Tafuta

2025.07.31 Mtakatifu Kardinali  John Henry Newman atakuwa Mwalimu wa Kanisa. 2025.07.31 Mtakatifu Kardinali John Henry Newman atakuwa Mwalimu wa Kanisa. 

Mtakatifu John Henry Newman atakuwa Mwalimu wa Kanisa la Ulimwengu!

Papa Leo XIV,tarehe 31 Julai 2025 alilidhia maoni ya Kikao cha Mkutano Mkuu wa Makardinali,Maaskofu na Wajumbe wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu kuhusu Jina la kupewa Mwalimu wa Kanisa la Ulimwengu ambalo Kardinali Newman atapew hivi karibuni.

Vatican News.

Tarehe 31 Julai 2025, Baba  Mtakatifu Leo XIV amekutana na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu. Katika mkutano huo Papa alithibitisha na kukubaliana na maoni thabiti ya Kikao cha Mkutano Mkuu wa Makardinali, Maaskofu na  Wajumbe wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu kuhusu Jina la kupewa  Mwalimu wa Kanisa la Ulimwengu ambalo  hivi karibi atapewa Mtakatifu Kardinali  John Henry Newman,  wa Kanisa Takatifu la Roma, na Mwanzilishi wa Kituo cha Mtakatifu  Filippo Neri  nchini Uingereza. Alizaliwa huo Londan, Uingereza, kunako tarehe 21 Februari 1801 na kifo chake huko Edgbaston, Uingereza kunako tarehe 11 Agosti 1890.

Papa: Kardinali Newman ni mwalimu wa Kanisa
31 Julai 2025, 18:02