristo, ambaye alijizamisha katika udhaifu wa hali yetu ya kibinadamu, kwa hiyo tunatakiwa kuzama katika majeraha ya wahitaji. Na kuifanya pamoja.

Ujumbe wa Kiekuemene kutoka Finland wakiwa Roma kusheherekea siku kuu ya Mtakatifu Enrico.
Ujumbe wa Kiekuemene kutoka Finland wakiwa Roma kusheherekea siku kuu ya Mtakatifu Enrico.

Baba Mtakatifu amesema katika jumuiya ya wabatizwa wote, tunajua ya kuwa ni kwa kuungana kati yetu, hapa na sasa kwa kila dada na kaka katika Kristo, lakini hata mama zetu na baba zetu katika imani ambao waliishi awali kabla yetu. Kutoka  na umoja  kamili wa Mbingu wanatutazama na kutualika kutembea pamoja katika dunia  hii. Mtakatifu Enrico, shuhuda wa imani na mjumbe wa tumaini na chombo cha upendo ni mmoja kati yao. Pamoja naye tunaadhimisha ushirika wa kiekumene wa watakatifu wote, wanaojulikana na wasiojulikana, waliozaliwa upya kwa maisha mapya kutoka kwa maji ya Ubatizo. Kwa maana hiyo tunaweza kukumbatia wakati huo kwa mtazamo wa neema asili ya Ubatizo na mtazamo wa maisha ya milele; kisima cha maisha ambayo duniani tumetufanywa kuwa wana wa Mbingu na Mbingu mahali ambapo watakatifu wanatusubiri na kututia moyo. Katika kila jambo, tunatambua jinsi umoja unaotuunganisha ulivyo mkuu na jinsi ilivyo muhimu kusali pamoja, kufanya kazi kwa bidii na mazungumzo kwa bidii ili kushinda migawanyiko na kwa mujibu wa  mapenzi ya Bwana, kuwa na umoja katika ushirika wa Utatu hadi  ulimwengu uamini ( Yh 17,21).

Hakika tunafahamu hili, lakini ufahamu pekee hautoshi. Inahitajika kukuza shauku ya kweli, shauku inayobubujika kutoka katika upendo wa ushirika, kutoka kwa hamu ya kushinda ushuhuda wa kupingana kutokana na migawanyiko ya kihistoria kati ya Wakristo, ambayo imeumiza sana umoja wa Mwili wa Kristo. Leo hii zaidi ya yote, ari ya bidii ya uinjilishaji inahitajika, kwa sababu kwa kutangaza pamoja tunajitambua upya kama kaka na dada; na kwa sababu tunatambua kwamba hatuwezi kueneza ipasavyo jina la Yesu, aliyezaliwa, akafa na kufufuka kwa ajili ya wote, bila kutoa ushuhuda wa uzuri wa umoja, ishara ya pekee ya wanafunzi wake.

Papa amekutana na Ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland
Papa amekutana na Ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland

Baba Mtakatifu Francisko wakati akipyaisha tena shukurani zake  kwa ziara yao ya kila mwaka, inayosubiriwa na kukaribishwa kila wakati, amependa kuomba pamoja zawadi ya shauku hiyo kubwa kwamba  wasichoke kupenda, kutumaini, kutafuta walio mbali, kuungua ndani kwa hamu ya kumtangaza Yesu na kujenga umoja ambao anautamani sana. Tunaomba zawadi ya ari mpya ya kitume, ambayo inatufanya tugundue tena kila wakati wamini wengine kama kaka na dada zetu katika Kristo, ambayo inatufanya tujisikie kama mitume waliopatanishwa na Mungu ili kupatanisha kati yetu na kuwa wasanii wa upatanisho kwa ulimwengu.  Kwa maana hiyo amependa kuwaalika kumkri Baba Yetu pamoja, sala ya watoto ambayo, bora kuliko nyingine yoyote, inadhihirisha ukweli wa Ubatizo wetu. Tunaweza kila mmoja kuiomba kwa lugha yake, lakini kwa pamoja: sisi kwa sisi na na kwa wote, kwa hiyo amehitimisha Baba Mtakatifu kwa kuomba kusali sala ya Baba Yetu Uliye Mbinguni kwa kila mmoja katila lugha zao.

Hotuba ya Papa kwa Ujumbe wa Kiekumene kutoka nchini Finland
19 January 2023, 16:05