Papa Leo XIV ndani ya Meli ya shule ya Amani:Ninyi ni Tumaini katika Ulimwengu uliogawanyika
Na Salvatore Cernuzio – Ostia
"Jifunzeni kuwa wapatanishi wa amani, jifunzeni kuwa waendelezaji wa amani katika ulimwengu ambao unaelekea zaidi kwenye vurugu, chuki, utengano, umbali na ubaguzi." Ni Sauti ya Papa Leo XIV iliyovuma kwenye upepo wa Ufukwe wa Ostia ikivuma kwenye ukingo wa Meli ya Med25 Bel Espoir ambapo Papa aliingia ndani, akizungumza kwa kipaza sauti. Ni siku ya Ijumaa 17 Oktoba 2025 alasili alikwenda huko Pwani ya Ostia, nje kidogo ya jiji la Roma, kutembelea Meli ya Shule ya Amani. Karibu naye kulikuwa na vijana 25 na wanawake na wanaume, wafanyakazi wa chombo hicho cha zama za 1940, che urefu wa mita 29 na vitanda 35. Meli hiyo ikipeperusha bendera ya Ufaransa, imekuwa ikisafiri kutoka bandari moja hadi bandari kwa muda wa miezi minane, ikipeleka ujumbe wa udugu kwenye njia panda za kukutana na mazungumzo ya Mediterania.
Hawa wanatoka Bosnia na Algeria, kutoka Hispania na Palestina, kutoka Ufaransa na Pakistan, na wamesimama katika Valletta, Tunis, Krete, Istanbul (ambako walikutana na Patriaki Bartholomew I), Ravenna, na Napoli. Walitakiwa kusafiri kwenda Civitavecchia, lakini walibadilisha ratiba yao kwa pendekezo la Papa Leo mwenyewe. Katika Mkutano wa hivi karibuni na Kardinali Jean-Marc Aveline wa Jimbo Kuu Katoliki la Marseille, nchini Ufaransa, mwanzilishi wa mpango huo na aliyekuwepo pia alasiri hiyo, Papa Leo alikuwa amemwambia kwamba ikiwa wangeingia na kusimama Ostia, labda angeweza kuwafikia.
![]()
Papa alitembelea Meli ya Shule ya Amani huko Ostia (@Vatican Media)
Ostia, ardhi ya "Agostino"
Ostia, ni eneo linalojulikana kwa Papa Leo XIV. Eneo la ibada ya kina kwa Mtakatifu Agostino na mama yake Mtakatifu Monica, kama inavyothibitishwa na sanamu, makanisa, na hata zahanati zilizopewa majina yao. Papa mwenyewe, katika maelezo yake mafupi kwa lugha ya Kiitaliano, anathibitisha hili: “Ostia kiukweli ni bandari muhimu katika historia ya ulimwengu, katika historia ya Kanisa, katika historia ya Mtakatifu Agostino na Mtakatifu Monica.” Papa aliendelea kusema “Kwa kuwa Mimi Mwagostino, nimekuja eneo hili mara nyingi, kwa sababu Ostia daima imekuwa bandari muhimu sana, na ni muhimu sana leo hii kwa sababu yenu. Na asante kwa kuwa hapa. Nina wasalimu nyinyi nyote katika mchana huu mzuri.”
"Sisi sote ni wanadamu ..."
Vijana walitabasamu. Wengi wao walizungumza Kifaransa, lakini wote pia wanazungumza Kiingereza. Walimkaribisha Papa bila viatu wengine wakiwa wamevaa kandambili, nguo zao za kawada, ndefu, wengine ushungi na kofia. Wengine walivaa, kaptula za Bermuda, sweta, shirts, na mashati ya kitani. Wote walikuwa tofauti, lakini wote wameungana; wote wakitaka kutuma ishara ya umoja. Aina ya ushirika ambao Papa mwenyewe katika matamshi yake kwa lugha ya Kiingereza aliwaomba waendeleze. “Tunaweza kuungana hata kama tunatoka nchi tofauti, tuna lugha tofauti, tamaduni tofauti, dini tofauti, na bado sisi sote ni wanadamu.”
