Maadhimisho ya Kipapa kwa mwezi Novemba hadi Januari 2026
Vatican News
Kuanzia tangazo la Newman kuwa Mwalimu wa Kanisa" mnamo Novemba 1 hadi ubatizo wa watoto kadhaa katika Kikanisa cha Sistine mjini Vatican mnamo tarehe 11 Januari 2026, ni katika taarifa ya Ofisi ya Maadhimisho ya Kiliturujia ya Kipapa iliyochapisha kalenda ya maadhimisho yatakayoongozwa na Papa Leo XIV katika miezi ya Novemba, Desemba na Januari.
Kwanza kabisa ni Misa ya saa 4:30 asubuhi, masaa ya Ulaya katika Uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 1 Novemba 2025 katika Maadhimisho ya Watakatifu Wote, kwa ajili ya kukabidhiwa wadhifa wa “Mwalimu wa Kanisa -iliyotangazwa tangu Julai 31 iliyopita kuhusu Mtakatifu John Henry Newman, aliyetangazwa kuwa mwenyeheri kwa mara ya kwanza na Papa Benedikto XVI mnamo tarehe 19 Septemba 2010 na baadaye Papa Francisko akamtangaza kuwa Mtakatifu, kunako tarehe 13 Oktoba 2019. Papa Leo XIV alitangaza tarehe hiyo, ambayo iko ndani ya Muktdha wa Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 28 Septemba 2025.
Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Papa Francisko na Makardinali na Maaskofu waliofariki, itafanyika Jumatatu, tarehe 3 Novemba 2025, ambapo Baba Mtakatifu anatarajia kuongoza misa Takatifu saa 5:00 asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kumwombea mtangulizi wake Papa Francisko, makadinali na maaskofu waliofariki mwaka huu 2025. Tarehe 9 Novemba, maadhimisho ya kuwekwa wakfu kwa Kanisa kuu la Laterano, ambapo Misa itaadhimishwa 9:30 alasiri huko Mtakatifu Yohane Laterano.
Dominika tarehe 16 Novemba, Ibada ya misa imepangawa saa 4.00 asubuhi masaa ya Ulaya katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Jubilei ya Maskini. Sherehe ya mwisho iliyopangwa kufanyika mwezi huo itakuwa ni tarehe 23 Novemba 2025, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4:30 asubuhi, kwa ajili ya maadhimisho ya Bwana Wetu Yesu Kristo, Mfalme wa Ulimwengu. Siku hiyo hiyo itaangukia maadhimisho ya Jubilei ya Kwaya na wanakwaya
Heshima kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili
Katika ratiba ya Maadhimisho yaliyotangazwa, pia ni kwamba Papa Leo XIV, ataendeleza mapokeo ya watangulizi wake, ambapo atakwenda katika Uwanja wa Hispania, Roma kwenye siku kuu ya Bikira Mtakatifu Mkingiwa Dhambi ya Asili tarehe 8 Desemba 2025 saa 10 jioni, masaa ya Ulaya ili kutoa heshima kwa Mama Maria.
Tarehe 12 Desemba saa 10:00 jioni inatazamiwa Misa Takatifu kwa ajili ya kumbukumbu ya Bikira wa Guadalupe kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Vatican. Pia katika Kanisa la Mtakatifu Petro, siku mbili baadaye, tarehe 14 Desemba, Papa ataongoza maadhimisho ya Jubilei ya Wafungwa, saa 4.00 kamili asubuhi.
Ibada za Noeli
Sherehe za Noeli pia zimethibitishwa. Misa hiyo ni pamoja na Misa ya Usiku wa manane katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tarehe 24 Desemba 2025 saa 4:00 usiku a dirisha kuu la Basilika ya Mtakatifu Petro.
Tarehe 31 Desemba 2025, kuelekea Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu, Papa ataongoza Masifu ya Jioni na Te Deum katika kutoa shukrani kwa mwaka uliopita saa kumi na moja jioni. Tarehe 1 Januari 2026, Misa kwa ajili ya Siku ya 59 ya Amani Ulimwenguni itafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 4.00 asubuhi.
Kufungwa kwa Jubilei
Mwaka 2026 katika Maadhimisho ya Tokeo la Bwana (Epifania,) Januari 6, utafungwa Mlango Mtakatifu, kuashiria hitimisho la Jubilei ya Kawaida ya 2025. Ibada hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Petro itafanyika saa 3:30 asubuhi, ikifuatiwa na Misa Takatifu.
Sherehe ya mwisho iliyopangwa kufanyika tarehe 11 Januari 2025 ni, Sherehe ya Ubatizo wa Bwana, itakayofanyika saa 3:30 asubuhi masaa ya Ulaya. Papa Leo XIV ataadhimisha Misa katika Kikanisa cha Sistine ambapo pia watabatiza watoto kadhaa.
