Papa:Kutembea pamoja ni mtindo wa maisha na utume wa Kanisa
Vatican News
Siku za mafunzo na ziongeze ufahamu upya kwamba kutembea pamoja ni mtindo wa maisha na utume wa Kanisa. Haya ndiyo matashi mema ambayo Papa Leo XIV anawapatia waendelezaji, wazungumzaji na washiriki wa Kongamano la Kitaalimungu lenye mada: "Ni Askofu wa aina gani katika Kanisa la Kisinodi?" linalofanyika kwenye Makao makuu ya Watawa wa Monasteri ya Camaldoli nchini Italia, kuanzia tarehe 6 hadi 9 Oktoba 2025
Ni Siku nne zilizotengwa kwa ajili ya kujifunza hasa sura na huduma ya Askofu katika Kanisa la kisinodi, kwa kutaka kufafanua jinsi mtindo wa sinodi na aina ya Kanisa hauwezi kuendelezwa bila kufikiria upya huduma ya kiaskofu kutoka katika mtazamo wa sinodi na kutembea pamoja.
Ujumbe wa Papa
Katika ujumbe huo, uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican na kuelekezwa kwa Dom Matteo Ferrari, Mkuu wa Shirika la Wa Camaldolesi, ambalo ni Shirika la Mkatifu Bedikito, Papa anaonesha uwepo wake wa “kiroho” kwenye mkusanyiko huo “muhimu.”.Mpango wa "kina wa kitaalimungu na kikanisa," ambapo Papa anaonesha shukrani zake. Matumaini yake ni kwamba siku hizi zitahamsisha mwamko mpya wa "kutembea pamoja," akikumbusha kwamba: "Sinodi halisi, kwa asili yake, inahitaji usikilizaji na ushiriki wa wabatizwa wote, kulingana na wito wa kila mtu, lakini haiwezi kupuuza mamlaka iliyotolewa na Kristo kwa Baraza la Maaskofu kwa kuongozwa na Mrithi wa Petro."
Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui
