Papa akutana na Rais wa Shirikisho la Uswiss
Vatican News
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican ilibanisha kwamba Baba Mtakatifu Leo XIV,alikutana na Rais wa Shirikisho la Uswiss, Bi Karin Keller-Sutter, asubuhi tarehe 3 Oktoba 2025, katika Jumba la Kitume mjini Vatican.
Bi Keller-Sutter baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Majadiliano katika Sekretarieti ya Vatican yalilenga juu ya "mahusiano mazuri na yenye matunda ya nchi mbili," na "dhamira ya ukarimu na ya kitaaluma ya Walinzi wa Kipapa wa Uswisi" ilikumbukwa.
Matukio ya sasa pia yalijadiliwa, hasa masuala ya kimataifa na maeneo yenye maslahi ya pamoja, kwa kurejea hasa matarajio ya amani baada ya kumalizika kwa vita vya Ukraine na Gaza.
Kwa upande wa Zawadi Papa alimkabidhi Rais wa Shirikisho la Uswiss, Karin Keller-Sutter, bamba la shaba lililochongwa katika picha ya ushairi, mojawapo ya taswira zilizochorwa na Raphael Sanzio kwenye chumba cha kutia saini katika Jumba la Kitume la Vatican kati ya 1508 na 1511. Sehemu ya mzunguko wa mapambo, Ushairi unashikilia kinubi na kitabu, alama za maelewano na uumbaji wa fasihi. Kimeandamana na makerubi wawili wenye maandishi "Numine Afflatur" ("Imeongozwa na Mungu"), usemi unaokumbuka imani ya kale kwamba ushairi si uwezo wa kibinadamu tu, bali ni zawadi iliyopuliziwa kutoka juu.
Wakati huo huo Rais wa Uswissi alimkabidhi Papa sanamu ya Mtakatifu Wiborada, mwanamke wa kwanza kutangazwa na Papa Clement II, aliyemtangaza Mtakatifu katika sherehe kuu ya mnamo 1047 mbele ya Mfalme wa Ujerumani Henry III.
Wiborada alizaliwa katika familia yenye hadhi mwishoni mwa karne ya 9 huko Thurgau, Uswiss ya leo, alijitolea maisha yake kuwatunza maskini na wagonjwa, na baadaye akaamua kustaafu maisha ya utawa katika moja ya Monasteri ya Mtakatifu Gallo. Aliuawa wakati alikuwa akisali mnamo Mei 926, wakati wa uvamizi wa Magyar. Anaoneshwa akiwa na kitabu, kinachoashiria maandishi ya thamani ya maktaba ya monasteri ambayo aliweza kuokoa kutokanana na wavamizi, na halberd, na silaha ambayo ilitumika kumuua.
Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here
