Tafuta

Papa Leo XIV atafanya ziara ya kitume nchini Urutuki na Lebanon. Papa Leo XIV atafanya ziara ya kitume nchini Urutuki na Lebanon.  (@Vatican Media)

Leo XIV,Ziara ya kwanza ya Uturuki na Lebanon,Novemba 27 hadi Desemba 2

Ziara ya kwanza ya kitume ya Papa Leo XIV imetangazwa,ikijumuisha hija ya İznik,Nicea ya kale,kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kiekumene.Papa anatimiza matashi ya mtangulizi wake Hayati Papa Fransisko,ambaye,kama alivyosema mara nyingi,alitaka kusherehekea ukumbusho muhimu.Pia Papa atakwenda katika nchi ya Mwerezi huko Lebanon.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV akipokea mwaliko wa Mkuu wa Nchi na Mamlaka za kikanisa nchini, atafanya Ziara ya Kitume nchini Uturuki kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba,  kwa kufanya hija ya Iznik katika maadhimisho ya miaka 1700 ya Baraza la Kwanza la Nicea. Haya yamesemwa na Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican, Jumanne tarehe 7 Oktoba 2025.

Baadaye,  imebainisha kwamba "Baba Mtakatifu akiitikia mwaliko wa Mkuu wa Nchi na mamlaka ya kikanisa ya nchi ya Lebanon, atafanya Ziara ya Kitume nchini humo kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 2 Desemba 2025. Mpango wa Safari utatangazwa kwa wakati ufaao."

Kutimiza matashi ya Papa Francisko

Hivyo Papa Leo XIV atatimiza matashi ya mtangulizi wake ya kusherehekea ukumbusho muhimu wa Mtaguso wa kwanza katika historia, akiwa na Patiaki wa kwanza wa Konstanopoli pamoja na maaskofu na Mapatriaki wa Kanisa katika sehemu moja ya kusanyiko, na nuingine  Nchi ya Mashariki ya Kati na, zaidi ya yote, kuwatembelea watu wa Lebanon. Vituo viwili, basi, katika safari ya kwanza ya kimataifa ya Papa, ambayo maelezo yake yatatangazwa baadaye. Ya kwanza itakuwa Uturuki kwa ajili ya ukumbusho wa Nicea, mahali ambapo Mababa waliidhinisha kanuni ya  Imani itunayosali sisi sote wakristo.

Kama inavyojulikana, Papa Francisko alielezea hamu yake kwa hafla kadhaa za  katekesi na mikutano kutaka kusafiri hadi Uturuki mnamo Mei na kushiriki katika maadhimisho hayo, pamoja na kaka yake "mpendwa" Bartholomew, Patriaki wa Constantinople. Hata baada ya kupona kwa muda mrefu katika Hospitali ya Gemelli, Papa  aliwaomba washirika wake wamruhusu kuondoka kwenye safari yake ya mwisho, bila kujali hali yake ya kimwili.

Ziara ya Papa Leo Uturuki na Lebanon

Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kusasishwa zaidi, jiandikishe katika makala za kila siku kwa kubonyeza hapa: Just click here

07 Oktoba 2025, 17:23