Tafuta

Papa:Mwaka huu tuchague tutakayemtumikia:haki au dhuluma au pesa

Ulimwengu unabadilika ikiwa sisi tunabadilika na lazima kujua kuchagua ikiwa tunamtumikia Mungu,haki au dhuluma au pesa.Haya yamo katika tafakari ya Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Katekesi ya Jubilie,tarehe 4 Oktoba 2025,kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro:Papa alijikita na mada yaMtakatifu Clara wa Asisi alikuwa jasiri asiyekuwa wa kawaida.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa tafakari yake kwa waamini 30 elfu waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 4 Oktoba 2025, kwa ajili ya kumsikiliza Katekesi ya Jubilei. Kabla ya Katekesi hiyo kama kawaida, Papa alifanya mzunguko na kigari chake katikati ya wanahija hasa katika muktadha wa Jubilei ya Wahamiaji na Wamisionari, akisimamai kubariki watoto. Akigusia juu ya Jubilei, alisisitiza jinsi ambavyo Jubilei inavyo fungua matumaini ya mgawanyo tofauti wa mali, kwa uwezekano kwamba ardhi ni ya kila mtu, kwa sababu kiukweli hii sivyo." Sura ya Mtakatifu Maskini wa Assisi ilikuwa mada ya Katekesi: “Kutumaini ni kuchagua: Clara wa Assisi", hasa katika Siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Francis wa Assisi, Msimamizi wa Italia.

Katekesi ya Papa Leo 4 Oktoba
Katekesi ya Papa Leo 4 Oktoba   (@Vatican Media)

Somo la Injili: "Yesu aliwaambia wanafunzi wake: "Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu, au atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na fedha." Mafarisayo, ambao walikuwa wapenda fedha, waliposikia haya yote, wakamdhihaki.”

Mahujaji wa Matumaini
Mahujaji wa Matumaini   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo mara baada ya kusomwa kifungu cha Injili hiyo kwa lugha mbali mbali, alianza kusema: “Katika maandishi ya kibiblia yaliyosomwa (Lk 16,13-14), Mwinjili anaona baadhi ya watu baada ya kumsikiliza Yesu walimdhihaki. Mazungumzo yake juu ya umaskini yalionekana kuwa ya kipuuzi kwao. Kwa usahihi zaidi, walihisi kuguswa hadi msingi kwa kushikamana kwao na pesa. Papa aliendelea kwamba wao wamekuwa kama mahujaji wa matumaini, na Jubilei ni wakati wa matumaini thabiti, ambayo mioyo yetu inaweza kupata msamaha na huruma, ili kila kitu kianze upya. Jubilei pia inafungua njia ya matumaini ya mgawanyo tofauti wa mali, kwa uwezekano kwamba dunia ni ya kila mtu, kwa sababu kiukweli, hii sivyo. Mwaka huu lazima tuchague tutakayemtumikia: haki au dhuluma, Mungu au pesa.

Umati wa waamini na mahujaji
Umati wa waamini na mahujaji   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo alisema kuwa “Kutumaini ni kuchagua. Hii ina maana angalau mambo mawili. Jambo lililo wazi zaidi ni kwamba ulimwengu unabadilika ikiwa tunabadilika. Ndiyo maana ibada ya Hija inafanywa; ni chaguo.”Tunapita kwenye Mlango Mtakatifu ili kuingia enzi mpya. Maana ya pili ni ya kina na ya hila zaidi: kutumaini ni kuchagua, kwa sababu wale ambao hawachagui hukata tamaa. Moja ya matokeo ya kawaida ya huzuni ya kiroho, yaani, mvivu hachagui chochote. Wale wanaoipitia wanashindwa na uvivu wa ndani ambao ni mbaya zaidi kuliko kifo. Kutumaini, hata hivyo, ni kuchagua.

Mahujaji wa Matumaini:Waseminari wa Urbaniania
Mahujaji wa Matumaini:Waseminari wa Urbaniania   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu kwa kuendelea na katekesi yake akielekeza muktadaha wa Mama Kanisa kauadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi,  alisema: “Ninataka kukumbuka leo hii mwanamke ambaye kwa neema ya Mungu, “alitambua kuchagua. Msichana jasiri na asiye wa kawaida: Clara wa Assisi. Ninayo furaha kuzungumza juu yake katika siku muafaka ya Mtakatifu Francis. Kwa kuongeza  Papa alisema kuwa: “Tunajua kwamba Fransis, katika kuchagua umaskini wa kiinjili, alilazimika kuachana na familia yake. Lakini alikuwa mtu: kulikuwa na kashfa, lakini ilikuwa ndogo.

