Kuhusu Gaza,Papa Leo XIV:Lazima tupate suluhisho lingine
Vatican News.
Ilikuwa yapata saa 2:30 hivi usiku wa Jumanne tarehe 16 Septemba 2025 kukiwa tayari kumefifia na giza limeingia, milango ya Villa Barberini kando ya ziwa la Castel Gandolfo ilifunguliwa, na ikawa ishara kwa waandishi wa habari waliokuwa wakisubiri nje kwamba Papa sasa anaondoka. Na hivyo, kabla ya kuingia kwenye gari lake, kwa namna ambayo inakaribia kuwa mazoea, Papa Leo XIV alisalimia vipaza sauti vya magazeti na watangazaji mbalimbali kwa tabasamu na kujibu maswali machache, huku umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika wakipiga makofi na kumshangilia “Viva il Papa .”
Wasiwasi kwa watu wa Gaza
Mwandishi wa habari alisikika akiuliza: Kuhama kwa watu huko Gaza, umeona wangapi wanakimbia...?" Papa alithibitisha kuwa alizungumza kwa njia ya simu na Jumuiya ya Gaza na Padre wa parokia hiyo na kueleza hofu yake. "Wengi," alisema, "hawana pa kwenda, na hivyo ni jambo la kuhangaisha. Pia nilizungumza na watu wetu huko, pamoja na Padre wa Parokia. Kwa sasa, wanataka kubaki; bado wanapinga, lakini kiukweli tunahitaji kutafuta suluhisho lingine."
NATO haikuanzisha vita
Alipoulizwa kuhusu madai ya Kremlin ya vita vya NATO na Urusi, Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba "NATO haikuanzisha vita. Wapoland wana wasiwasi kwa sababu wanahisi anga lao limevamiwa; ni hali ya wasiwasi sana." "Kuna wasiwasi mwingi," alifichua.
Waamini wamtakia Papa heri ya kuzaliwa
Nyimbo kadhaa za za kumtakia matashi mema ya furaha ya Siku ya Kuzaliwa na Siku ya Somo wake, ambayo inayoadhimishwa Septemba 17, katika Kumbukumbu ya Mtakatifu Robert Bellarmine, zilisikika kabla ya Papa kuondoka kwa gari. Pia walimsindikiza na shada la maua na kadi kutoka kwa kikundi cha waamini wa Poland. Papa Leo XIV alihitimisha siku kali ambayo mada za amani, nguvu ya sala, na pia wasiwasi juu ya vita vilitawala mkutano wa kwanza wa asubuhi hiyo na Patriaki Karekin II, Mkuu wa Wakatoliki wa Waarmenia Yote, na mazungumzo ya simu na ParokoPadre Gabriel Romanelli wa Familia Takatifu huko Gaza.
