Tafuta

Picha mojawapo ya papa akiwa anasalimia watu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Picha mojawapo ya papa akiwa anasalimia watu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro  (@Vatican Media)

Papa anamwandikia mwanafunzi:Tusipoteze matumaini katika nyakati hizi ngumu

Katika toleo la hivi karibuni liitwalo"Piazza San Pietro,"Papa Leo XIV anajibu barua ya Veronica,mwanafunzi kijana wa Roma ambaye anahoji mustakabali wa ulimwengu na vijana."Tunaishi katika nyakati ngumu;maovu yanaonekana kutawala maisha yetu.Papa anajibu:“Ni lazima tuweke tumaini letu kwa Bwana Yesu,”akimwomba msichana huyo aendelee kumjulisha kuhusu masomo yake.

Vatican News

Papa Leo XIV anajibu wasomaji wa Uwanja wa Mtakatifu Petro, katika gazeti linalochapishwa na Kanisa kuu la Vatican na kuhaririwa na Padre Enzo Fortunato. Jarida hilo linafungua kwa sehemu ya kawaida ya "Mazungumzo na Wasomaji". Na katika toleo la Septemba, Papa anamjibu Veronica, wa Roma mwanafunzi wa udaktari, mwenye umri wa miaka 21. "Ndoto yangu ni kuwa daktari na kusaidia watu kupona kutokana na magonjwa yao," aandika kijana huyo wa kike  akihangaishwa na wakati huu ulio na wasiwasi mwingi na kuchanganyikiwa, kwa sababu ya matukio ya vita, uharibifu, na vifo, hasa vya wasio na hatia. "Inaonekana kuwa haiwezekani kuishi kwa amani. Je! anauliza Veronica. "Je, tunaweza kutumaini ulimwengu bora zaidi? Na sisi vijana tunaweza kufanya nini ili hili litokee?"

Nyakati Ngumu

"Tunaishi katika nyakati ngumu, lakini hii haipaswi kutufanya tupoteze tumaini katika ulimwengu bora," Papa Leo anaandika, akijibu kwa sauti ya upendo na ya kutia moyo, kwa maneno rahisi na thabiti. “Mpendwa Veronica, kwanza kabisa, natumaini kwa dhati kuwa unaweza kufikia ndoto yako. Taaluma unayotamani ni miongoni mwa taaluma bora zaidi, hasa ikiwa inaishi kama huduma kwa wanyonge na wasio na bahati. Kwa kuzingatia maalum kwa wale ambao hawana uwezo wa kiuchumi au wanaoishi katika hali ngumu ... Maswali yako ni yale yale ambayo wenzako wengi wanayo mioyoni mwao."

Matumaini kama Upinzani

Kwa kutambua uchungu wa sasa, Papa Leo XIv  anarudia ujumbe wa uaminifu kwamba: matumaini kama upinzani. "Ni kweli kwamba tunaishi katika nyakati ngumu. Uovu unaonekana kutawala maisha yetu. Vita vinazidi kuwaathiri watu wasio na hatia," lakini hatupaswi kamwe kukata tamaa. “Kama nilivyokwisha sema, nikimnukuu Mtakatifu Agostino: ‘Tuishi vyema na nyakati zitakuwa nzuri. Sisi ni nyakati.’ Hakika, nyakati zitakuwa nzuri tukiwa wema! Ili hili litokee, ni lazima tuweke tumaini letu kwa Bwana Yesu,” Papa anathibitisha. "Ni yeye ambaye ameamsha moyoni mwako hamu ya kufanya jambo kubwa na maisha yako. Yeye ndiye atakupatia nguvu ya kujiboresha mwenyewe na jamii inayokuzunguka, ili nyakati tunazoishi ziwe nzuri kweli."

Urafiki na Yesu

Barua inahitimishwa  kwa usikivu na huruma ya baba. Hakuna umbali kati ya Papa na mwamini kijana. “Kwa sababu hiyo, ninarudia mwaliko niliowaambia ninyi na vijana wote waliokuja Tor Vergata: 'Sitawisha urafiki wako pamoja na Yesu.' Inastahili kuwa na uhakika. Niweke ufahamu kuhusu masomo yako na safari yako ya kiroho ninakubariki.”

26 Septemba 2025, 19:42