Tafuta

2025.10.24 Papa akutana na wanahija wa Estonia. 2025.10.24 Papa akutana na wanahija wa Estonia.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akutana na Wanahija wa Estonia:Pongezi kwa ushuhuda wa kiekumene!

Papa Leo XIV alikutana na wanahija 250 wa Jubilei kutoka nchini Estonia na kusisitiza thamani ya kiekumene ya mpango huo,ambao unawaunganisha Wakatoliki, Walutheri na wafuasi wote wa kutangazwa kuwa mwenyeheri kwa Askofu Mkuu Eduard Profittlich,ambao ulifanyika katika mji mkuu wa Tallinn mwezi Septemba. Pia alikumbuka ushuhuda wa Askofu wa kwanza wa Estonia na sasa ndiye wa kwanza kubarikiwa kwa taifa,kinyume cha chuki kilichoonekana wakati wa mateso.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo  XIV aliwaomba waamini wapatao mia mbili  hamsini kutoka Estonia walio fika katika fursa ya hija yao ya  Jubilei  kwa bidii kwa ajili ya amani, wakati wa kukutana nao mjini Vatican tarehe 24 Oktoba 2025 na kuwashukuru kufika Roma wakati wa Mwaka Mtakatifu kusherehekea uhusiano wa karibu wa Kanisa katika ardhi ya Estonia na Mrithi wa Mtakatifu Petro, kwa matumaini kwamba vifungo hivi vitaimarishwa zaidi.

Papa alianza hotuba hiyo kwa kuonesha furaha sana ya kuwakaribisha Roma katika hafla ya hija yao wakati wa Mwaka huu wa Jubilei unaozingatia fadhila ya kitaalimungu ya matumaini. Aliomba kwamba wanapotembelea maeneo mbalimbali matakatifu, tumaini lao katika ahadi za Bwana liimarishwe ili waweze kurudi nyumbani wamejaa furaha na  tayari, walikuwa tayari na furaha hapo na tunasherehekea zawadi hiyo ya uzima!,  na natumaini kwamba watakuwa tayari kushiriki imani yao na wale wanaokutana nao kwa kutangaza Injili kwa njia rahisi kila siku.

Papa akutana na wanahija wa Estonia
Papa akutana na wanahija wa Estonia   (@VATICAN MEDIA)

Kwa njia maalum, aliwasalimu makuhani wawili waliowekwa wakfu hivi karibuni. Papa ameapongeza. “Mungu awabariki kila wakati. Ukarimu wao katika kusema ndiyo kwa wito wa Bwana wa kumtumikia yeye na Kanisa kama wahudumu waliowekwa wakfu wa Injili ni ishara ya matumaini kwa jamii ya Kikristo katika nchi yao. Mwitikio wao kwa wito wao uwatie moyo wengine wengi kufanya vivyo hivyo!,” Papa aliwashauri.

Ishara nyingine ya matumaini ni kuinuliwa kwa Kanisa lao la karibu, hadi kiwango cha Jimbo, karne moja baada ya kuanzishwa kwake kama Uwakilishi wa Kitume na karibu miaka 500 baada ya kutoweka kwa Kiti cha kale cha Tallinn. Uwepo wao umempa Papa Leo XIV fursa ya kuwapongeza wote  ana kwa ana, na kuwatia moyo kuombeana, na hasa kwa ajili ya Askofu wao, ambaye aliwasalimu kwa uchangamfu, ili umoja wao  kama jumuiya ya imani iweze kulishwa na Bwana na kuvutia waamini wapya.

Wanahija wa Estonia
Wanahija wa Estonia   (@VATICAN MEDIA)

Ni vizuri sana kwamba wana uwezo, kwa niaba ya kaka na dada zao wote huko Estonia, na kutoa shukrani kwa Mungu jijini  Roma kwa neema hii maalum iliyotolewa na Mungu Mwenyezi, na kusherehekea uhusiano wa karibu wa Kanisa katika nchi yao na Mrithi wa Mtakatifu Petro. “Ni matumaini yangu kwamba uhusiano huu utakuwa na nguvu zaidi kutokana na hija yenu.” Papa Leo  XIV alieleza anavyojua pia kwamba miongoni mwao kuna baadhi ya waamini wa Kanisa la Kilutheri la Estonia, pamoja na wengine wasio Wakatoliki, wakiwemo kundi la wale waliounga mkono kwa ukarimu maandalizi ya kutangazwa kuwa mwenyeheri kwa Askofu Mkuu Eduard Profittlich, ambayo ilifanyika katika Uwanja wa Uhuru wa mji mkuu wao mwezi uliopita Septemba.

Picha ya pamoja na wanahija wa Estonia
Picha ya pamoja na wanahija wa Estonia   (@VATICAN MEDIA)

Ushuhuda wao wa kiekumene, ambao unaweza kukua tu kupitia kuhiji pamoja, ni kielelezo kinachokaribishwa cha ushuhuda wa Mwenyeheri Eduard mwenyewe, na ni kinyume kabisa cha chuki iliyokuwa ikionekana kwa njia ya kusikitisha wakati wa mateso ya serikali ya Kisovieti kwa Kanisa.Baba Mtakatifu alisema kuwa “leo hii kama wanavyojua vyema, bado tunaona mantiki ya vita ikiendelea barani Ulaya, na ningewaomba muombe kwa bidii kwa ajili ya amani, hasa wakati uliobaki wa muda wenu huko Roma. Wapendwa marafiki, asanteni kwa ziara yenu. Mnaporudi majumbani mwenu, tafadhali mjue kwamba mnafanya hivyo pamoja na sala zangu.

Kwa namna fulani, ninawaomba mpeleke salamu zangu za joto kwa wanafamilia wenu na marafiki zenu. Waambieni kwamba Papa anawaombea!”Papa kwa kuhitimisha alisema “Na kwa hisia hizi, ninawakabidhi kila mmoja wenu kwa maombezi ya Maria, Mama wa Kanisa. Asanteni. “Papa Leo alisali nao  ya Baba Yetu pamoja na kuwatakaia hija njema na Mungu awabariki wote.

24 Oktoba 2025, 16:18