Tafuta

Papa Leo IXI,Kutukuka kwa Msalaba:Tujitoe kama Yesu alivyojitoa kwa ajili yetu

Dominika Septemba 14,Mama Kanisa anashehereka Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu ambapo Papa Leo XIV aliongoza Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana,akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume na tarehe hii ameadhimisha miaka 70 ya kuzaliwa.“Mungu alitukomboa kwa kujionesha kwetu,kwa kujitoa kama msindikizaji wetu,mwalimu,tabibu, rafiki,hadi kujifanya mkate uliomegeka katika Ekaristi.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kabla ya  Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari yake akidavua maana ya Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu inayoadhimishwa  kila tarehe 14 Septemba ya kila mwaka. Akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican alisema: “Leo Kanisa linaadhimisha Siku kuu ya Kutukuka  kwa Msalaba Mtakatifu, ambayo inaadhimisha ugunduzi wa Mti wa Msalaba na Mtakatifu Elena huko Yerusalemu katika karne ya nne, na kurudishwa kwa masalia ya thamani katika Mji Mtakatifu na Mfalme Heraclius." Papa aliongeza: “Lakini kuadhimisha Siku kuu hii kunamaanisha nini kwetu leo? Injili inayowasilishwa kwetu katika liturujia inatusaidia kuielewa (Yh 3:13-17). Tukio hilo linatokea usiku: Nikodemu, mmoja wa wakuu wa Kiyahudi, mtu mnyoofu na akili iliyo wazi (Yh 7, 50-51), alikwenda kukutana na Yesu. Alikuwa na anahitaji mwanga, kiongozi: anatafuta Mungu na kuomba msaada wa Mwalimu wa Nazareti, kwa sababu katika Yeye anamjua Nabii, mtu ambaye anatimizi ishara maalum."

Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV alisema kuwa "Bwana anampokea, anamsikiliza na mwisho anamwonesha kuwa mwana wa binadamu lazima ainuliwe, “kwa sabu amwaminiye apate uzima wa milele” (Yh 3,15) na aliongeza: “Mungu kiukweli aliupenda sana Ulimwengu hadi kumtoa mwanae wa pekee, ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele (Yh 3,16). Nikodemu, labda kwa wakati huo alikuwa haelewi maana kamili ya maneno hayo, na angeweza kwa hakika  kueleea wakati baada ya kusulibiwa, kusaidia kuzika mwili wa Mwokozi (Yh 19,39): ndipo atatambua kuwa Mungu ili kuwakomboa wanadamu, alijifanya mtu na akafa juu ya Msalaba.

Papa Leo XIV alisisitiza kuwa: “Yesu anazungumza hivyo na Nikodemu, kwa kukumbusha tukio la Agano la Kale (Hes 21,4-9) ambalo wakati Waisrael wako jangwani , walianza kuumwa na nyoka wa sumu, na ili waokoloewa walikuwa lazima walikuwa  watazame nyoka wa shaba ambaye Musa kwa kutiii amri ya Mungu, alikuwa ameitengeneza na kuiweka juu ya mti. Mungu alitukomboa kwa kujionesha kwetu, kwa kujitoa kama msindikizaji wetu, mwalimu, tabibu, rafiki, hadi kujifanya mkate uliomegeka katika Ekaristi. Na kwa kutimiza kazi hiyo alisaidiwa na moja ya zana ya kifo cha ukatili sana ambacho mtu hakuwahi kugundua: yaani Msalaba.

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@VATICAN MEDIA)

Kwa hiyo, Papa Leo XIV alisisitiza kwamba “  leo hii hata sisi tunasherehekea Kutukuka  kwa Msalaba: kwa upendo mkubwa sana ambao Mungu kwa kukumbatia wokovu wetu, alibadilisha katikati ya kifo,  hadi chombo cha maisha, kwa kutufundisha kuwa hakuna ambacho kinaweza kututengenisha naye (Rm 8,35-39) na kwa upendo wake ni  mkubwa kuliko dhambi zetu wenyewe.

Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema tuombe basi kwa maombezi ya Maria, mama aliyepo  Kalvario, karibu na mwanae ambaye ndani  mwetu tunasimike mizizi, na kukua katika upendo unaookoa, na kwamba hata sisi tutambue kujitoa kwa ajili ya mmoja na mwingine kama Yeye alivyojitoa kila kitu kwa ajili ya wote.

Papa: Tafakari ya Kutukuka kwa Msalaba
14 Septemba 2025, 15:45