Tafuta

2025.10.27 Kabla ya Maazimisho ya Misa kwa wanafunzi wa vyo vikuu vya Kipapa, Papa alitia saini 2025.10.27 Kabla ya Maazimisho ya Misa kwa wanafunzi wa vyo vikuu vya Kipapa, Papa alitia saini  (@VATICAN MEDIA)

Papa atia saini Barua ya Kitume:“Kuchora ramani mpya za matumaini"

Jumatatu Oktoba 27 Papa Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Vyuo vikuu vya Kipapa na kabla ya misa hiyo alitia saini Barua ya Kitume baada ya miaka 60 ya Tamko la Mtaguso II la "Gravissimum educationis."Wakati wa mahubiri Papa alisisitiza kuwa Kanisa linahitaji mtazamo wa pamoja na kuhimiza Vyuo vikuu kulisha njaa ya ukweli na maana na bila hiyo mtu anaweza hata kufa.Utafiti unawawezesha kuwa na mtazamo mpya na wa jumla.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Chini ya mtazamo wa Bikira Maria, Kikao cha Hekima, Picha iliyokuwa karibu na Madhabahu ya Ungamo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Leo XIV, kabla ya Misa ya  wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Kipapa jioni ya  Jumatatu tarehe 27 Oktoba 2025, alitia saini barua ya Kitume yenye kichwa: "Kuchora Ramani Mpya za Matumaini," miaka 60 baada ya Tamko la Mtaguso  wa Pili wa Vatican la : Gravissimum educationis  la Mtakatifu Paulo VI.  Lakini Hati hiyo itachapishwa rasmi, siku ya  Jumanne tarehe 28 Oktoba 2025,  katika kumbukumbu ya Hati hiyo ya Mtaguso wa Pili wa Vatican. Karibu na Papa Leo XIV  wakati wa tukio hilo, kulikuwa na Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu. Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya saini, hiyo alikwenda kujiandaa tayari kwa maadhimisho ya misa ambayo ilikuwa inafungua Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu.

Kutia saini Hati ya Kipapa kuhusu Elimu
Kutia saini Hati ya Kipapa kuhusu Elimu   (@VATICAN MEDIA)

Katika mahubiri yake, Papa alianza kusema kuwa "Kukusanyika mahali hapa wakati wa Mwaka wa Jubilei ni zawadi ambayo hatupaswi kuichukulia kirahisi. Zaidi ya yote, ni zawadi kwa sababu kwenda hija, kupitia Mlango Mtakatifu, kunatukumbusha kwamba maisha yana maana tu wakati yanapoishi kama safari, wakati yanajua jinsi ya kuendelea mbele, yaani, wakati yanapoweza kufanya uwepo wa uhalisia wa Pasaka. Basi, ni vizuri kufikiria jinsi Kanisa, kupitia kusherehekea Jubilei katika miezi hii, limekuwa likikumbuka kwamba linahitaji kupitia uongofu kila mara na kwamba lazima litembee nyuma ya Yesu kila wakati bila kusita na bila kishawishi cha kusonga mbele yake. Kiukweli, daima linahitaji Pasaka, yaani, "kuvuka" kutoka utumwa hadi uhuru, kutoka kifo hadi uzima. Nnatumaini kwamba nyote mnapata ndani yenu zawadi ya tumaini hili, na kwamba Jubilei inaweza kuwa fursa ambayo maisha yenu yanaweza kuanza upya, " alisisitiza Papa Leo.