Chaguo la Clara lilikuwa la kuvutia zaidi: msichana ambaye alitaka kuwa kama Francis, ambaye alitaka kuishi, kama mwanamke, huru kama ndugu hao! Clara alielewa kile ambacho Injili inataka. Lakini hata katika jiji linalojiamini kuwa la Kikristo, Injili ikizingatiwa kwa uzito inaweza kuonekana kama mapinduzi. Basi, kama leo hii, lazima tuchague! Clara alichagua, na hiyo inatupatia tumaini kubwa. Hakika, tunaona matokeo mawili ya ujasiri wake katika kufuata hamu yake hiyo: kwanza ni kwamba wasichana wengine wengi katika eneo hilo walipata ujasiri huo na kuchagua umaskini wa Yesu, maisha ya Heri; na  tokio la Pili ni kwamba chaguo hilo halikuwa moto katika nyasi, ikiwa na maana la haraka na kuisha,  lakini la kudumu kwa wakati, hadi kwetu.

Mahujaji wa Matumaini:Waseminari wa Urbaniana na Papa
Mahujaji wa Matumaini:Waseminari wa Urbaniana na Papa   (@Vatican Media)

Chaguo la Clara ilihuisha chaguzi za miito yote ulimwenguni na linaendelea kufanya hivyo leo. Yesu anasema: huwezi kutumikia mabwana wawili. Hivyo, Kanisa ni kijana na linawavutia vijana. Clara wa Assisi anatukumbusha kwamba Injili inawavutia vijana. Bado ni hivyo: vijana wanapenda watu waliowachagua na kubeba matokeo ya uchaguzi wao. Na hii inawafanya wengine watake kuchagua. Ni mwigo mtakatifu: hatuwi "nakala," lakini kila mtu - anapochagua Injili - anachagua mwenyewe. Anajipoteza na kujikuta. Uzoefu unaonesha: hivi ndivyo inavyotokea. Basi tuwaombee vijana; na tuombe kuwa Kanisa lisiwe linalotumikia fedha wala lenyewe, bali Ufalme wa Mungu na haki yake. Kanisa ambalo, kama Mtakatifu Clara wa Assisi, lina ujasiri wa kuishi katika jiji tofauti. Hii inatoa matumaini!” Papa alihitimisha Katekesi yake.

Salamu kwa wanahija kutoka mataifa mbali mbali

Papa Leo kadhalika alitoa salamu mbali mbali kwa mahujaji. “Ninawakaribisha asubuhi ya leo mahujaji na wageni wote wanaozungumza Kiingereza wanaoshiriki katika Katekesi ya leo, hasa wale wanaotoka Afrika Kusini, Korea Kusini na Marekani. Salamu maalum kwenu nyote mnaoshiriki katika Jubilei ya Kimisionari na Wahamiaji. Katika kusali ili mpate kuongezeka kwa fadhila ya matumaini katika Mwaka huu wa Jubilei, ninawaombea ninyi nyote, na familia zenu zote, furaha na amani ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu awabariki nyote!”

Vijana wa shule Poland: Kuiga mfano wa Clara wa Assisi

Papa aliendelea kwa wanaozungumza lugha nyingine: “Nawasalimu Wapoland wote, hasa vijana wanaosoma shule na vyuo vikuu kuchukua majukumu mbalimbali katika jamii na katika jamii mbalimbali. Mfano wa Watakatifu Fransisko na Clara uwaimarishe katika kufanya maamuzi ya kijasiri katika maisha, ili mpate kutamani na kudai zaidi kutoka kwenu, na kuwa ishara ya matumaini kwa wengine, hasa wenzenu. Ninawabariki kwa moyo wote!”

Kuvuka Mlano kwa kuchagua maisha ya Injili

“Nawasalimu waamini wanaozungumza Kireno, hasa kutoka Ureno na Brazili, waliokusanyika hapa kwa ajili ya hija ya Jubilei. Ninawaomba mvuke kizingiti cha Mlango Mtakatifu, mkichagua maisha ambayo Yesu anatupatia katika Injili: maisha ya umaskini, haki, huruma, amani na furaha. Mungu awabariki!

Kuwa mashuhuda wa udugu na upendo wa kiinjili

Ninawakaribisha sana waamini wanaozungumza Kiitaliano, hasa wa Jimbo la Piacenza-Bobbio, wakisindikizwa na Askofu Adriano Cevolotto. Ndugu wapendwa, ninatumaini kwamba, mkiimarishwa na neema ya Jubilei, mpate kuwa mashahidi wa udugu na upendo wa Kiinjili katika jumuiya zenu. Kisha ninawasalimu parokia za Francavilla al Mare, Mtakatifu Felice wa Cancello, na Sarno, na Shirikisho la Italia la waendesha Pikipiki.

Vijana, wazee na wanandoa wapya

Hatimaye, Papa alisema “ mawazo yangu yanageukia vijana, wagonjwa, na wenye ndoa wapya. Leo tunaadhimisha siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Kwa ninyi vijana, awe kielelezo cha maisha ya Kiinjili; kwenu ninyi wagonjwa, kielelezo cha upendo kwa Msalaba wa Kristo; kwa ajili yenu, enyi waliooa hivi karibuni, ninawaalika daima kuwa na imani katika Maongozi ya Mungu. Baraka yangu kwa wote!”

Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here

04 Oktoba 2025, 11:41