Papa Leo XIV; Misa katika Parokia ya Mt.Anna:Kiu ya utajiri,inahatarisha kuchukua nafasi ya Mungu mioyoni mwetu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa saa 4.00 kamili asubuhi, masaa ya Ulaya, sawa na saa 5 .00 kamili masaa ya Afrika Mashariki na Kati, Dominika tarehe 21 Septemba 2025, katika Parokia ya Mtakatifu Anna jijini Vatican. Katika mahubiri yale Papa alieleza alivyokuwa na furaha ya kadhimisha misa katika Parokia ya kipapa ya Mtakatifu Anna. Na kwa namna ya pekee akawasalimia waamini na watawa Waagostiniani ambao wanajikita na huduma yao, hasa Paroko Padre Mario Millardi, pamoja na na kama pia Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino aliyekuwapo, Padre Joseph Farrell, na alipenda pia kumsalimia Padre Gioele Schiavella, ambaye hivi karibuni alisherehekea umri wa kuheshimiwa wa miaka 103. Papa aliendelea, Kanisa hili linasimama katika eneo maalum, ambalo pia ni ufunguo wa huduma ya kichungaji inayofanywa na kwamba “sisi tunaweza kusema ni "mpakani," na karibu wote wanaoingia na kutoka Vatican wanapita karibu na Mtakatifu Anna. Kuna wanaopita kwa ajili ya kazi, biashara, kama wageni au mahujaji, wakiwa na haraka, wenye woga au utulivu. Kila mmoja anaweza kufanya uzoefu kwamba hapo kuna milango na mioyo iliyo wazi kwa sala, kusikiliza na kwa upendo.”
Baba Mtakatifu Leo XIV katika muktadha huo, alieleza kuwa Injili ambayo imesikilizwa punde inatuchochea kutathimini kwa makini juu ya uhusiano wetu na Bwana na kwa hiyo kati yetu. Yesu anaweka ufinyo mbadala kati ya Mungu na mabwana wawili” kwa hiyo: “hamwezi kutumikia Mungu na mali (Lk 16,13). Hii haina maana ya uchaguzi mbadala, kama ilivyo mambo mengine mengi, wala kuwa chaguo la pili la kutazamia katika mchakato wa kipindi, kwa mujibu wa hali. Inahitaji kuamua kweli na kwa mtindo hasa wa maisha. Hii ni kuchagua mahali pa kuweka moyo wetu, kuweka wazi ni nani kweli tunampenda, ni nani tunamhudumia kwa yote na ni wema gani wa kweli kwa ajili yetu
Mambo Msingi wa maisha ya binadamu:chakula,malazi na mavazi
Na ndiyo maana Yesu anapinga ukweli wa utajiri kwa Mungu: Bwana anazungumza namna hiyo kwa sababu anajua kuwa sisi ni viumbe wahitaji, ambao maisha yetu yamejaa mahitaji. Tangu tunapozaliwa, maskini, na uchi, wote tunahitaji utunzaji na upendo, nyumba chakula na mavazi. Kiu ya utajiri, inahatarisha kuchukua nafasi ya Mungu katika moyo wetu, wakati tukizingatia kuwa hiyo inaokoa maisha, kama alivyokuwa anafikiria yule wakili dhalimu katika somo(Lk 16,3-7). Kishawishi ni hiki: kufikiria kwamba bila Mungu tunaweza kwa vyovyote vile kuishi vizuri, wakati bila mali tutakuwa na huzuni na migogoro elfu ya mahitaji. Mbele ya majiribu ya mahitaji tunahisi kuwa hatarini, kinyume badala ya kuomba msaada kwa imani, na kushirikishana na udugu, tunajipeleka kuhesabu, kulimbikiza, kwa kugeuka na shuku na wasioamini wengine. Mawazo haya yanabadilisha mwingine kuwa mshindaji, katika mpinzani au ambaye ni kupata faida. Kama anavyoonya nabii Amosi. Wale ambao wanataka kufanya utajiri kuwa chombo cha kujibinafsisha hawaoni Mwezi mpya utaondoka lini, wapate kuuza nafaka (Am 8,6)” kwa kuwanyonya maskini. Kinyume chake Mungu uhatimisha mali ya uumbaji kwa wote.
