Tafuta

Papa Leo XIV akutana na Patriki Karekin II. Papa Leo XIV akutana na Patriki Karekin II.  (ANSA)

Papa Leo XIV akutana kwa mara kwanza na Patriaki wa Waarmenia,Karekin II

Papa Leo XIV alikutana na Patriaki Karekin II,wa Waarmenia Wote,katika mkutano uliofanyika Jumanne Septemba 16 huko Castel Gandolfo, nyumba ya kipapa mahali ambapo Papa Leo alifika huko Septemba 15.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Karekin II, Mkuu wa wakatoliki wa Waarmenia Wote, alikutana na Baba Mtakatifu Leo XIV siku ya Jumanne tarehe 16 Septemba 2025, katika mkutano wa kwanza kati ya wawili hao. Tangu kuchaguliwa kwake miaka ishirini na mitano iliyopita, Mkuu hiyo  Karekin II amekutana na Mtakatifu Yohane Paulo II, Benedikto XVI, na Francisko. Mkutao wao ulifanyika  katika Villa Barberini, makazi ya Papa huko Castel Gandolfo, ambapo Papa Leo XIV amekuwa huko tangu Jumatatu jioni tarehe 15 Septemba. Mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya kidugu na ya ukarimu, ambayo masuala mbali mbali ya kikanisa yalijadiliwa. Patriaki wa Armenia alisisitiza hatima ya Waarmenia wa Artakh,” ambapo Askofu Mkuu Khajag Barsamian, mwakilishi wa Kitume wa  Armenia wa Etchmiadzin, alieleza katika mahojiano ya simu na Vatican News. Patriaki alitoa mwaliko kwa Papa kutembelea Armenia, Askofu Mkuu Barsamian aliendelea, na “wote wawili walithibitisha umuhimu wa amani, lakini amani inayotokana na haki, kama Patriaki Karekin alivyosisitiza.”

Leone XIV e Karekin II a Castel Gandolfo

Leone XIV a Karekin II huko Castel Gandolfo   (@Vatican Media)

Pamoja na Patriaki huyo  alikuwa na  wajumbe waliofuatana naye katika ziara hii ya Roma. Kwa hiyo  Kundi lililokutana na Papa lilielekea Vatican, ambako Patriaki alikutana na Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, na Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Programu ya siku hiyo pia ilijumuisha hata kutembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, Kanisa la Kipapa ambapo Patriaki Karekin II alitaka kutoa heshima zake kwa Hayati Papa Francisko, ambaye alikuwa ameanzisha uhusiano wa mazungumzo na urafiki, kwa kusali mbele ya kaburi lake. Kisha alitulia ili kutumia muda katika maombi mbele ya sanamu ya  Bikira Salus Populi Romani , yaani "Bikira Maria Afya ya Waroma."

Karekin II prega davanti alla tomba di Papa Francesco a Santa Maria Maggiore

Karekin II anasali mbele ya Kaburi ya Papa Francisko katika kanisa Kuu la Mtakatifu maria Mkuu

Ziara za awali Vatican

Ziara ya kwanza ya Patriaki huyo jijini  Roma ilianza  mnamo tarehe 9-10 Novemba 2000, wakati, kama Patriaki  mpya wa Waarmenia Wote, alikuwa mgeni wa Mtakatifu Yohane Paulo II katika Jubilei ya 2000. Wakati wa ziara hiyo, kufuatia tamko lililotiwa saini na Mtakatifu Paulo VI na Patriaki  Vasken I,  tarehe 12 Mei, 1970, Tamko la Pamoja lilitiwa saini: hatua katika safari ambayo bado inaendelea kuelekea kurejesha ushirika kamili kati ya Makanisa haya mawili. “Pamoja tunakiri imani yetu kwa Mungu wa Utatu na Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, ambaye alifanyika mwanadamu kwa ajili ya wokovu wetu, pia tunaamini katika Kanisa Moja, Katoliki, la Mitume na Takatifu.

