Tafuta

Wakati wa kufunga Mtaguso wa Vatican II kunako 1965 Wakati wa kufunga Mtaguso wa Vatican II kunako 1965  

Mapapa na “Nostra aetate:”watu wawe ndugu wanaotembea pamoja

Imepita miaka 60 tangu tamko kuhusu mahusiano ya Kanisa na dini zisizo za kikristoTafakari na sauti za Mapapa katika hati hiyo kuanzia na ile ya Papa Paulo VI,kwa wote wanasisitiza udugu wa wanadamu kwa ujumla.

Na Amedeo Lomonaco – Vatican.

“Nostra aetate”, ambayo inaadhimisha miaka 60 yake, ni Tamko kuhusu Mahusiano ya Kanisa Katoliki na Dini Zisizo za Kikristo. Hati hii(documento,) iliyoidhinishwa na Mababa wa Mtaguso wa Pili wa Vatican na kutangazwa na Papa Paulo VI, inachukuliwa kuwa maandishi ya msingi ya mazungumzo na imani zingine za kidini. Chapisho lake, mnamo tarehe 28  Oktoba  1965, lilitanguliwa hata kabla ya kuandikwa kwake na mkutano: ule kati ya Papa Yohane  XXIII na mwanahistoria wa Kiyahudi Jules Isaak, ambaye mnamo tarehe 13 Juni  1960, alimkabidhi Papa Denkschrift, mkusanyiko wenye ombi la kukuza maono mapya ya uhusiano kati ya Kanisa na Uyahudi. Ulikuwa wakati ambapo majeraha yaliyosababishwa na Vita vya Pili vya Dunia kwa wanadamu yalikuwa bado makubwa.

Haiwezekani kufanya bila Mungu

Hati ya “Nostra aetate” Ilizaliwa katika muktadha wa kihistoria kufuatia Mauaji ya Kimbari, yaani, jaribio la Ujerumani ya Kinazi ya kulazimisha ukuu wake na kuwaangamiza Wayahudi. Na mara moja inazungumzia kipengele kikuu cha jamii ya wanadamu: kutegemeana kwa watu mbalimbali. Aya ya utangulizi inaalika kutafakari kile ambacho watu wanafanana. Kuna  marejeo mengi ya Maandiko Matakatifu kuonesha kwamba familia nzima ya wanadamu ina asili moja: mpango wa Mungu wa wokovu na upendo wa huruma unamkumbatia kila mtu. Tofauti zinatambuliwa, lakini umoja wa msingi unatambuliwa: "Watu mbalimbali," inasomeka, "huunda jumuiya moja. Wana asili moja, kwa kuwa Mungu amesababisha jamii nzima ya wanadamu kukaa juu ya uso mzima wa dunia." Haiwezekani kumpuuza Mungu, Papa Paulo VI anasisitiza. Katika Katekesi yake tarehe 10 Desemba 1968(’udienza generale del 18 dicembre 1968.)

Hatusemi kwamba kabla ya Yesu Kristo, Mungu hakujulikana: Agano la Kale tayari ni ufunuo, na huunda wafuasi wake katika hali ya kiroho ya ajabu na halali kila wakati: Hebu fikiria Zaburi, ambazo bado hulisha sala ya Kanisa leo kwa utajiri usio na kifani wa hisia na lugha. Hata katika dini zisizo za Kikristo, mtu anaweza kupata unyeti wa kidini na ujuzi wa Umungu, ambapo Mtaguso ulitushauri kuheshimu (tazama Azimio la Nostra Aetate).

Heshima ya pande zote kati ya Wakristo na Wayahudi

Nguvu ya hati hii na maslahi yake ya kudumu inatokana na ukweli kwamba "inazungumza na watu wote na watu wote kutoka kwa mtazamo wa kidini." Papa Yohane  Paulo II, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya "Nostra Aetate", tarehe 6Desemba 1990 (il 6 dicembre del 1990), kwa Wajumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Wayahudi ya Mashauriano ya Dini Mbalimbali na wajumbe wa Tume ya Mahusiano ya Kidini na Wayahudi, ambapo alisisitiza uhai wa maandishi haya "mafupi lakini muhimu" wa  hati hiyo  ambayo pia inachukuliwa kama wakati muhimu katika uhusiano kati ya Kanisa na dini ya Kiyahudi.

