Papa,yuko wapi Ndugu yako?:katika uso wa maskini,mkimbizi,hata adui ni Fumbo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV Ijumaa, tarehe 12 Septemba 2025 ametoa hotuba yake mjini Vatican kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu “Udugu wa Kibinadamu”. Alianza kwa kuwakaribisha na kuwashukuru uwepo wao kutoka sehemu nyingi za dunia katika toleo hilo la tatu, lililoandaliwa na Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Mfuko wa Fratelli Tutti, Chama cha Be Human na Mfuko wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Ubinadamu. Papa aliesema kuwa Sayari imegubikwa na migogoro na migawanyiko na ndiyo sababu kubwa ya msukumo na ujasiri wa kusema: “hapana kwa vita na Ndiyo kwa amani na udugu." Papa Leo XIV alikumbusha kuwa, kama Papa Francisko alivyotufundisha, kiukweli vita siyo njia ya haki, ya kuondokana na migogoro." Kakubiliana na migogoro, kuisuluhisha na kuibadilisha katika pete ya kushikamano na mchakato mpya (Evangelii gaudium,227, ni safari ya hekima na safari ya wenye nguvu.
Papa Leo XIV aliongeza kusema kuwa uwepo wao unashuhuda hekima hiyo, ambayo unaunganisha tamaduni na dini, nguvu ile ya kimya ambayo inatufanya kukua kama kaka na dada licha ya tofauti zetu zote. Katika simulizi ya kibiblia, uhusiano wa kwanza kidugu, ule kati ya kaino na Anili, ulikuwa ni janga tupu la kimigogoro. Licha ya hayo, mauaju ya kwanza, yatupelekea kuhitimisha tukisema: “daima imekuwa hivi.” Hata kama ni ya zamani, na kama ilivyoenea, vurugu, Kanisa, haliweza kuvumilia na kama za “kawaida.” Kinyume chake, kanuni inasikika katika swali la Mungu, linalomwelekea mkosaji: “ yuko wapi ndugu yako?(Mw4,9). Ni katika swali hilo, kuna wito wetu, sheria, na kanoni za haki. Mungu halipizi kisasi cha Abeli na Kaini, lakini anauliza swali ambalo linasindikiza safari yote ya historia.
Baba Mtakatifu Leo, kadhalika alisema swali lenyewe, leo hii kuliko hapo awali ambalo linaulizwa kwetu, kama msingi wa upatanisho. Kwa kina zaidi, linatasikika tena hivi: “Kaka, dada, huko wapi? Huko wapi katika biashara ya vita ambavyo vinavunja maisha ya vijana wanaolazimika kushika silaha, zinazoua raia, watoto, wanawake, na wazee wasio na ulinzi, kusambaratisha mji, vijiji na viumbe vyote, kwa kuacha uharibifu ndani mwake vifusi na uchungu? Kaka na dada, huko wapi katikati ya wahamiaji wanaodharauliwa, wafungwa na kukataliwa, kati ya wale ambao wanatafuta wokovu na matumaini na kukutana na kuta na sintofahamu? Huko wapi ndugu, wakati maskini wanahukumiwa na umaskini wao, wamesahuliwa na kubaguliwa, katika ulimwengu ambao unashabikia faida zaidi ya watu? Kaka na dada, huko wapi katika maisha yaliyochangamana, lakini ambamo, upekwe unaumana mahusiano ya kijamii na kutufanya kutojuana hata sisi wenyewe?
Baba Mtakatifu baada ya maswali hayo, alijibu, kuwa majibu hayawezi ni kimya. Na jibu ni wao, kwa uwepo wao, kazi wanayojikita nayo na ujasiri wao. Jibu ni kuchagua mwelekeo mwingine wa maisha, wa kukuza na maelendeleo. Kutambua kwamba mwingine ni kaka au dada kunamaanisha kujikomboa kutoka katika kisingizio cha kujiamini kuwa sisi ni watoto tu, na pia kutoka katika mawazo ya wengine ambao hukaa pamoja kwa masilahi ya kibinafsi. Sio ubinafsi tu ndio unaotuweka pamoja. Tamaduni kubwa ya kiroho na maendeleo ya kufikiri muhimu huturuhusu kwenda zaidi ya mahusiano ya damu au ya kikabila, zaidi ya undugu huo ambao hutambua wale tu wanaofanana na kukataa wale ambao ni tofauti.
