Tafuta

2025.09.10 2025.09.10 Waraka wa Kitume Dilexi Te yaani "Nimekupenda". 2025.09.10 2025.09.10 Waraka wa Kitume Dilexi Te yaani "Nimekupenda".  Tahariri

Petro anatukumbusha kuwa maskini ni moyo wa Injili

Waraka wa Kitume wa Papa Leo XIV:Andiko linalopendekeza misingi ya Uonesho wa Kikristo na wa utamaduni wa Kanisa.

Andrea Tornielli

Dilexi te, Waraka wa kwanza wa Kitume wa Papa Leo XIV, kuanzia na kichwa chenyewe kinaunganisha Waraka wa mwisho wa Papa Francisko, Dilexit nos (Oktoba 2024)na unawakilisha, kwa namna moja, mwendelezo. Hili si andiko la Mafundisho ya kijamiii ya Kanisa, haliingiliani na tathimini ya matatizo maalum. Unapendekeza zaidi ya yote misingi ya Uonesho, kujikita na uwazi wa nguvu yake ambayo ipo kati ya upendo wa Kristo na wito wake wa kutufanya kuwa karibu na maskini. Kitovu cha upendo kwa maskini kiukweli ni moyo wa Injili yenyewe na auwezi kushuka daraja kama vile kimpira kidogo cha baadhi ya Mapapa au aina za kisasa za kiitikadi, na hauwezi kuwakilishwa kama matokeo ya kijamii na kibinadamu ya nje ya imani ya kikristo na katika tangazo lake

Matokeo kwa ajili ya Bwana yanaunganisha yale ya maskini, anaandika Papa Leo. Kwa njia hiyo isiyoweza kutengenishwa: “Yote mliyomtendea mmoja wa ndugu hawa wadogo zaidi, mlinitendea mimi” anasema Yesu. Kwa njia hiyo hapa “hatuko katika upeo wa ufadhili, bali Uonesho: Kuwasiliana na yule ambaye hana uwezo na ukuu ni njia msingi ya kukutana na Bwana wa Historia.” Papa anabainisha kuwa kwa bahati mbaya, hata kwa Wakristo wana hatari ya kufanya “kuambukiza, na tabia za kidunia, itikadi na maono ya kisiasa, na kiuchumi ya kupotosha. Kero ambayo mara nyingi inasikika ikizungumzwa katika jitihada kwa masikini, karibu kusema kuwa heshima ya hovyo kwa upendo na kwa ibada inayoelekea kwa Mungu, kuonesha jinsi gani hati hiyo ni muhimu.

Kutokana na kwamba zoezi la upendo linaonesha kudharauliwa au kuchekwa, kama vile utafikiri ni kukariri baadhi, kama kiungo kinachong’aa cha utume wa kikanisa, unanifanya nifikirie, anathibitisha Papa Leo XIV, kwamba kuna haja daima na mpya ya kusoma Injili, ili kusiwe na hatari ya kuibadilisha katika mantiki ya kidunia.” Kwa njia ya rejea za kibiblia na tafakari za Mababa wa Kanisa, inatujia akilini kukumbuka kwamba upendo kwa masikini hakuwezi kuwa “mchakato mbadala”, bali unawakilisha kigezo kuelekea ibada. Kwa kuakisi hata kwa ajili ya leo hii ya Kanisa, kuna mifano ya maneno ya Mtakatifu Yohane Crisostom na Mtakatifu Agostino.

Wa kwanza anaalika kuheshimu Yesu katika mwili wa maskini kwa kijiuliza ina maana gani kuwa kwa ajili ya wengine huku kwa kujaza vikombe vya dhahabu, wakati Kristo anakufa na njaa mara tu unapotoka nje ya Kanisa; wa pili anamwelezea maskini kama: “uwepo wa Sakramenti ya Bwana”, kwa kuona unamtunza mskini, ni jaribio la dhati la kweli na la imani: “Anayesema kupenda Mungu na bila kuwa na huruma akilini kwa  yule mwenye kuhitaji. Kwa nguvu ya uhusiano huu na ujumbe wa sasa wa kikristo, katika sehemu ya mwisho ya Dilexi te ni maudhui yanayotoa mwaliko kwa kila mbatizwa ili ajikite  kwa dhati kwa ajili ya kutetea na kuhamasisha walio dhaifu zaidi: Ni kazi ya wote wajumbe wa Watu wa Mungu kufanya kusikika sauti ambayo imshe, na kutangaza, na kujielezea.” Hata kwa gharama ya kutazamwa kama “wajinga.”

Ujumbe ni wa kina wa matokeo kwa ajili ya maisha ya kikanisa na kijamii: wa sasa katika mfumo wa uchumi, kifedha na miundo yake yote ya dhambi, ambayo haiepukiki na kwa hiyo uwezekano wa kujitahidi kufikiria na kujenga, kwa nguvu za wema, jamii tofauti na usawa kwa njia ya “mabadilishana ya kiakili lakini hata kwa msaada wa sayansi, na ufundi, kwa njia ya maendeleo ya kisasa ya dhati katika kubadilika kwa jamii.” Waraka wa ulikuwa umeanza kuandaliwa na Papa Francisko. Kwa kufanya kuwa wake ni mfuasi wake Papa Leo XIV, ambaye kama Mtawa, na baadaye Askofu Mmisionari, alishirikishana kwa sehemu kubwa ya maisha yake na walio wa mwisho na kuacha ainjilishwe na wao.

Tahariri ya Tornielli

Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here

09 Oktoba 2025, 12:05