Papa atia saini Waraka wa Kitume 'Dilexi Te',utawasilishwa Oktoba 9
Siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Francis wa Assisi,Papa Leo XIV ametia saini Hati yenye kichwa:"Nimekupenda,"Itakayowasilishwa kwa waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Vyombo vya habari,Vatican tarehe 9 Oktoba 2025,saa 5.30,masaa ya Ulaya.
Vatican News
Katika siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Francis wa Assisi, Jumamosi tarehe 4 Oktoba 2025, saa 2.30 asubuhi masaa ya Ulaya, katika Maktaba ya faragha ya Jumba la Kitume, Vatican, Baba Mtakatifu Leo XIV alitia saini, Waraka wake wa Kwanza wa Kitume, wenye jina: “Dilexi te,” yaani, “Nimekupenda,” kwa uwepo wa Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Vatica n kwa ajili ya Mambo ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican.
Hati hiyo itawakilishwa tarehe 9 Oktoba 2025, saa 5.30 majira ya Ulaya katika Ukumbi wa Vyombo vya Habari vya Vatican.
Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here
04 Oktoba 2025, 10:53
