Papa kwa Waagostinian:Msisahau wito wenu wa kimisionari
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV Jumatatu tarehe 15 Septemba 2025, alikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa 188 wa Shirika Waagostiniani ambao hivi karibuni Papa Mwenyewe alishiriki ufunguzi wake. Asubuhi Papa Leo mwenyewe alishiriki moja moja katika Taasisi ya Baba wa Kanisa ambapo walianza mkutano huo kuanzia Septemba 1 na utahitimishwa tarehe 18 Septemba. Katika hotuba yake alionesha furaha ya kuwa pamoja nao. Alisema alivyohisi kuwa nyumbani, na kushiriki kwa kina hata yeye, Roho ya kushirikishwa kiroho, kwa kile ambacho wako wanakiishi katika siku hizi. Papa alimshukuru Mkuu wa Shirika ambaye amehitimisha muda wa huduma na kumkaribisha mkuu Mpya ambaye amechaguliwa hivi karibuni. Papa alisema katika kazi hizi zinazowawajibisha zinahitaji sala za wote na kuwaomba wasisahahu! Mkutano mkuu ni fursa ya thamani kwa ajili ya kusali pamoja na kutafakari zawadi waliyopokea, karama ya sasa. Na hata juu ya changamoto na matatizo ambayo yanadai Jumuiya. Wakati wanaendelea kupeleka mbele shughuli, Papa aliongeza , kuadhimisha Mkutano Mkuu maana yake ni kujiweka katika usikivu wa Roho, kwa namna inayofanana na kile alichokisema Baba wao Mwanzilishi wa Shirika Mtakatifu Agostino, akiwakumbusha umuhimu wa undani wa safari ya imani kwamba: “Usitoke nje yako, rudi ndani mwako; ukweli unaishi katika undani wa mtu (De Vera Religione 39,72).
Undani si kukwepa uwajibikaji kibinafsi na kijumuiya
Baba Mtakatifu Leo alikazia kusema: kwa upande mwingine, undani siyo kukimbia uwajibikaji wetu kibinafsi na kijumuiya, kutoka katika utume ambao Bwana alitukabidhi katika Kanisa na katika Ulimwengu, kutoka katika mahitaji na matatizo ya dharura. Ni kuingia ndani binafsi ili baadaye kutoka kwa namna ambayo inahuishwa zaidi na kwa shauku katika utume. Kuingia ndani mwetu ni kupyaisha mwamko wa kiroho na kichungaji: ni kurudi katika kisima cha maisha ya kitawa, na kwa wawekwa wakfu, ili kuweza kutoa nuru kwa wale ambao Bwana anatuwekea mbele katika safari yetu. Ni kugundua uhusiano na Bwana na kwa ndugu, katika familia yenyewe ya kitawa, kwa sababu kuanzia katika muungano wa upendo, tunaweza kutoa uhuisho na kukabiliana vema masuala ya maisha ya kijumuiya na changamoto za utume.
Utawa si upamoja na kanuni za kutimiza, ni wito wa kuhisi mvuto wa upendo
Katika muktadha huo, Papa Leo XIV alisema: baada mapana na ushirikishwaji wa tafakari ambazo walipeleka mbele kwa miaka hii, walijikita juu ya baadhi ya mantiki ambazo Papa alipenda kuzisisitiza kwa kifupi. Awali ya yote mada msingi: ya miito na malezi ya kwanza. “Ninapenda kukumbusha ushauri wa Mtakatifu Agostino: Penda mtakachokuwa(Hotuba 216, 8). Papa aliongeza kwamba hapo anapata kile ambacho ni maelezo ya thamani, hasa ili kutoangukia katika makosa ya kufikiria malezi ya kitawa kama upamoja wa kanuni za kutimiza au mambo ya kufanya au tena kama nguo ambayo tayari imeshonwa kwa ajili ya kuivaa kimyakimya. Kitovu cha hayo yote, kinyume chake kuna upendo. Wito wa kikristo na ule wa kitawa kwa namna ya pekee, unazaliwa pale tu ambapo ni kuhisi mvuto wa kitu kikubwa zaidi, cha upendo ambao unaweza kumwilisha na kusaza moyo.
