Tafuta

Tuzo ya Zayed,Papa:tunaitwa kukuza utamaduni wa amani,mazungumzo&mshikamano

Katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya toleo la 2023,Papa Francisko ametuma ujumbe kwa video,anashukuru kwa mpango huo na kuwatia moyo ambao wamejitolea kujenga maelewano na amani na kuthibitisha tena jukumu la kuamua la dini katika kuishi pamoja kwa watu kubadilisha mtu kutoka ndani.Kardinali Ayuso alikuwepo na walisoma ujumbe wa rais Joe Biden wa Marekani.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Huko Abu Dhabi, nchi za Falme za Urabuni, mnmao tarehe 4 Februari, 2023 ilifanyika afla ya kutoa Tuzo ya Zayed 2023 kwa ajili ya Udugu wa kibinadamu kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na mwanaharakati wa amani wa Kenya “Mama Shamsa”.  Katika Alfla hiyo iliona  hotuba ya Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano ya  Kidini, na rais msaidizi wa Kamati Kuu ya  Udugu Kibinadamu hata kwa kumwakilisha Kardinali Tagle, mjumbe wa Uamuzi wa Tuzo ya  Zayed  aliyekuwa anaambatana na Ziara ya PapaFrancisko huko DRC na Kusini Mwa Sudan. Katika hafla hiyo ujumbe kwa njia ya  video kutoka kwa Papa Francisko ulitangazwa na  vile vile kusomwa ujumbe kuotoka kwa  Rais wa Marekani, Bwana Joe Biden kwa ajili ya Siku ya III ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu iliyoanzishwa mnamo  tarehe 4 Februari 2019. Ujumbe kwa njia ya video wa Papa umefika katika  miaka minne hasa baada ya kusainiwa kwa Hati ya Udugu wa binadamu kwa ajili ya amani uliwenguni  na kuishi kwa pamoja kwa dhati huko Abu Dhabi pamoja na Imamu Mkuu Ahmed Al-Tayyeb.

Wajibu wa kidini katika kuishi pamoja kwa amani

Hati hiyo inasisitiza wajibu wa dini katika kuishi pamoja kwa amani kati ya watu na hata kama njia ni ndefu, inathibitisha imani kwamba inawezekana. Papa Francisko akisalimiana na Imamu Mkuu kwa upendo na shukrani Sheikh Mohammed bin Zayed, muundaji wa tuzo hiyo, na wale wote wanaojitolea kwa njia mbalimbali katika kuunga mkono udugu alisema, tunaitwa kukuza utamaduni wa amani, mazungumzo na mshikamano, sote tunatamani kuishi kama ndugu na ukweli kwamba mara nyingi hii haifanyiki  ambapo kwa bahati mbaya tunazo dalili kubwa kuhusu hilo na hivyo inapaswa kuchochea hata zaidi kutafuta udugu. Papa akiendelea  katika ujumbe wake alisema: “Ni kweli kwamba dini hazina nguvu ya kisiasa ya kulazimisha amani, lakini kwa kumbadilisha mwanadamu kutoka ndani, kumwalika kujitenga na maovu, zinamwongoza kuelekea mtazamo wa amani. Kwa hivyo, dini zina jukumu la kuamua katika kuishi pamoja kwa watu: mazungumzo yao yanasuka njia ya amani, inakataa jaribu la kusambaratisha mfumo wa kiraia na inaweka huru kutoka kwa unyonyaji wa tofauti za kidini kwa malengo ya kisiasa”.

Dini zifanye mazungumzo kati yao na kukuza ushirikiano

Baba Mtakatifu Francisko aidha alisisitiza haja ya dini mbalimbali kufahamiana na kufanya mazungumzo kati yao na kukua kwa ushirikiano kwa manufaa ya wote. Kwa pamoja wanaweza kuchangia mengi kwa udugu: “Ikiwa tunaweza kuonyesha kwamba inawezekana kuishi tofauti katika udugu, tutaweza kujikomboa wenyewe kidogo kidogo kutoka katika woga na kutoaminiana kwa mwingine ambaye ni tofauti na mimi. Kukuza utofauti na kuoanisha tofauti si mchakato rahisi, lakini ndiyo njia pekee yenye uwezo wa kuhakikisha amani thabiti na ya kudumu, ni dhamira inayotuhitaji kuimarisha uwezo wetu wa kufanya mazungumzo na wengine.” Kila mkutano kati ya dini, mara kwa mara katika ulimwengu ambapo kila kitu kinazidi kuunganishwa, kinaweza kuwa tukio la makabiliano, alisema Papa, au kwa ajili ya kutiana moyo kusonga mbele kama kaka na dada. Ndugu wapendwa, tunafahamu kwamba safari ya udugu ni safari ndefu na ngumu. Dhidi ya migogoro mingi, dhidi ya vivuli vya ulimwengu uliofungwa, tuisimamie ishara ya udugu!