Hii ndiyo imani yetu ya kawaida, yenye msingi wa mafundisho ya Mitume na Mababa wa Kanisa,” Tamko hilo lilisema: “Tunaendelea kusali kwa ajili ya ushirika kamili na unaoonekana kati yetu, utume wa pamoja, yaani, kufundisha imani ya kitume na kushuhudia upendo wa Kristo kwa wanadamu wote, hasa wale wanaoishi katika hali ngumu,” lilibainisha Tamko hilo.Katika ziara hiyo, Mtakatifu Yohane  Paulo II alimkabidhi Karekin masalia ya Mtakatifu Gregory Mkuu. Mwaka mmoja baadaye, kuanzia Septemba 25-27, 2001, Papa wa Poland alitembelea Armenia kuadhimisha mwaka wa 1700 tangu kutangazwa kwa Ukristo kama dini ya serikali. Alikuwa Papa wa kwanza kukanyaga ardhi ya Armenia. Masalia ya Mtakatifu Gregory pia yaliwasilishwa kwa Patriaki wa Nyumba Kuu ya Kilikia ya Waarmenia, Aram I, na kwa Patriaki Mkatoliki wa wakati huo wa Armenia, Nerses Bedros XIX Tarmouni.

Lo scambio dei doni durante l'udienza

Lo scambio dei doni durante l'udienza   (@Vatican Media)

Mikutano na Benedikto XVI na Papa  Francisko

Catholicos Karekin II alirejea Vatican tarehe 6-9 Mei 2008, kwa mwaliko wa Papa Benedikto XVI, kushiriki katika maadhimisho ya kiekumene iliyoongozwa na Papa. Tarehe 12 Aprili 2015, Patriaki  huyo alijikuta kwa mara nyingine tena Vatica, kwa mujibu wa matakwa ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyetaka kuwa na mkuu wa Kanisa la Armenia la Etchmiadzin pembeni mwake wakati wa Misa iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi wa Armenia wa mwaka 1915.

Wakati wa maadhimisho hayo, Papa Francisko alimtangaza Mtakatifu Gregory wa Narek kuwa Mwalimu wa  Kanisa la Ulimwengu, wakati wa umuhimu mkubwa kwa Kanisa zima la Armenia. Kwa kufuata nyayo za Yohane Paulo II, Papa Francisko pia alitembelea Armenia, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Juni 2016. "Nchi ya kwanza ya Kikristo" - kama kauli mbiu ya ziara ya kitume ilivyotangazwa - iliheshimiwa tena na Papa wa Argentina mnamo 2018, alipozindua sanamu ya Mtakatifu Gregory wa Narek katika bustani ya Vatican. Karekin II alikuwepo siku hiyo pia, pamoja na Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Armenia, Serzh Sargsyan. Mwaka huo huo, mnamo Oktoba, Karekin II alimtembelea tena Papa Francisko na kukutana na washiriki wengi wa Curia Romana. Mkutano mwingine ulifanyika mnamo Septemba 2020, na katika hafla hiyo Patriaki ilishikishwa na Papa sasisho juu ya hali iliyotokea kufuatia operesheni za kijeshi dhidi ya Artsakh. Hivyo alisisitiza umuhimu wa maombi ya Papa ya kumaliza mzozo huo na kurejesha amani.

La foto del Papa con Karekin II e la sua delegazione, a Castel Gandolfo

 Papa na Karekin II na uwakilishi huko Castel Gandolfo

Il colloquio nella residenza di Villa Barberini, a Castel Gandolfo

Mazungumzo katika makao ya  kitume huko Villa Barberini, Castel Gandolfo

Karekin II ha incontrato il cardinale Kurt Koch, prefetto del Dicastero per la Promozione dell'Unità dei Cristiani

Karekin II alikutana na Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa kikristo.L'incontro con il cardinale José Tolentino de Mendonça, prefetto del Dicastero per la Cultura e l'Educazione

16 Septemba 2025, 13:13