Wasiwasi wa kwanza ni kusaidia vijana watambue wito wao
Kwa njia hiyo Papa alisema : awali ya yote “Wasiwasi wetu wa kwanza unapaswa kuwa ule wa kusaidia, hasa vijana waweze kunuia uzuri wa wito na wa kupenda kile ambacho kwa kukumbatia wito, wanaweza kuwa. Wito na malezi si ukweli unaotabilika: ni tukio la kiroho ambalo linajumuisha historia nzima ya mtu, na linahusu awali ya yote tukio la upendo na Mungu. Upendo ambao kama tujuavyo, Agostino aliuweka katikati ya utafutaji wake wa kiroho ni kigezo msingi hata kinachohusu mafunzo ya kitaalimungu na ya mafunzo ya kiakili. Katika utambuzi wa Mungu kamwe hakuna uwezekano wa kufika kwake kwa kutumia sababu yetu pekee na kwa safu za mafunzo ya kinadharia, bali awali ya yote inahitajika kuacha kushangazwa na ukuu wake, kujiuliza sisi wenyewe na maana ya mambo yanayotokea ili kuweza kuingiliana na kanuni za Muumba na hasa kumpenda na kufanya upende. Kwa wale ambao wanajifunza. Agostino anapendekeza ukarimu na unyenyekevu, unaotokana na upendo: ukarimu wa kushiriki utafiti wa mtu na wengine, ili kufaidi imani yao; unyenyekevu wa kuepuka ufahari wa wale wanaotafuta elimu kwa ajili yao wenyewe, wakijiona bora kuliko wengine kwa kuwa nayo.
Kubaki waaminifu kwa umaskini
Na wakati huo huo, zawadi isiyoshindwa ya upendo wa Mungu ni kile ambacho tunapaswa kukitazama ikiwa tunataka kuishi vema haraka kwa maisha ya kijumuiya, na shughuli za kitume, kwa kuweka pamoja mali zetu, kama ilivyo hasa za kibinadamu na kiroho. Papa alisema wakumbuke kile ambacho ni muhimu kilichoandikwa kwenye kanuni: “Kama unavyolishwa kutoka kwenye chungu kimoaja vivyo hivyo jivikeni kutoka katika kabati moja(Kanuni ,30). Kubaki waaminifu wa umaskini wa kiroho na kufanya kwa namna ya mantiki ya kuishi kile ambacho sisi ni, na tulicho nacho, ikiwa ni pamoja na vyombo na miundo ya majengo , huduma ya utume wa kitume.
Ushauri wa Papa: kutosahau wito wa kimisionari
Hatimaye Papa Leo alitoa ushauri wasisahau wito wao wa kimisionari. Kuanzia na tume wa kwanza kunako mwaka 1533, Waagostinian walitangaza Injili katika sehemu mbali mbali za dunia kwa shuku na ukarimu, huku wakichulia utunza wa jumuiya za kikristo mahalia, kwa kujikita katika elimu, mafundisho, kwa kujitoa kwa maskini na kutimiza kazi za kijamii na za upendo. Roho hiyo ya kimisionari haipaswi kuzimwa kwa sababu hata leo hii kuna haja sana. Baba Mtakatifu Leo amewashauri kuhuisha tena kwa kukumbuka kuwa utume wa uinjilishaji, ambao wote tunaitwa, unahitaji kushuhudia kwa furaha nyenyekevu na rahisi, uwezekano wa huduma, kushirikishana maisha na watu ambamo tumetumwa. Papa Leo XIV amewatakia mema ya kuendelea na kazi ya Mkutano mkuu kwa furaha ya udugu na kwa moyo ulio tayari kupokea mawaidha ya Roho. Papa anasali kwa ajili yao ili upendo wa Bwana auhishe mawazo yao na matendo yao, kwa kuwafanya mitume na mashuhuda wa Injili duniani. Kwa maombezi ya Bikira Maria na Mtakatifu Agostino, na anawasindikiza kwa baraka ya kitume.
