Papa kwa Wanaindonesia:kuwa manabii wa ushirika katika Ulimwengu unaotaka kugawanya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican , Jumatatu tarehe 22 Septemba 2025 na Jumuiya ya Wakatoliki wa Indonesia inayoish iRoma katika hotuba yale alifurahi kukutana nao wakati tunapoadhimisha matukio mawili maalum: ukumbusho wa kwanza wa ziara ya upapa nchini Indonesia na miaka sabini na mitano ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Indonesia na Vatican. Tangu mwanzo kabisa, Vatican imetembea pamoja na taifa lao, ikitambua uhuru wake mara baada ya kuzaliwa kwake. Katika miongo hii, vifungo vimejengwa juu ya mazungumzo, heshima, na kujitolea kwa pamoja kwa amani na maelewano.
![]()
Papa na Jumuiya ya Waindonesia wanaokaa Roma (@Vatican Media)
Kumbukizi ya Ziara ya Papa Francisko 2024
Ziara ya kihistoria ya Papa ya Papa Francisko mwaka 2024 , ambayo ilikuza urafiki huu na kuleta ujumbe wa matumaini kwa visiwa vyao vingi. Pia iliwasilisha ulimwengu maonesho yanayoonekana ya ushirikiano wa kidini kupitia Azimio la Istiqlal, lililotiwa saini na Papa na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Istiqlal ili kukuza umoja kwa manufaa ya ubinadamu. Leo, tunafurahi katika vifungo hivi vya urafiki; tunafurahi kuwepo kwao, pamoja na mamlaka za kiraia zinazowakilisha Indonesia.
![]()
Papa akutana na Jumuiya ya Waindonesia wanaoishi Roma (@VATICAN MEDIA)
Umoja katika Utofauti
Mkutano huu wenyewe ni ishara ya matunda mema ya imani na umoja. Hata mbali na nyumbani, hifadhi mila yao ya kuishi na kujaliana. Baba Mtakatifu Leo XIV alishukuru kwa uhusiano thabiti wanaodumisha na majirani zao, Wakristo na wasio Wakristo. Matendo haya ya utulivu ya huduma yanaonesha kauli mbiu ya Indonesia, "Umoja katika Utofauti." Kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema huko Jakarta, watu wa Indonesia wanaunda "kiunganishi" wanapounganishwa na kutafuta faida ya wote; kweli, kudumisha maelewano katikati ya utofauti kunafanana na "ufundi maridadi uliokabidhiwa kwa wote" (Francis,ko Mkutano na Mamlaka, Mashirika ya Kiraia, na Kikundi cha Wanadiplomasia katika Ukumbi wa Ikulu ya Rais "Istana Negara," 4 Septemba 2024).
![]()
Waindonesia wanaoishi Roma (@Vatican Media)
Manabii wa Ushirika
Katika suala hilo, Papa Leo XIV alitiwa moyo na jinsi wanavyoweka mshikamano huu katika vitendo, kuanzia kuwakaribisha wahamiaji wapya hadi kushiriki utamaduni wao na jumuiya za wenyeji. Hii ni mifano ya wazi ya "utamaduni wa kukutana," ambao ni msingi wa amani na ushirika. Papa aliwasihi wawe manabii wa ushirika katika ulimwengu ambao mara nyingi unatafuta kugawanya na kuchochea. Njia ya mazungumzo, njia ya urafiki, inaweza kuwa na changamoto, lakini inazaa matunda ya thamani ya amani. Papa aliwasifu kuwa wanaonesha kwamba inawezekana kuwa Wakatoliki waaminifu na Waindonesia wenye fahari, waliojitolea kwa Injili na waliojitolea kujenga maelewano katika jamii. Akiwa na matumaini kwamba wataendelea kujenga madaraja kati ya watu, tamaduni na imani, aliwakabidhi kwa Bikira Maria, Mama wa Kanisa. Kwa maombezi yake, waendelee kuwa mahujaji wa matumaini na mafundi wa amani. “Asante, na Mungu aibariki Indonesia, ninyi nyote, na wapendwa wenu kwa umoja na matumaini ya kudumu.”
![]()
Papa akutana na wanaindosia wanaoishi Roma (@Vatican Media)