Kanisa la Kristo," tunasoma katika "Nostra Aetate," "linatambua kwamba mwanzo wa imani yake na kuchaguliwa kwake tayari vimepatikana, kulingana na fumbo la kimungu la wokovu, katika mababu, katika Musa, na katika manabii." Uwazi wa Nostra Aetate kwa wote umejikita na hutoa mwelekeo wake kutoka kwa hisia ya kina ya upekee kabisa wa uchaguzi wa Mungu wa watu fulani, watu "wake", Israeli kulingana na mwili, ambao tayari wanaitwa "Kanisa la Mungu" (Lumen Gentium, 9); (taz. Neh 13:1; taz. Hes 20:4; Kum 23:1 na kuendelea). Kwa hivyo, tafakari ya Kanisa kuhusu utume wake na asili yake ya kweli inahusiana kindani na tafakari juu ya ukoo wa Ibrahimu na asili ya watu wa Kiyahudi (taz. Nostra Aetate, 4). Kanisa linafahamu kikamilifu kwamba Maandiko Matakatifu yanashuhudia kwamba watu wa Kiyahudi, jumuiya hii ya waumini na walinzi wa mapokeo yenye umri wa maelfu ya miaka, ni sehemu muhimu ya "siri" ya ufunuo na wokovu.

Heshima ya Kanisa kwa Waislamu

"Nostra Aetate" inaendelea kuwatia moyo washiriki wa Kanisa Katoliki, katika ngazi mbalimbali, kukuza uhusiano wa heshima na mazungumzo na watu wa imani zingine. Kuhusu Uislamu, hati hiyo inasisitiza kwamba "Kanisa pia linawaheshimu Waislamu, wanaomwabudu Mungu mmoja, aliye hai na anayeishi, mwenye huruma na mwenye nguvu zote, muumba wa mbingu na dunia, ambaye amesema na wanadamu." Miaka arobaini baada ya kuchapishwa kwa Tamko kuhusu Mahusiano ya Kanisa na Dini Zisizo za Kikristo, Papa Benedikto XVI katika Sala ya  Malaika wa Bwana, tarehe 30 Okotba 2005 (30 ottobre del 2005), alisisitiza kwamba hati hii haijapoteza umuhimu wake wowote.

Ni wakati muafaka sana kwa sababu inahusu mtazamo wa jumuiya ya kanisa kuelekea dini zisizo za Kikristo. Kuanzia kanuni kwamba "watu wote huunda jumuiya moja" na kwamba Kanisa "lina wajibu wa kukuza umoja na upendo" miongoni mwa watu, Baraza "halikatai chochote kilicho cha kweli na kitakatifu" katika dini zingine na linamtangaza Kristo kwa wote, "njia, ukweli, na uzima," ambaye ndani yake watu hupata "ukamilifu wa maisha ya kidini." Kwa Tamko  la Nostra Aetate, Mababa wa Mtaguso II wa  Vatican  walipendekeza ukweli fulani wa msingi: walikumbuka waziwazi kifungo maalum kinachowaunganisha Wakristo na Wayahudi, walithibitisha tena heshima yao kwa Waislamu na wafuasi wa dini zingine, na kuthibitisha roho ya udugu wa ulimwengu wote ambayo inapiga marufuku ubaguzi wowote wa kidini au mateso.

Mchango wa Uhindu, Ubuddha, na Dini Nyingine

"Nostra Aetate" pia inaakisi mchango wa dini tofauti: "Katika Uhindu," hati hiyo inasema, "wanadamu huchunguza fumbo la kimungu na kulielezea kupitia matunda yasiyoisha ya hadithi za uongo na uchunguzi wa kina wa falsafa." Katika Ubuddha, "upungufu mkubwa wa ulimwengu huu unaobadilika unatambuliwa na njia inafundishwa ambayo watu, wenye mioyo ya kujitolea na inayoamini, wanaweza kufikia hali ya ukombozi kamili." Dini zingine, tamko hilo linakumbuka, pia hujitahidi kushinda "kutotulia kwa moyo wa mwanadamu kwa kupendekeza njia, yaani, mafundisho, kanuni za maisha, na ibada takatifu."