Inashangaza kwamba katika Biblia, kama vile ufafanuzi wa kitaalamu umefunua, ni maandishi ya hivi karibuni na yaliyokomaa ambayo yanasimulia udugu unaovuka mipaka ya kikabila ya watu wa Mungu na ambao umejikita katika ubinadamu wetu wa kawaida. Historia za uumbaji na nasaba zinashuhudia hili: watu mbalimbali—hata maadui zao—wana asili moja, na Dunia, pamoja na utajiri wake, ni vya wote, si wachache tu. Katika moyo wa Waraka wa Fratelli tutti, tunasoma: “Kuna utambuzi wa msingi, muhimu ambao lazima ufanywe ili kuelekea urafiki wa kijamii na udugu wa ulimwengu wote: kutambua ni kiasi gani mwanadamu, ni kiasi gani mtu ana thamani, daima na katika hali yoyote.”(Ft 106). Udugu ni jina zaidi la ukaribu wa kweli. Maana yake ni kupata sura ya mwingine. Na katika sura ya maskini, mkimbizi, hata aliye adui, ni kujua Fumbo: kwa anayeamini anakuwa sura ya Mungu mwenyewe.
Baba Mtakatifu aliwashauri kugundua michakato, katika kanda na kimataifa ambayo inahamasisha maendeleo ya mitindo mipya ya upendo kijamii, ya mshikamano kati ya ulewa na mshikamano kati ya kizazi. Iwe michato inayofahamika, ambayo inajumisha hata maskini, na si kama hatima ya kusaidia, lakini kama atu wa kufanya mang’amuzi na wa Neno. Papa aliwatia moyo kuenedelea katika kazi hiyo ya semina ya kimya. Katika hiyo inaweza kuzaa mkachato wa kushiriki kuhusu ubinadamu na juu ya udugu ambao hausimamii kuheshimu haki, lakini unajumuisha hata matendo na sababu za dhati ambazo zinatufanya kuwa tofauti katika maisha kila siku. Papa alisisitiza kuwa tunahitaji kwa upana “mshikamani wa kibinadamu”, usiokita mizizi katika uwezo bali katika utunzaji, usio kuwa wa kifaida, bali katika zawadi; usioshuku, bali juu ya kuaminiana. Utunzaji zawadi, imani, sio fadhila kwa wakati ulio huru: ni nguzo za uchumi ambao hauuwi, bali unazidisha na kupanua ushirika katika maisha.
Papa Leo amependa kuwashukuru wasanii, ambao pamoja na ubunifu wao, watazindua ujumbe huu kwa ulimwengu, kutoka katika Mkumbatio maarufu wa nguzo za Bernini. Shukrani za kipekee ziwaendee waloituza tuzo za Nobel, ikiwa ni pamoja na kuandika Tamko la Pamoja kuhusu Udugu wa Kibindamu wa tarehe 10 Juni 2023 , pia ikiwa kwa ushuhuda ambao wanatoa maana inayokubaliwa ya kimataifa. Papa aliwaomba waendelee kukua kiroho kidugu kwa njia ya utamaduni, mahusiano ya kazi, na matendo ya kidiplomasia. Wabebe daima katika moyo maneno ya Yesu ya Injili ya Yohane “Nawapa amri mpya: mpendaneni ninyi kwa ninyi. Kama nilivyo wapenda ninyi, nanyi pia mpendane (Yh 13,34-25). Papa alisema anavyowasindikiza kwa sala na kuwapatia baraka ya kitume.
