Tafuta

2025.09.22 Papa amekutana na Washiriki wa Mikutano Mikuu ya Mashirika ya Kitawa. 2025.09.22 Papa amekutana na Washiriki wa Mikutano Mikuu ya Mashirika ya Kitawa.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa watawa:kujinyima moyo,sala,Sakramenti,ukaribu na Mungu

Papa Leo XIX alikutana na Masista wa Mtakatifu Katherine Bikira na Shahidi,Wamisionari Wasalesiani wa Maria Immaculate,Masista wa Mtakatifu Paulo wa Chartres,na Wakarmeli Waliotengwa wa Nchi Takatifu,akawakumbusha urithi wa waanzilishi wao,wanawake wa ajabu ambao walizingatia maadili na hali mbaya ya maisha ya jamii iliyoachwa.Alitoa salamu za pekee kwa Watawa katika sehemu zilizoharibiwa na chuki na jeuri,ambao wanatoa ushahidi wa kutumaini kwa imani bila kuachwa na Mungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican tarehe 22 Septemba 2025 na washiriki wa Mikutano Mikuu ya Mashirika ya Watawa wa kike wa Mtakatifu Katherine Bikira na Shahidi, Wamisionari Wasalesiani wa Maria Immaculata, Masista wa Mtakatifu Paulo wa Chartres, na Wakarmeli wa Ndani  wa Nchi Takatifu, akionesha furaha ya kukutana nao asubuhi hiyo na kuwasalimia Wakuu wa Mashirika waliokuwapo. Papa alisema kwamba sifa ya kawaida ya Taasisi wanazoshiriki ni ujasiri ambao ulionesha mwanzo wao. Kwa njia hiyo Papa Leo alipenda kuwa na msukumo kwa tafakari fupi kutoka katika kifungu cha Kitabu cha Mithali kinachosema: "Mwanamke hodari, ni nani awezaye kumwona? Thamani yake ni mbali na marijani"(Mithali 31:10). Kwa sababu historia yao inatoa jibu hilo: ndani yao  kiukweli, Mungu hakupata mmoja tu, lakini wanawake wengi wenye nguvu na wenye ujasiri, ambao hawakusita kuthubutu na kukabiliana na matatizo ili kukumbatia mipango yake na kusema "ndiyo" kwa wito wake.

Papa alikutana na watawa washiriki wa mikutano mikuu
Papa alikutana na watawa washiriki wa mikutano mikuu   (@VATICAN MEDIA)

Papa alikazia kusema zaidi ya hayo, waliwatengenezea njia wengine wengi ambao, kama watawa hao , wakimfuata Kristo, maskini, wasafi, na watiifu, waliendelea na kazi yake, nyakati nyingine hadi kufikia hatua ya kufia imani. Tunazungumza juu ya wanawake wa ajabu ambao walianza misheni katika nyakati ngumu; ambao waliinamia juu ya taabu za kimaadili na za mali za maeneo yaliyopuuzwa zaidi ya jamii; ambao, walikuwa karibu na wale waliohitaji, walihatarisha maisha yao, hata kuwapoteza, waathriwa kwa  jeuri ya kikatili wakati wa vita. Wimbo wa zamani kutoka katika Liturujia ya masifu ya  jioni unaimba sifa za wanawake kama wao, ukifunua siri yao kwa maneno haya: "Walidhibiti mwili wao kwa kufunga, walilisha akili zao kwa chakula kitamu cha sala, walikata kiu yao kwa furaha ya mbinguni”(Commune Sanctarum Mulierum, Ad I Vesperas).

