Papa Leo XIV ahimiza wataalimungu kujibu changamoto za kidijitali
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican tarehe 13 Septemba 2025 katika Ukumbi wa Clementine wa Jumba la Kitume ya Vatican na Washiriki takribani 130 wa Semina ya kimataifa, iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Taalimungu, yenye mada “Uumbaji, Asili, Mazingira kwa Ulimwengu wa Amani.” Papa kwa njia hiyo aliwahimiza kufanya taalimungu ya hekima yenye uwezo wa kutoa majibu ya busara hata kwa changamoto za kidijitali. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu kwa mara ya kwanza alitoa muhtasari wa malengo ya Semina hiyo iliyofanyika Alhamisi tarehe 11 na Ijumaa tarehe 12 Septemba 2025 katika ukumbi wa Casina Pio IV kwenye bustani nzuri za Vatican.
Semina hiyo ililenga mada muhimu pia kwa watangulizi wake, Mtakatifu Yohane Paulo II, Benedikto XVI, na Francisko, kama vile uendelevu wa mazingira na ulinzi wa uumbaji. Baadaye alisisitiza jinsi ambavyo juhudi ya kuboresha hali ya mazingira na kijamii ya ulimwengu wetu inahitaji kujitolea kwa kila mtu. Haja ambayo, kwa mujibu wa Papa, semina hiyo ilizingatia, na kupendekeza sahihi, kiutamaduni na kidini, mtazamo wa mshikamano na ushirikiano unaoshinda vikwazo na mipaka ya kikanda, kitaifa, kiutamaduni na hata kidini. Mtazamo huo, Papa Leo XIV aliendelea, unaakisi mabadilishano makali zaidi na zaidi, na mipango ya kuvutia na yenye matunda. Taalimungu, ambayo ni kipimo cha msingi cha umisionari wa Kanisa na shughuli ya uinjilishaji Papa alitoa jukumu la kuendeleza tafakari hiyo. Kwa hakika kwa sababu inashughulikiwa kwa kila mtu katika kila zama, taalimungu msingi ili kutimiza utume huu lazima uwe, katika maneno yaliyotungwa na Papa Francisko, yemye 'kutoka nje' yaani, yenye uwezo wa kuunganisha ukali wa kisayansi na shauku ya historia; taalimungu iliyojumuishwa, iliyojaa maumivu, furaha, matarajio, na matumaini ya wanadamu.
Papa Leo XIV alionesha mifano ya kihistoria ya Taalimungu ya hekima yenye uwezo wa kuunganisha mambo haya tofauti kwa mfano: "Mababa wakuu na Waalimu wa Mambo ya Kale," ambao walijua jinsi ya kuchanganya imani na sababu, kutafakari, sala, na Ibada kali. Miongoni mwao, Mtakatifu Agostino, mfano wa wakati unaofaa, Papa alielezea kuwa, ni ambaye alikuza taalimungu iliyoeleweka sio utafiti wa kufikirika, bali kama tunda la uzoefu wa Mungu na uhusiano muhimu na Yeye. Kwa njia hiyo Askofu wa Hippo, alisema Papa leo XIV kuwa hasa katika Maungamo yake, alipendekeza tafakari ya kitaalimungu iliyokuwa mwili na yenye uwezo wa kujibu mahitaji ya kiroho, mafundisho, kichungaji, na kijamii ya wakati wake. Kwa upande wa Mtakatifu Thomas kisha akaratibu safari ya Agostino ya kuwepo na yenye hisia kwa kutumia mbinu za Aristotle," akielewa taalimungu kama sayansi ya uelewa au hekima. Ukuzaji huu wa kiakili ulikamilishwa baadaye na Mwenyeheri Antonio Rosmini, ambaye, kama Papa Leo XIV alivyosema, alichukulia Taalimungu kuwa usemi bora wa upendo wa kiakili.
Kisha Papa Leo alibainisha juu ya changamoto za kidijitali kama mpaka unaofuata wa matumizi ya kazi ya kitaalimungu. Ushuhuda muhimu wa ujuzi wa imani katika huduma ya ubinadamu, katika nyanja zake zote: kibinafsi, kijamii, na kisiasa, ni Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa, yanayoitwa leo hii kutoa majibu ya busara kwa changamoto za kidijitali pia. Katika utafutaji huu wa majibu, Taalimungu inapingwa moja kwa moja,kwa sababu mbinu ya kipekee ya kimaadili kwa Ulimwengu mgumu wa Akili Unde (AI) haitoshi."
Nidhamu ya hekima ina kazi ya kutoa maono ya kianthropolojia ambayo yana msingi wa hatua ya kimaadili. Ni muhimu, Papa alisema, kurejea swali la kudumu: mwanadamu ni nani, ni nini hadhi yake isiyo na mwisho, isiyoweza kupunguzwa kwa android yoyote ya kidigitali? Hatimaye katika hotuba yake, Papa Leo XIV aliwahimiza Wataalimungu kujihusisha sio tu na falsafa, bali pia na fizikia, biolojia, uchumi, sheria, fasihi, na muziki, ili kuleta chachu nzuri ya Injili kwa tamaduni mbalimbali na kukuza na kumwilisha taalimungu hii ya hekima, katika huduma ya Kanisa na ulimwengu wote.