Misa kwa wana vyuo vikuu vya kipapa
Misa kwa wana vyuo vikuu vya kipapa   (@VATICAN MEDIA)

Baba Mtakatifu aidha aliendeleza kusema kuwa "Leo, ningependa kuwahubiri ninyi ambao ni sehemu ya taasisi za vyuo vikuu na wale wote ambao, kwa njia mbalimbali, hujitolea kusoma, kufundisha na kufanya utafiti. Ni neema gani inayoweza kugusa maisha ya mwanafunzi, mtafiti, na msomi? Ningejibu hivi: ni neema ya maono makuu, mtazamo unaoweza kufahamu upeo wa macho, wa kutazama zaidi ya hapo. Tunaweza kuona ufahamu huu katika kifungu cha Injili kilichosomwa hivi punde (Lk 13:10-17), ambacho kinaonesha picha ya mwanamke kibiongo, mara mbili na, aliponywa na Yesu, hatimaye anaweza kupokea neema ya mtazamo mpya, na maono mapana zaidi. Hali ya mwanamke huyu inafanana na hali ya ujinga, ambayo mara nyingi huhusishwa na kujifungia ndani na kukosa utulivu wa kiroho na kiakili. Ana kibiongo mara mbili, anajisalimisha, na hivyo hawezi kutazama zaidi ya hapo. Wakati wanadamu hawawezi kuona zaidi ya hapo, zaidi ya uzoefu wao wenyewe, mawazo na imani zao, zaidi ya mipango yao wenyewe, basi hubaki wafungwa, watumwa na hawawezi kuunda hukumu za kukomaa.

Mwanzo wa Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu
Mwanzo wa Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea kusema kuwa, kama mwanamke mwenye kibiongo wa Injili, hatari huwa ni ile ya kubaki wafungwa wa mtazamo wetu wa ubinafsi. Hata hivyo, kiukweli, mambo mengi muhimu maishani - tunaweza kusema, mambo ya msingi zaidi - hayatoki kwetu; tunayapokea kutoka kwa wengine. Yanakuja kwetu kupitia walimu wetu, matukio na uzoefu wa maisha. Huu ni uzoefu wa neema, kwani hutuponya kutokana na kujifyonza. Huu ni uponyaji wa kweli ambao, kama vile kwa mwanamke katika Injili, huturuhusu tena kusimama kidete mbele ya maisha na uhalisia wake, na kuyaangalia kwa mtazamo mpana zaidi.

Mwanzo wa Jubiliei ya Ulimwengu wa Elimu
Mwanzo wa Jubiliei ya Ulimwengu wa Elimu   (@Vatican Media)

Mwanamke aliyeponywa alipokea tumaini, kwani hatimaye anaweza kuinua macho yake na kuona kitu tofauti, anaweza kuona kwa njia mpya. Hasa hii hutokea tunapokutana na Kristo maishani mwetu, tunapojifungulia ukweli unaobadilisha maisha unaoweza kutufanya tujitokeze na kutuweka huru kutokana na kujifyonza kwetu. Wale wanaosoma "wanainuliwa," wakipanua upeo na mitazamo yao ili kupata maono ambayo hayaangalii chini, lakini yenye uwezo wa kutazama juu: kuelekea Mungu, wengine na fumbo la maisha. Hakika, Papa alisisitiza neema ya kuwa mwanafunzi, mtafiti au msomi inamaanisha kukubali maono mapana ambayo yanaweza kuona mbali; ambayo hayarahisishi matatizo wala kuogopa maswali; ambayo hushinda uvivu wa kiakili na, kwa kufanya hivyo, pia hushinda uozo wa kiroho.

Mwanzo wa Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu
Mwanzo wa Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu   (@Vatican Media)

Tukumbuke kila wakati kwamba mambo ya kiroho yanahitaji mtazamo huu, ambao masomo ya Taalimungu, falsafa na taaluma zingine huchangia kwa njia fulani. Leo,hii tumekuwa wataalamu katika maelezo madogo kabisa ya ukweli, lakini tumepoteza uwezo wa maono makuu yanayounganisha mambo kupitia maana ya kina na kubwa zaidi. Hata hivyo, uzoefu wa Kikristo unataka kutufundisha kutazama maisha na ukweli kwa mtazamo mmoja, wenye uwezo wa kukumbatia kila kitu huku ukikataa njia za kufikiri zisizo kamili.

