Jubilei ya Faraja:Papa Leo XIV ataongoza Mkesha wa Sala,Spetemba 15
Vatican News
Mkesha wa Sala, utakaoongozwa na Papa Leo XIV saa 11:00 Jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican ambao utakuwa wakati muhimu wa Jubilei ya Faraja, inayotarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo, tarehe 15 Septemba 2025. Tukio hili maalum la Mwaka Mtakatifu litakalojitolea kwa wale wote ambao wanapitia, au wamepitia, nyakati za shida fulani, huzuni, mateso, au umaskini katika maisha yao.
Ushuhuda kutoka kwa Diane Foley na Lucia Di Mauro Montanino.
Liturujia ya Neno, iliyojikita katika mfano wa Msamaria Mwema, kutoka Injili ya Marko (Mk 10:25-37)itasoma na itafuatiwa na ushuhuda kutoka kwa wanawake wawili, Diane Foley, kutoka Marekani, na Lucia Di Mauro Montanino, kutoka Napoli, nchini Italia. Foley anazunguka dunia, akisimulia historia ya upatanisho na msamaha kupitia nguvu ya imani, pamoja na Alexanda Kotey, mwanachama wa kundi la wanajihadi waliomuua mwanawe, mwandishi wa habari James Wright Foley, nchini Syria mwaka wa 2014. Picha za kukatwa kichwa kwake kikatili zilinakiliwa na kusambazwa mtandaoni na wauaji wake. Mnamo Agosti 29, alipokelewa mjini Vatican na Papa, pamoja na mwandishi Colum McCann, ambaye alijitolea kuandika kitabu kuhusu tukio hilo.
Kutoka kwa Maumivu hadi Kuzaliwa Upya
Ushahidi wa pili utatolewa na Lucia di Mauro Montanino, ambaye atasimulia jinsi alivyobadilisha maumivu ya mauaji ya mumewe, Gaetano aliyekuwa mlinzi aliyeuawa mnamo tarehe 4 Agosti 2009, na vijana kadhaa wakati wa jaribio la wizi, na kuzaliwa upya, kupitia kukutana na kuandamana na Antonio, mmoja wa vijana walioshiriki katika shambulio hilo. Baada ya shuhuda hizo, Papa atatoa hotuba yake mbele ya watakaoudhuria.
Sanamu ya Mama yetu wa Tumaini
Wakati wa Mkesha huo, sanamu ya Mama yetu wa Matumaini, kutoka Parokia-takatifu ya Battipaglia, iliyooneshwa hapo awali katika Kanisa la Mtakatifu Petro wakati wa kipindi cha Noeli itakuwepo katika Kanisa Kuu la Vatican. Kisha kila mshiriki atapokea Agnus Dei, medali ya nta inayoonesha Mwanakondoo wa Pasaka, ishara ya ufufuko na ishara ya matumaini, ambayo itabarikiwa na Papa. Kwa upande mwingine wa sarafu, uwakilishi wa Maria Salus Populi Romani, mpendwa kwa jiji la Roma.
Hija ya Mlango Mtakatifu
Mkesha huo utatanguliwa na hija kwenye Mlango Mtakatifu wa Kanisa kuu la Vatican, iliyotafanyika tarehe 12 Septemba kati ya saa 2:00 asubuhi hadi saa 6 mchana. Zaidi ya watu 8,500 wanatarajiwa kushiriki kutoka duniani kote, hasa kutoka Italia, Ujerumani, Poland, Hispania, Marekani, Canada, Brazili, Mexico, Colombia, Argentina, Peru, Bolivia, na Australia.
Zaidi ya washiriki 8,500
Mashirika mengi, yaliyowekwa wakfu, na mashirika ya kitawa yaliyojitolea kusaidia wale wanaohitaji usaidizi na utunzaji pia yamehusika. Hizi ni pamoja na Jumuiya ya "Figli in Cielo", ambayo hutoa programu kwa familia ambazo zimepoteza mtoto au mpendwa mapema; Nyumba ya Familia ya Paolo VI, ambayo inakaribisha familia zinazohamia Roma kwa matibabu ya saratani ya watoto wao bila malipo; Chama cha Villa Maraini, ambacho hutoa matibabu kwa wale wanaokabiliwa na utumiaji wa dawa za kulevya, matumizi mabaya ya pombe, kamari, na aina mpya za matumini kama vile teknolojia, na kuunga mkono urekebishaji wa magereza; Chama cha Italia cha Wahanga na Majeruhi wa Ajali za Barabarani - shirika lisilo la kiserikali, ambalo hutoa msaada wa kisaikolojia na kiutawala kwa familia za waathiriwa; na Jumuiya ya Scintille di Speranza, iliyoko kwenye Makaburi ya Laurentino huko Roma, ambayo inasaidia wale ambao wamepoteza familia zao.
Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Jumuiya ya Huruma ya Mungu
Washiriki pia watakuwepo kwenye Kongamano la kwanza la Kitaifa la Jumuiya ya Huruma ya Kimungu, lililopangwa kufanyika Dominika, Septemba 14 na Jumatatu, Septemba 15, huko Roma. Ikidhaminiwa na Barza la kipapa la Uinjilishaji na kuandaliwa na uratibu wa kitaifa wa Huruma Italia, shirika linaloongozwa na Padre Pasqualino di Dio, tukio hilo litaitwa "Kupenda, Kutumaini, Rehema. Barabara Iliyo Wazi kwa Mungu" na itaandaliwa Dominika na Fraterna Domus huko Sacrofano, na Jumatatu na Kanisa la Roho Mtakatifu huko Sassia.
Wazungumzaji katika hafla hiyo ya siku mbili ni pamoja na wataalimungu Padre Fabio Rosini na Padre Luigi Epicoco. Hatimaye, Maadhimisho mawili ya Ekaristi Takatifu yamepangwa: Tarehe 14 saa 12:00 Jioni, Kardinali Angelo De Donatis, Mkuu wa Idara ya Toba, ataongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa Sheria ya Ukabidhi wa Moyo Safi wa Maria, na siku inayofuata saa 7:30 Kardinali Angelo Comastri, Mkuu Mstaafu wa Kanisa Kuu la Vatican. "Uratibu wa kitaifa wa vyombo vyetu," anasema Padre Pasqualino, "hauna lengo la kuwa Baraza linaloongoza, bali huduma ya ushirika" ili "kukuza utamaduni wa huruma!"