![]()
Papa huko Ostia (@Vatican Media)
Tumaini jema
"Nimefurahi sana kufika hapa alasiri ya leo na kuwa sehemu ya wakati huu mfupi na safari hii ndefu ambayo ninyi na vijana wengine wengi mmefanya katika kipindi hiki cha hivi karibuni,” Papa alisema, akiwashukuru kwa zawadi alizopokea, ikiwa ni pamoja na mchoro wa meli, Kitabu Nyeupe cha Mediterania, na ramani iliyotiwa saini na vijana wote. Makofi yalichanganyikana na sauti ya mawimbi yaliyoanguka dhidi ya miamba yenye tabia ya Ostia. Hewa ilijaa harufu ya chumvi na samaki wa kukaanga kutoka kwenye bar na migahawa iliyoko maeneo hayo.
Nguzo tatu za meli (ambazo baadhi ya vijana walipanda ili kupiga picha) kulikuwa na mahali pa kujikinga na joto la jua, ambalo liliongezeka mara tu Papa Leo XIV alipotoka kwenye gari lenye vioo vyeusi saa 10:10 jioni. Ishara ya kwanza, ilikuwa salamu kwa Mamlaka ya Bandari na Kamanda wa Walinzi wa Pwani, ikifuatiwa na kupeana mkono na kuzungumza na Kardinali Aveline na Monsinyo Alexis Leproux.
Yote haya yalianzia huko Marseille, yakichochewa na ziara ya Papa Francisko mnamo Septemba 2023. Akitazama juu ya maji ya Mediterania, Papa wa Argentina alizindua ombi kubwa la kurejesha "Mare Nostrum," yaani “bahari yetu”ambayo ilikuwa na ni ya "Mortum” yaani Kifo" na vita na janga la uhamiaji. Vijana wa Bel Espoir walikubali agizo hilo na kuanza safari kwenye Bel Espoir,yaani "Tumaini Jema." Matumaini ya kufanya jambo zuri katika ulimwengu huu ambapo wenzao wamezoezwa kupigana na kuua, hata ikiwa ni kuimba tu pamoja, kujifunza kuendesha meli au kukunjua matanga, kupika vyakula vya kiutamaduni na kufundisha wengine mapishi. Ishara ndogo za kuonesha kwamba inawezekana kuishi pamoja, licha ya ugumu wa kuishi pamoja, na licha ya umbali wa kijiografia na kiutamaduni.
![]()
Baraka ya Papa kwa wanafunzi wa shule ya Amani (@Vatican Media)
Ishara, zaidi ya Maneno
"Ulimwengu wa leo unahitaji ishara zaidi ya maneno. Maneno ya ushuhuda ambayo yanatoa tumaini. Kutokana na jina lenyewe la mtumbwi huo na pia kutokana na uwepo wenu nyote hapa leo," Papa anathibitisha, “Ninyi ishara ya matumaini kweli kwa Mediterania na kwa ulimwengu.
“Peace, pace, mir. Paz, salam.. Bel Espoir… Peace, paci, paix. Love we share in unity,” Vijana walijibu kwa wimbo, wimbo ambao karibu umezoeleka kwa masaa mengi ambayo walitumia wakimsubiri katika ziara ya Papa: kutoka katika matembezi ya awali hadi sehemu ya mbali zaidi ya bandari na wakati wa safari ya Mtumbwi huo, Papa Leo XIV alitumia muda wa kuwajua vijana mmoja baada ya mwingine, akiuliza kila mmoja jina na nchi yake ya asili. “Nilimuuliza kila mmoja wao kimakusudi, huku nikizunguka kuwasalimia: ‘Ninyi, mmetoka wapi?’” Papa mwenyewe alieleza.
"Nilifanya hivyo ili kujua jinsi uzoefu ulivyo mzuri wa kukutana na watu, wakati mkisafiri kihalisi kuvuka Mediterania kutoka nchi tofauti, tamaduni tofauti, lugha tofauti, na bado tulipata njia ya kuifanya, na kwa njia ya kibinadamu."