Misa kwa wanafunzi vya vyuo vikuu vya kipapa
Misa kwa wanafunzi vya vyuo vikuu vya kipapa   (@VATICAN MEDIA)

Kwa hivyo Papa Leo XIV aliwasihi wanafunzi, watafiti na walimu pia, wasisahau kwamba Kanisa linahitaji mtazamo huu mmoja kwa leo na kesho. Tunaweza kutazama mfano wa wanaume na wanawake kama vile Agostino, Thomas Aquinas, Teresa wa Avila, Edith Stein na wengine wengi ambao walijua jinsi ya kuunganisha utafiti katika maisha yao na safari yao ya kiroho. Sisi pia tumeitwa kusonga mbele katika juhudi zetu za kiakili na utafutaji wa ukweli bila kutenganisha na maisha. Ni muhimu kukuza umoja huu ili kinachotokea katika madarasa ya vyuo vikuu na mazingira ya kielimu ya kila aina kisibaki kuwa zoezi la kiakili la kufikirika. Badala yake, inakuwa na uwezo wa kubadilisha maisha, na kutusaidia kuimarisha uhusiano wetu na Kristo, kuelewa vyema fumbo la Kanisa, na kutufanya mashuhuda jasiri wa Injili katika jamii.

Mwanzo wa Jubilie ya Elimu
Mwanzo wa Jubilie ya Elimu   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisisitiza  tena kwamba masomo, utafiti na ufundishaji huleta jukumu muhimu la kielimu, na alipenda kuhimiza vyuo vikuu kukubali wito huu kwa shauku na kujitolea. Kuelimisha ni sawa na muujiza uliosimuliwa katika Injili iliyosomwa, kwani shughuli ya mwalimu ni kuwainua watu, kuwasaidia kuwa wao wenyewe na kuweza kukuza dhamiri zilizoelimika na uwezo wa kufikiri kwa kina. Vyuo vikuu vya Kipapa lazima viweze kuendelea na "shughuli" hii ya Yesu. Hili ni tendo la kweli la upendo, kwani ni aina ya upendo unaooneshwa kupitia masomo, maarifa na utafutaji wa dhati wa kile kilicho kweli na kinachostahili kuishi. Kulisha njaa ya ukweli na maana ni kazi muhimu, kwani bila hivyo tungeanguka katika utupu na hata kufa.

Katika safari hii, kila mmoja wetu anaweza pia kugundua upya zawadi kubwa zaidi, ambayo ni kujua kwamba hatuko peke yetu na kwamba sisi ni wa mtu fulani, kama Mtume Paulo anavyothibitisha: “Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ndiyo watoto wa Mungu. Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa inayowafanya muogope tena, bali mlipokea roho ya kufanywa wana. Tunapolia, ‘Aba! Baba!’…” (Rm 8:14-17).

Baada ya Misa
Baada ya Misa   (@Vatican Media)

Kiukweli, kile tunachopokea tunapotafuta ukweli na kujitolea kujifunza kinatusaidia kugundua kwamba sisi si viumbe vilivyotupwa kwa bahati duniani, bali kwamba sisi ni wa mtu anayetupenda na ambaye ana mpango wa upendo kwa maisha yetu. Papa Leo aliendelea kuwaeleza wasomi hao kuwa, pamoja nao anamwomba Bwana kwamba uzoefu wa masomo na utafiti wakati wa miaka yao ya chuo kikuu uweze kuwapatia uwezo wa mtazamo huu mpya. “Safari yenu ya kitaaluma iwasaidieni kujua jinsi ya kuzungumza, kusimulia, kuzidisha na kutangaza sababu za tumaini lililo ndani yetu (taz. 1 Pet 3:15). Chuo Kikuu na kiwafunde kuwa wanaume na wanawake ambao hawajielekezi wenyewe kamwe,  bali daima ni wanyofu, wenye uwezo wa kupeleka furaha na faraja ya Injili popote wanapokwenda. Bikira Maria, Kikao cha Hekima, awasindikize  na kuwaombea.”

Hitimisho la misa kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vya kipapa
Hitimisho la misa kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vya kipapa   (@Vatican Media)
Papa kwa vyuo vikuu vya kipapa

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: 

Just click here

27 Oktoba 2025, 20:05