Udugu wa Ulimwenguni

"Hatuwezi kumwita Mungu kama Baba wa watu wote ikiwa tunakataa kuishi kama ndugu kwa baadhi ya wanadamu, ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu." Sura ya mwisho ya "Nostra Aetate" inaanza kwa maneno haya. Katika tukio la maadhimisho ya miaka 50 ya kutangazwa kwa tamko la  hati hiyo, Papa Francisko alihutubia katika katekesi yake ya tarehe 28 Oktoba 2015(28 ottobre 2015, inaelekeza njia ya Udugu.  "Sisi ni ndugu," Papa alithibitisha, akihutubia Wayahudi na Waislamu, Wahindu na Wabudha, Wajaini na Wasikh, wawakilishi wa Ukonfusimu, Watenrikyo, na dini za kiutamaduni za Kiafrika.

"Sisi ni ndugu," tukiwa tumeitwa kutembea katika njia ya mazungumzo, Papa wa Argentina alisisitiza tarehe 4 Februari 2019(4 febbraio del 2019) pamoja na Imam Mkuu wa Al-Azhar, walitia saini "Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Amani Duniani na Kuishi Pamoja."

Mazungumzo tunayohitaji yanaweza kuwa wazi na ya heshima tu, na kisha yanafanikiwa. Kuheshimiana ni hali na lengo la mazungumzo ya kidini: kuheshimu haki za wengine za maisha, uadilifu wa kimwili, na uhuru wa msingi yaani, uhuru wa dhamiri, mawazo, kujieleza, na dini. Ulimwengu unatutazama sisi waamini, ukituhimiza kushirikiana na wanaume na wanawake wenye mapenzi mema ambao hawadai dini yoyote, na kudai majibu yenye ufanisi katika masuala mengi: amani, njaa, umaskini unaowasumbua mamilioni ya watu, mgogoro wa mazingira, vurugu, hasa zile zinazofanywa kwa jina la dini, ufisadi, kuoza kwa maadili, migogoro ya familia, uchumi, fedha, na, zaidi ya yote, mgogoro wa matumaini. Sisi waamini hatuna suluhisho la matatizo haya, lakini tuna rasilimali kubwa: sala. Na sisi waumini tunaomba. Lazima tuombe.

Kusali Pamoja

Mwaka huu, ili kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Tamko  kuhusu Mahusiano ya Kanisa na Dini Zisizo za Kikristo, mkutano maalum wenye kichwa: "Kutembea Pamoja katika Tumaini" unafanyika tarehe 28 Oktoba 2025 kuanzia saa 12:30 za jioni hadi saa 2:00 usiku masaa ya Ulaya,  katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican. Kilele cha tukio hilo ni hotuba ya Papa Leo XIV, ikifuatiwa na sala ya kimya kimya ya amani. Safari hii ni mojawapo ya alama za hati hiyo. Tangu kuchapishwa kwake, "Nostra Aetate" imethibitika kuwa hatua muhimu katika mahusiano na dini zingine. Kufuatia hati hii, mipango na mikutano muhimu imefanyika kwa miaka mingi, kama vile ile iliyofanyika Assisi, iliyoitishwa na Mtakatifu Yohane  Paulo II.

Kunako tarehe 27 Oktoba 1986 (27 ottobre 1986,) katika jiji la Mtakatifu Francis wa Assisi, Papa Wojtyła aliita tukio hilo, lililohudhuriwa na viongozi wa kidini wa imani tofauti, "ishara yenye ufasaha sana kwa ajili ya amani." Kwa kufuata njia ya "Nostra Aetate," ahadi hii ya pamoja imeimarika, na mazungumzo kati ya dini mbalimbali yamezidi kuchukua ladha ya sala.

28 Oktoba 2025, 11:18