Tafuta

Papa Leo XIV akutana na Jannik Sinner,bingwa wa tenisi!

Wakati mashindano ya Wazi ya Italia ya 2025 yakiendelea jijini Roma,Jumatano tarehe 14 Mei 2025 Papa Leo XIV alikutana na mchezaji wa tenisi na bingwa Jannik Sinner mjini Vatican pamoja na familia yake na rais wa Shirikisho la Tenisi nchini Italia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku ya Jumatano, tarehe 14 Mei 2025 Papa Leo XIV alikutana na  bingwa wa tenisi Jannik Sinner mjini Vatican. Kwa mujibu wa Ofisi ya Wanahabari ya Vatican, ilibainishakuwa akutana na waliokuwapo kati ya Papa na mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 waliojumuisha familia ya Sinner na Rais wa Shirikisho la Tenisi la Italia, Bwana Alberto Binaghi. Mkutano huo ulifanyika katika vyumba vilivyounganishwa na Ukumbi wa Paulo wa VI, mjini Vatican.

Papa na Bingwa wa Tenisi
Papa na Bingwa wa Tenisi   (ANSA)

Msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni kwa waandishi wa habari alisema kuwa: “mapenzi ya Papa Leo XIV ya kucheza tenisi yanajulikana sana.” Kwa hiyo katika video hiyo, bingwa Sinner anaonekana akimpatia Papa mpira wa tenisi na kumuuliza kama alitaka kucheza. Lakini Papa alijibukwamba: "Hapa tutavunja kitu. Bora tusifanye!"

Bingwa alimuuliza kama Papa anataka kujaribu kucheza
Bingwa alimuuliza kama Papa anataka kujaribu kucheza   (ANSA)

Michuano ya Wazi ya Italia ya mwaka 2025, inayojulikana rasmi kama ‘Internazionali BNL d'Italia,’ kwa sasa inaendelea mjini Roma katika Eneo la michezo liitwalo ‘Foro Italico’. Mashindano haya ya kifahari ya tenisi, ni sehemu ya ATP na WTA 1000, yaliyoanza tarehe 7 Mei 2025 na yatakamilika tarehe 18 Mei 2025. Wachezaji wakuu wa kimataifa na Italia wanachuana kwenye hafla hiyo.

Mkutano wa Papa na Bingwa wa Tenisi wa Italia katika Ukumbi mdogo wa  Paulo VI
Mkutano wa Papa na Bingwa wa Tenisi wa Italia katika Ukumbi mdogo wa Paulo VI   (ANSA)
14 Mei 2025, 15:53