Tafuta

Sinagogi ya Roma Sinagogi ya Roma  (©CdG - stock.adobe.com)

Papa atuma telegram ya matashi mema kwa Wayahudi Roma:tuhamasishe amani

Katika telegram iliyotumwa kwa Mkuu wa Kiyahudi wa Roma,Di Segni,katika fursa ya Maadhimisho ya Rosh Ha-Shanah,ya Yom Kippur na ya Sukkot,Papa Leo XIV,anatoa matashi yake mema kwa matumaini ya kuimarisha urafiki kati ya Wakatoliki na Wayahudi.

Vatican News

Katika fursa ya maadhimisho yajayo ya Rosh Ha-Shanah 5786, Yom Kippur na ya Sukkot, Baba Mtakatifu Leo XIV, ametuma matashi yake mema kuelekea kwa Jumuiya Kiyahudi Roma, katika telegram aliyomtumia mkuu wa Kiyahudi kwa niaba ya Jumuiya nzima kwamba “kwa rehema zake Mungu zisizo na kikomo, atujalie zawadi ya amani na hamu isiyochoka ya kuihamasisha daima.”

Papa akianza matashi yake hayo alieleza kwamba:“Ningependa kueleza, heri zangu za dhati kwako na kwa jumuiya yote ya Wayahudi ya Roma.” Kisha Papa Leo XIV alikumbuka uwepo wa Mkuu wa Kiyahudi Mario Di Segni kwenye Misa ya “mwanzo wa huduma yake ya Kuwa Kharifa wa Mtume Patro mjini Vatican” kunako tarehe 18 Mei 2025. Papa alisema kuwa “Mungu wa milele awe karibu na jumuiya na awasindikize katika jitihada zetu zote za kuimarisha urafiki kati yetu, katika jiji la Roma na ulimwenguni pote.” Papa alihitimisha kwa salamu ya “Shalom Alechem.”

 

22 Septemba 2025, 17:23