Umaskini wetu kama viumbe unauhusinao na Bwana
Umaskini wetu kama viumbe unabainisha kwa hiyo ahadi na uhusiano ambao Bwana anamtunza mtu akiwa wa kwanza. Zaburi inafafanua mtindo huu wa mpaji: “Anyenyekeaye kutazama, mbinguni na duniani;” Humwinua mnyonge kutoka mavumbini na kumpandisha maskini kutoka katika taka.”(Zab 113,6-7). Hivyo ndivyo afanyavyo Baba mwema, daima na kuelekea wote: si kuelekea tu ambaye ni maskini wa mali za duniani, bali hata kuelekea umaskini wa kiroho na kimaalidili ambao unaangaisha wenye nguvu kama wadhaifu, maskini kama matajiri. Neno la Bwana hakika, halipingani na watu wenye hali ya juu, bali kwa wote, kufanya mapinduzi ya ndani, kwa uongofu ambao unaanzia moyoni. Kwa njia hiyo mikono yetu itafunguliwa: kwa kutoa, na si kutaka kunyakua. Kwa njia hiyo akili zetu zitafunguliwa: kwa akili ya kufanya mipango ya jamii iliyo bora, si kwa ajili ya kuchimba biashara kwa gharama ya juu. Kama anavyoandika Mtakatifu Paulo: “ Kabla ya mambo yote, nataka maombi, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka” (1Tm 2,1).
Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa: “leo hii kwa namna ya pekee, Kanisa linasali ili watawala wa Mataifa wawe huru dhidi ya vishawishi vya kutumia utajiri dhidi ya binadamu, kwa kuubadili kuwa silaha ambazo zinaharibu watu na kuwatumia kwa kuwabeza wafanyakazi. Anayetumikia Mungu anakuwa huru kutoka katika utajiri, lakini anayetumikia utajiri anabaki mtumwa! Anayetafuta haki anabadili utajiri kuwa wema wa pamoja; anayetafuta madaraka anabadili wema wa pamoja kuwa lindi la uchoyo wake mwenyewe. Papa Leo XIV alisema kwamba Maandiko Matakatifu, yanaibua nuru kuhusu kushikilia huku kwa vitu na mali, ambavyo vinachanganya moyo wetu na kupotosha mstakhabali wetu. Askofu wa Roma, hatimaye, alitoa shukurani kwao kwa namna nyingi, kushirikiana kutunza kwa uhai jumuiya hiyo ya Parokia, katika kuendesha hata kwa ukarimu, utume. Aliwatia moyo wa kuvumilia kwamatumaini katika kipindi ambacho kinatishiwa sana na vita. Watu wote leo hii wamekandamizwa na vurugu, na zaidi bila aibu kuwa na sintofahamu, wakiachwa katika hatima ya umaskini. Mbele ya majanga haya, Papa alisema tunataka kuwa watiifu, lakini kwa kutangaza kwa neno na kwa kmatendo ambayo Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu, ambaye anatukomboa na ubaya wote. Roho yake ibadili mioyo yetu ili kwa kumwilishwa na Ekaristi, hazina ya juu kabisa ya Kanisa tunaweza kugeuka mashuhda wa upendo na wa amani.
Hata hivyo akiwa kama Kardinali Prevost, aliwahi kuadhimisha Liturujia ya Ekaristi hapo tarehe 26 Julai 2024, katika fursa ya ukumbusho wa kiliturujia ya Watakatifu Joachim na Anna. Kanisa hilo la kale, lililojengwa katika karne ya 16, lilikuwa makao makuu ya chama cha udugu wa ‘Palafrenieri’ wa Kipapa, uliokuwa unahusika na mabanda ya kipapa, ambao Mtakatifu wake Msimamizi alikuwa Mtakatifu Anna. Baada ya Mkataba wa Lateran, tarehe 30 Mei 1929, Papa Pio XI, pamoja na Barua ya Kitume ya Ex Lateranensi pacto, aliianzisha kama Parokia na kuikabidhi chini ya uchungaji wake kwa watawa wa Shirika la Mtakatifu Agostino. Paroko wake wa kwanza, Padre Agostino Ruelli, aliteuliwa mwaka huo huo mnamo tarehe 7 Agosti 1929. Paroko wa sasa ni Padre wa Agostino Mario Millardi.
Parokia ya Mtakatifu Anna imetembelewa na Papa Pio XI, ambaye alitamani kuwapo kwenye uzinduzi wa chombo hicho mnamo tarehe 7 Februari 1931; Papa Yohane XXIII, ambaye alitembelea mnamo 20 Januari 1961; Papa Paulo VI, ambaye aliadhimisha kumbu kumbu ya miaka 50 ya ukuhani wake saa 2:00 asubuhi tarehe 29 Mei 1970; Papa Yohane Paulo II, aliyeiita "Parokia yangu" katika mahubiri yake tarehe 10 Desemba 1978; Papa Benedikto XVI, ambaye aliongoza ibada ya misa tarehe 5 Februari 2006; na Papa Francisko, ambaye aliichagua Misa yake ya kwanza kwa umma tarehe 17 Machi 2013.