Amani inahimiza kukaribisha wengine na kuheshimu utambulisho wao

Amani inahimiza kuwakaribisha wengine na kuheshimu utambulisho wao, inatuhimiza kufanya kazi kwa imani kwamba inawezekana kuishi kwa maelewano na amani. Ninawashukuru wale wote ambao watajiunga na njia yetu ya udugu, na ninawahimiza kujitolea kwa ajili ya amani na kujibu matatizo na mahitaji halisi ya maskini, wasio na ulinzi, wale wanaohitaji msaada wetu. Hata Tuzo ya Zayed ya Udugu wa Kibinadamu pia inakwenda katika mwelekeo huo, Papa aliendelea na kuhitimisha kwa kuwashukuru washindi wa toleo hilo ambao ni Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Mkenya Shamsa Abubakar Fadhil kwa kazi yao na ushuhuda wao.

Ayuso Guixot:tujenge udugu wa kibinadamu pamoja

Kwa upande wa Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini alisema “ Sisi ni raia wa ubinadamu, sisi ni waamini wa tamaduni mbalimbali za kidini na pia watu wenye mapenzi mema. Kufuatia ushuhuda wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, inayohudumia wanadamu kila siku, sisi sote tukiwa wajumbe wa amani na wajenzi wa ushirikiano, tunajenga mshikamano wa kibinadamu kwa pamoja ili kuponya majeraha ya ubinadamu”. Shamsa Abubakar Fadhil pia alitunukiwa mwaka huu na Kadinali alisema  kuwa yeye ni mwanamke aliyechukua kwa uzito na binafsi wito wa Waraka juu ya udugu wa kibinadamu wa kulinda hadhi ya vijana.

Rais Biden: fursa ya kufanya upya ahadi yetu

Katika taarifa yake, Rais Joe Biden wa Marekani  alisema jinsi anavyojivunia kuungana na watu ulimwenguni kote  kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Akiendelea kuandika “Kwa kila kizazi tunaitwa kupigana na moto wa chuki ambao umepewa oksijeni nyingi kwa muda mrefu sana. Ni lazima tupande mbegu za udugu kati ya watu wote, dini na imani. Aidha alisisitizia  umuhimu wa ujuzi wa pamoja na mazungumzo na watu wa asilia, tamaduni na imani zote. “Siku ya leo ni tukio, la kufanya upya juhudi zetu za kuwatunza wahitaji, kuomba amani, haki na uhuru kwa kila mtu, kila mahali. Na ni wakati wa kusherehekea ujasiri wa maadili wa viongozi wa kidini na  wa wengine wanaoendelea kushirikiana kwa manufaa ya wote.”

Washindi wawili wa toleo la Zayed la 2023

Kuhusiana na washindi wa Toleo hilo la Mwaka wa III, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambalo kwa hakika ni harakati ya kikanisa yenye  makao yake makuu mjini Roma, ambayo ilipokea tuzo hiyo kwa mchango wake katika mazungumzo ya amani na utatuzi wa migogoro katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini pia kwa kujitolea kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi kupitia mikondo ya  kibinadamu, ambayo inawaruhusu watu na familia kuondoka makwao ili kufikia nchi za Ulaya  wakiwa salama. Shamsa Abubakar Fadhil anayejulikana kama “Mama Shamsa” ni mwanaharakati na mpenda amani nchini Kenya. Alitunukiwa Tuzo ya Zayed kwa kuwasaidia vijana katika nchi yake kwa kuwaokoa kutokana na vurugu, uhalifu na itikadi kali na kwa kampeni zake katika bara la Afrika za kukuza ufahamu wa umma kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Ujumbe wa Papa kwa njia ya vido katika Siku III ya kimataifa ya Udugu wa kibinadamu
06 February 2023, 15:56