![]()
Papa alifika katika Meli ya shule ya amani (@Vatican Media)
Mazungumzo, madaraja, amani
Papa aliwaachia vijana "mawazo" matatu kama miongozo ya matendo yao: "Mazungumzo," "madaraja" na "amani." “Ni muhimu kujifunza kuzungumza na wenzetu, kuketi chini, kusikiliza, kueleza mawazo na maadili yetu, na kuheshimiana ili wengine wahisi kusikilizwa kiukweli.” “Kuheshimiana,” Papa Leo XIV alirudia, “hii ni ishara ya tumaini hakika.” Na kwa njia ya mazungumzo, madaraja yanajengwa: "Si lazima daraja la Mediterania, lakini daraja kati yetu sote, watu wa mataifa mengi tofauti," Papa alisisitiza.
Nina hakika kwamba watu wengi sana wanaoishi kwenye mtumbwi mdogo kama huu… Bado sijashuka… Ni lazima mjifunze kuishi pamoja, kuheshimiana, na kushinda matatizo. Na hii pia ni uzoefu mzuri kwa nyinyi vijana wote, lakini ni jambo ambalo mnaweza kutufundisha sisi sote.
![]()
Papa alitembelea shule ya Amani: hili ni jiko (@Vatican Media)
"Kujifunza kuwa wapatanishi"
Hatimaye, neno la tatu, “ambalo ni muhimu sana, na baadhi yenu mliniambia kwamba mwingine ni Mpalestina, ni kujifunza kuwa wapatanishi,” kwa sababu “sisi sote ni wana na binti wa Mungu mmoja. Sote tunaishi pamoja katika Ulimwengu huu na sote tuna wajibu wa pamoja: kutunza uumbaji, kujaliana, na kuendeleza amani duniani kote.” “Hongereni sana!” Askofu wa Roma alipaza sauti, na kusema “asante” kwa “kuchangia ishara hii kwa ajili ya ulimwengu, ambayo kiukweli inatupatia matumaini sisi sote.” Naomba kizazi chenu na vijana wengine wengi kama ninyi uendelee kukuza aina hii ya mpango, ambao kwa hakika utakuza amani duniani kote... Asante, asante, asante.”
![]()
Hii ni Meli ya Shule ya Amani iliyosimama huko Ostia (@Vatican Media)
![]()
Meli ya Shule ya amani ilisimama Ostia (@Vatican Media)
Vijana hao walipiga makofi zaidi, basi Papa aliingia kwenye umiliki wa "Med25 Bel Espoir." Mara moja baadaye, katika "chumba cha kulia," wakati wa faragha na baadhi ya vijana wa kiume na wa kike kwenye bodi. Kati ya kunywa kahawa na kutafuna pancakes na "zvienoiserie," mapishi yaliyotengezwa na mtaalamu wa Kifaransa wa brioche za chokoleti, ambpo Papa Leo alisikiliza uzoefu na ushuhuda kadhaa:
“Alikuwa Papa lakini pia baba... Alizungumzia amani, ya utofauti, alisema kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu mmoja, kwamba kila mmoja ana njia yake na njia yake ya kusali, lakini sisi sote ni binadamu na tunaweza kuishi pamoja,” alisema Leila kutoka Oran, Algeria.
![]()
Papa akiwa ndani ya Meli ya Shule ya amani (@Vatican Media)
Papa Leo XIV pia alijibu baadhi ya maswali, akishangazwa na ukina cha vijana hao, hasa Hannan, kutoka Bosnia, ambaye alisema: "Sote tuko katika mtumbwi mmoja ndogo, na kwa nini hatuwezi kuishi hivi katika ulimwengu mkubwa?" Hatimaye picha ya pamoja na kuimba zaidi kunaonesha hitimisho la ziara hiyo, majira ya saa 11:00 jioni, Papa Leo alipanda gari kurejea mjini Vatican huku vijana wakipanga foleni. Au tuseme, kuamka, kama ile Bel Espoir ikiondoka kwenye bahari ya Ostia dakika chache baadaye ili kuendelea na utume wake. Kituo kinachofuata watasimama: Corsica.
