Salamu za Papa Leo XIV kwa wanahija wa Umbria:Tangazeni uzuri wa tamaduni na asili yenu!
Vatican New.
Baba Mtakatifu Leo XIV Jumamosi tarehe 13 Septemba 2024 akikutana na washiriki wa hija ya Jubilei kutoka majimbo mbali mbali ya Mkoa wa Umbria nchini Italia waliofika mjini Vatican na ambao walikuwa wamekusanyika katika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro alisema: “Dunia hii tunayoishi inahitaji uzuri ili kuepuka kuzama katika kukata tamaa." Na eneo la Umbria inazo kwa wingi kama vile kisanii, kihistoria na asili. Ni nukuu ya maneno ya Mtakatifu Paulo VI kuonesha urithi wa eneo la Italia ya Kati. Kwa njia hiyo Papa alisema “ Mnatoka katika kanda ambayo ni nzuri kwa njia nyingi: moyo wa kijani wa Italia, na asili yake na muhuri wa hazina ya sanaa, pamoja na vijiji na mila yake; na nchi ya watakatifu. Kwa hakika aliweza kuwasilisha uzuri wa Mkoa huo.
Karne za utakatifu
"Kila jumuiya yenu inaweza kusimulia historia ya kipekee kwa maana hii, ikiibua majina yanayojulikana sana na historia zisizojulikana," Papa Leo XIV aliwaeleza mahujaji, wakiwemo Mapadre kadhaa na watawa wa kike na kiume. “Kuwaona hapa pamoja kunaleta akilini uzuri wa Mwili wa Kristo katika upatanisho wake wa rangi. Hii inasisitizwa katika mandhari ya ardhi yenu, ambapo uumbaji huungana na kazi ya mwanadamu, na sanaa na asili hufungamana.”Zaidi ya yote, hii inashuhudiwa na "karne za utakatifu" ambazo zimepambua maeneo ya mashambani ya Umbria, yakipitiwa na "wafikra na watubu, washairi na wataalimungu, watia nanga walio kimya, wanawake waliojaa imani na ujasiri, na vijana wenye shauku, ambao kutoka kizazi hadi kizazi wamepitisha urithi ule ule wa ajabu wa Injili ya Yesu," alisisitiza Papa Leo XIV.
Msukumo kwa Carlo Acutis
Ni kutokana na "mto huu wa wema" kwamba Mtakatifu kijana sana ambaye alitangazwa kuwa Mtakatifu Dominika iliyopita (Septemba 7)alichota "msukumo na nguvu," alisema Papa Leo, akimaanisha Carlo Acutis, ambaye masalia yake yamepumzika, kwa chaguo lake mwenyewe, huko Assisi, mji wa Mtakatifu Francis. Hili ni muhimu, kwa sababu linatukumbusha kwamba hazina tuliyopokea inaendelea kukua, mzabibu kuchanua na kuzaa matunda, na huo mzuri lazima uchachuke na kueneza harufu yake.
Kutangaza Uzuri
Katika kuhitimisha hotuba yake, Papa alimnukuu Papa Paulo VI: "Uzuri ni lile tunda la thamani linalopinga uharibifu wa wakati, ambalo huunganisha vizazi na kuviruhusu kushiriki katika kupendeza." Hili linakuja agizo kwa mahujaji wa Umbria kwamba: "Mmezungukwa nao, kwa njia mbalimbali: uthamini, upendeni, uache useme nanyi juu ya Mungu, na kuwa watangazaji wake kwa zamu yenu." Papa Leo aliwaalika kuonja misa ya takatifu kwa njia hii pia: wenye shukrani, umoja, makini, mshangao, na tayari kuondoka kwenye Madhabahu hayo kama wamisionari wa upendo na amani.