Haya ni maneno ya busara na ya kina, ambayo yanakumbuka mizizi ya maisha yao kama wanawake waliowekwa wakfu, katika kutafakari na katika kujitolea kitume. Nguvu ya uaminifu, kiukweli, katika viwango vyote viwili, hutoka kwa chanzo kimoja, Kristo, na njia za kupata kutoka katika utajiri wake ni, kama uzoefu wa milenia wa Kanisa unavyofundisha, wale waliotajwa: kujinyima moyo, sala, Sakramenti, ukaribu na Mungu, na Neno lake, na mambo ya Mbinguni (taz. Wakolosai 3:1-2). Pengine baadhi, katika ulimwengu wetu usioaminika, wanaweza kufikiri hii kama aina ya "umizimu," lakini hii inaweza kupingwa kwa urahisi na ushuhuda wenyewe wa kile, kwa karne nyingi, Mashirika yao yamefanya na yanaendelea kufanya. Hakika haya yote yamewezekana tu kwa nguvu zitokazo kwa Mungu. Baada ya yote, tunapitia kila siku: kazi yetu iko mikononi mwa Bwana, na sisi ni vyombo vidogo tu na visivyofaa, "watumishi wasiofaa," kama Injili inavyosema (taz. Luka 17:10). Hata hivyo, tukijikabidhi kwake, tukiendelea kuungana Naye, mambo makubwa hutokea, hasa kupitia umaskini wetu.

Papa akizungumza na washiriki wa mikutano mikuu ya mashirika
Papa akizungumza na washiriki wa mikutano mikuu ya mashirika   (@VATICAN MEDIA)

Kuhusiana na hili, Mtakatifu Agostino alipendekeza kwa watawa kuwa: "Njoo juu kwa unyenyekevu. Mungu huwainua wale wanaomfuata kwa unyenyekevu [...]. Mkabidhi zawadi alizokupatia, ili azihifadhi kwa ajili yako; weka nguvu zako kwake (Zab 58: 10) "(De sancta virginitate, 52,53). Na Mtakatifu Yohane Paulo II, akitafakari juu ya maisha ya kitawa katika kifungu cha Kugeuka Sura kwa Kristo (Mt 17:1-9), alizungumza juu ya "kupanda mlima" na 'kushuka mlima'" (Waraka wa Kitume Vita Consecrata, Machi 25, 1996, 14), ambapo "wanafunzi waliwafunikwa kwa ukaribu " fahari ya maisha ya Utatu na ushirika wa watakatifu, karibu kupenya kwenye upeo wa umilele, na mara moja wanarudishwa kwenye uhalisia wa kila siku, ambapo wanamwona tu ‘Yesu peke yake’ katika unyenyekevu wa asili ya kibinadamu, na wanaalikwa kurudi bondeni, kuishi naye taabu ya mpango wa Mungu na kuchukua njia ya msalaba kwa ujasiri." Katika nuru hiyo , Papa aliwataja waanzilishi wa shirika kwamba,  tunawatazama: Regina Protmann, Maria Gertrude wa Damu Azizi, Marie-Anne de Tilly – pamoja na Padre Louis Chauvet – Mtakatifu Teresa wa Avila, walinzi wa Mlima Karmeli, kama watu waliounganika kwa ukaribu na Mungu na hivyo kujiweka wakfu kwa ajili ya huduma yake na kwa ajili ya mema ya Kanisa zima, waliojitolea kukita mizizi na kuimarisha roho ya ndugu zao wote katika ufalme wa Kristo. na kuieneza katika kila sehemu ya dunia”( Lumen gentium, 44).

Papa alikutana na washiriki wa mikutano Mikuu ya mashirika
Papa alikutana na washiriki wa mikutano Mikuu ya mashirika   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza tena kwamba huo ndio urithi mlioupata na unafanya uwepo wenu hapa uwe wa maana sana. Hakika, hata katika siku zetu, kuna haja ya wanawake wakarimu. Katika suala hili, niruhusu nitoe salamu maalum kwa Masista wa Wakarmeli Waliokataliwa wa Nchi Takatifu, waliopo hapa: Wanachofanya ni muhimu, pamoja na uwepo wako wa kukesha na wa kimya katika maeneo yaliyogawanyika kwa huzuni na chuki na vurugu, pamoja na ushuhuda wako wa kuamini kuachwa kwa Mungu, pamoja na maombi yako ya kudumu ya amani. Sisi sote tunakusindikiza kwa maombi yetu na, kupitia kwako pia, tunakaribia wale wanaoteseka. Asanteni kina dada kwa wema mnaofanya katika nchi nyingi duniani na katika mazingira tofauti tofauti. Ninakubariki kutoka moyoni mwangu na kukukumbuka kwa Bwana.

Papa na watawa wa mashirikia wakati wa mikutano yao mikuu
22 Septemba 2025, 17:21