Tafuta

Heri ya Kuzaliwa kwa Papa Leo XIV

Katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa papa leo XIV tarehe 14 Septemba 2025,heri nyingi kutoka kila kona ya dunia imemfikia,mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa aliwashuru wazazi wake na wale wote waliomtakia matashi mema.

Vatican News

Salamu za matashi mema ya siku ya kuzaliwa zimemiminika kutoka ulimwenguni kote kwa  ajili ya Baba Mtakatifu Leo XIV, ambaye ametimiza miaka 70,  tarehe 14  Septemba 2025. Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, alimpatia "kwa niaba ya watu wa Italia, pamoja na matashi mema yake ya dhati kwa ajili ya ustawi wake wa kiroho na wa kibinafsi. Katika ujumbe wake, Mkuu wa Nchi hiyo aliakisi "maombi makubwa" ya Papa "ya kusitishwa kwa mapigano na kurudi kwenye njia ya mazungumzo, kwa manufaa ya watu wote," wakati ambapo "kuna hofu inayoongezeka kwamba ulimwengu unaelekea kwenye mteremko hatari, unaochochewa na mantiki iliyoenea ya ukandamizaji na inazidi kuwa alama ya migogoro inayozidi."

Kwa kwa mkuu huyo wa Italia anabainisha kwamba: "Wale wanaolipa bei isiyovumilika ya kila siku ya damu na uharibifu  juu ya yote, maelfu ya waathirika wa kiraia, katika hali ya wasiwasi kama huo, ni wanawake na wanaume wenye mapenzu mema ambao  anaweza kuhisi haraka hitaji la amani na haki" na kwamba "kila bara linatazama kwa tumaini la dhati" kwa maneno ya Papa. Rais wa Jamhuri ya Italia, akimnukuu Mtakatifu Agostino, ambaye alisema kwamba "sisi ni nyakati," alisisitiza kwamba ni juu ya kila mtu, "na hasa wale walio katika ofisi ya umma," kujitolea "kuhakikisha kwamba hali inaboreshwa, kufungua tena upeo wa mazungumzo, haki, na ulinzi thabiti wa utu wa kila mtu," na alimhakikishia  Papa Leo XIV  ushirikiano wa hali halisi  ya Italia na  katika "ushirikiano wa kitume."

Kila la heri kutoka Baraza la Maaskofu wa Italia

Na  Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) limemuelekeza Papa "matashi ya dhati ya Makanisa yote nchini Italia," pamoja na sala "za sifa na shukrani kwa ajili ya huduma yake." Wakimshukuru Papa "kwa ajili ya roho ya ubaba" ambayo "inamsindikiza  na  "kuhimiza" Kanisa la Italia, maaskofu hao wanaungana naye "kuombea 'kupokonywa silaha na amani" katika hali zote za migogoro ambayo ilimwaga damu maeneo makubwa ya sayari. Wanaendelea kuwa: "karibu na watu wanaoteseka kupitia vitendo vya mshikamano na kukuza binadamu," na wanatumaini "kwamba umoja wa kusudi, sauti, na sala ambazo hutolewa kutoka ulimwenguni kote kuomba suluhisho za amani zinaweza kusikilizwa hivi karibuni.

Upendo wa Jimbo Kuu la  Roma

"Katika siku yako ya kuzaliwa, Jimbo lako lote linaungana nawe kumshukuru Baba kwa zawadi ya uhai,." Ndivyo ujumbe kutoka kwa Kardinali Vicar Baldassare Reina, Makamu wa Papa Jimbo Kuu la Roma kwa niaba ya Jimbo la Roma anaandika. "Sala na upendo wetu zikufikie kwa yote unayofanya kila siku, kwa kujitolea bila kuchoka, katika huduma ya Kanisa la ulimwengu wote, kuanzia Kanisa la Roma," Kardinali aliendelea. Pamoja na Jimbo la  Roma, tukishiriki wasiwasi wa Papa, "hasa ​​kwa ajili ya vita vingi vilivyomwaga damu ulimwenguni," na kueleza  tumaini "kwamba tunaweza kufikia shauku za moyo wako na kuendelea kupanda tumaini kwa wanaume na wanawake wa wakati wetu."

Michoro kutoka kwa wadogo wa Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù

Michoro mingi ilitumwa kwa Papa na wagonjwa wadogo wa Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù, ambao katika chumba cha kucheza cha hospitali waliacha mawazo yao ya rangi tofauti ili kumtakia Papa Leo XIV "heri ya kuzaliwa." Katika ubunifu wao wa kupendeza, watoto wanarudia matashi ya Papa ya amani kwa ulimwengu mzima, yaliyooneshwa tangu siku ya kuchaguliwa kwake, kwa mawazo yao. Wakiwa na uhakika kwamba Papa anaweza kuwa mtu sahihi wa kupata njia sahihi ya mazungumzo, mchoro unaonesha Papa Leo akitangaza, "Usijali, nitalishughulikia," akipeperusha bendera ya amani, kati ya njiwa mwenye tawi la mzeituni na Basilika ya Mtakatifu Petro, iliyopakwa rangi nyeupe na njano kama bendera ya Vatican. "Tunakupenda sana, Papa Leo wa Kumi na Nne," ni kukumbatia kwa uchangamfu wa watoto wa Bambino Gesù waliotuma Ujumbe kwa Papa katika siku yake ya kuzaliwa.

Matashi mema ya kuzaliwa kwa Papa 14 Septemba

 

14 Septemba 2025, 11:38