Tafuta

2025.09.10 Mkutano Mkuu wa Wakarmeli. 2025.09.10 Mkutano Mkuu wa Wakarmeli.  (https://ocarm.org/it/ )

Papa Leo XIV kwa Wakarmeli:Muwe mashahidi wa umoja katika jamii zilizogawanyika

Katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakarmeli uliofunguliwa Septemba 9 huko Malang,Indonesia, ambapo Papa alituma ujumbe wa kuwatia moyo,ulioelekezwa kwa Mkuu wa Shirika Míċeál O'Neill anahimiza:Kukuza utulivu unaowawezesha kutambua alama za nyakati,hasa kupitia mtazamo wa maskini.

Vatican News

Baba Mtakati Leo XIV aliwatia moyo Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakarmeli, linalofanyika kuanzia Septemba 9 hadi 26 huko Malang nchini Indonesia, katika katika ujumbe uliosomwa Jumanne tarehe 9 Septemba  katika ufunguzi wa mkutano huo. Papa aliandika kuwa: "Ninaomba kwamba dhamana ya upendo katika jumuiya zenu itashuhudia zawadi ya umoja, hasa katika sehemu zile za jamii zilizogawanyika na migawanyiko na ubaguzi."

Katika barua hiyo, iliyotiwa saini tarehe 5 Agosti 2025 na kutumwa kwa Mkuu wa Shirika hilo Padre Míċeál O'Neill, Papa Leo XIV alisisitiza jinsi ambavyo mada iliyochaguliwa kwa mkutano huo isemayo: "Udugu Wetu wa utafakari unatambua utume wake," inaakisi "moyo wa karama ya Wakarmeli" kwa sababu inaonesha jinsi "maisha ya pamoja ya sala" yanajumuisha msingi wa huduma yao kwa Kanisa na Ulimwengu." Kwa njia hiyo "kwa kujikita katika sala ya kimya na kujaliana, unasitawisha utulivu unaowawezesha kutambua alama za nyakati, hasa kupitia mtazamo wa maskini, na kujibu kwa uthabiti wa kimya wa upendo."

Mkuu wa Wakarmeli akisoma ujumbe wa Papa
Mkuu wa Wakarmeli akisoma ujumbe wa Papa   (https://ocarm.org/it/)

Kumwilisha Mtazamo wa Upendo wa Kristo Kupitia Matendo


Papa Leo XIV alinukuu Kanuni ya Wakarmeli, ambayo inahimiza: "kufanya kazi fulani, na kurudia jinsi hiyo, ina maana kubwa katika huduma ya Shirika hili la kidini  kwa sababu  inaalika kumwilisha macho ya upendo wa Kristo, anayemkumbatia kila mtu kwa huruma na upendo." Kwa namna hiyo, iwe kupitia mahubiri ya mafungo, mwongozo wa kiroho, kazi ya parokia, au elimu ya vijana," Papa anatumaini kwamba Wakarmeli wanaweza kuwa vielelezo vya upendo na umoja katika ulimwengu ambao mara nyingi unakumbwa na mivutano na migogoro." Hatimaye, Papa anakabidhi Mkutano Mkuu huo kwa maombezi ya Mama Yetu wa Mlima Karmeli," akiamini kwamba mkutano huo, unaofanyika wakati wa Mwaka Mtakatifu,  wa Jubilei 2025 utakuwa fursa ya kujipyaisha kiroho."

10 Septemba 2025, 16:45