Tafuta

2025.10.25 Papa aliadhimisha Miza kwa Mihimili ya Kikatiba nchini Italia. 2025.10.25 Papa aliadhimisha Miza kwa Mihimili ya Kikatiba nchini Italia.   (@VATICAN MEDIA)

Papa kwa Jubilei ya mihimili ya kikatiba,Italia:serikali hubadilishwa kuwa bora kama mtu anahisi kuwajibika

Katika Misa Oktoba 25 iliyoongozwa katika Ukumbi wa Baraka wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Jubiliei ya vyombo vya kikatiba vya Italia,Papa Leo XIV alisisitiza:Serikali inajengwa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kutunza manufaa ya wote na akaelezea matumaini kwamba maisha ya kiongozi wa dola,Polisi na hakimu yatahimiza uongofu ambao Yesu Kristo anatualika.Alitoa mifano ya sura muhimu za kitaasisi nchini Italia:De Gasperi na D’Acquisto na Livatino.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa Jumamosi iliyopita, tarehe 25 Oktoba 2025, katika Ukumbi wa Baraka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wakati wa Jubilei ya Mihili ya Katiba ya Italia. Katika mahubiri yake, Papa aliwasisitiza kwamba "katika hali ya kurudiarudia kwa maovu," Mwenyezi Mungu "yuko tayari kila wakati kutupatia wokovu na kutukomboa kutoka katika maovu, tukitaka hivyo, kwamba mwelekeo mpya ambao Mungu anatuelekeza ni safari inayotoka tulipo hadi milele.

Mwanzo mwa mahubiri yake alisema kwamba “Mwanzoni mwa Misa Takatifu, tulirejesha salamu nzuri zaidi tunayoweza kupeana: amani iwe nanyi! Amani hii ni zawadi ya Bwana Mfufuka na hamu ya kila moyo mnyoofu. Leo, wakati wa Jubilei yenu, kwa hivyo ninawaalika mfungue mioyo yenu kwa neema ya Mungu. Mmekusanyika hapa, kwenye Kaburi la Mtakatifu Petro, kama mahujaji wa matumaini: jina hili halioneshi matarajio moja kati ya mengine mengi, bali ni fadhila inayotoa nguvu na maana kwa matarajio yetu yote ya mema.”

Papa aliadhimisha misa kwa wanajubilei ywa kitaasisi Italia
Papa aliadhimisha misa kwa wanajubilei ywa kitaasisi Italia   (@VATICAN MEDIA)

Papa aliendelea kwamba “Tumaini la kweli hufungua mlango Mtakatifu wa wokovu, ambao kupitia huo tunachukua hatua za imani, tukiishi miongoni mwa kila mmoja katika upendo wa kidugu. Kwa hivyo, mwanga huu wa roho unaonesha njia hata wakati ulimwengu, pamoja na rasilimali zake zote, hauwezi kufanya hivyo. Injili tuliyosikia inatualika kukuza tumaini kwa lugha ambayo inaweza kusikika kuwa kali: "Msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo" (Lk 13:3, 5). Yesu anatamka onyo hili mara mbili, akichota msukumo kutoka vipindi vya vurugu na bahati mbaya.”

Baadhi ya Wagalilaya waliuawa kwa amri ya gavana wa Kirumi, huku wengine wakifa katika kuanguka kwa mnara. Cha kusikitisha, matukio kama hayo yanaendelea kutokea katika historia ya mwanadamu. Hata hivyo, tukikabiliwa na huzuni  kwa  kurudia maovu, Bwana anaelekeza kwenye upya wa maisha, akitualika kufanya tofauti: "Tubuni!" Kiukweli, Mungu yuko tayari kila wakati kutupatia wokovu na kutukomboa kutoka katika maovu, ikiwa tunataka. Ikiwa, yaani, tunaendana na uhuru wetu kwa maongozi yake: huu ndio uongofu ambao Kristo anauomba.

Misa ya Jubilei ya Kitaasisi
Misa ya Jubilei ya Kitaasisi   (@Vatican Media)

Neno la Kigiriki metanoia linaelezea hili vizuri, likimaanisha mabadiliko ya mawazo, mabadiliko ya njia ya kuishi, kufikiri, na kutenda. Mwelekeo mpya ambao Bwana anatuita tuuchukue ni safari kutoka tulipo, sasa, hadi kwa Mungu, umilele. Hivi ndivyo wema wa tumaini unavyofanya kazi: unatushangaza kwa undani na ahadi ya kuishi huru kutoka kwa barabara hiyo ya njia moja, ambayo inaongoza kwenye kifo bila ukombozi. Papa alindelea kusisistiza kuwa uongofu ambao Yesu anazungumzia ni juhudi ya kweli ya kila siku, inayojikita katika  shughuli zetu zote. Ahadi hii inafunua maana tunayoipa maisha na mwelekeo ambao mioyo yetu inaelekezwa.

Tukikabiliana na mateso na majaribu ya historia, Injili inatukumbusha kwamba kuishi bila tumaini kunamaanisha kubaki bila kusonga mbele katika uhakika wa kifo, huku tukibadilisha maisha yetu kuwa tumaini ambalo Kristo anatupatia inamaanisha kubeba nuru ya Mfufuka mioyoni mwetu. Mabadiliko haya yanatuhusisha sote: yanatumika kwa kila dhamiri, kwa Kanisa lote, kwa kila raia, na kwa hivyo pia kwa Serikali. Ndiyo: ikiwa Serikali haitabadilika kutoka kwa dhuluma zinazoitishia na ufisadi unaoiharibu, ina hatari ya kutoweka. Kwa busara sana, Katiba ya Italia ilileta maisha mapya kwa nchi kwa kutangaza kwamba "Jamhuri imejengwa juu ya kazi"(Kifungu cha 1).

Jubilei ya kitaasisi Nchini Italia
Jubilei ya kitaasisi Nchini Italia   (@VATICAN MEDIA)

Ni kwa kufanya kazi kwa uaminifu kwamba Serikali hujengwa, ikijali manufaa ya wote. Katika uwanja huu, mnaitwa kutoa ushuhuda mzuri: kiukweli, sherehe, haijiadhimishi yenyewe, bali hutumikia taasisi na, kwa hivyo, raia wanaowawakilisha. Hasa kama walinzi wa utaratibu huu, mnajitolea kwa manufaa ya watu, mkitoa utaalamu wenu ili mashirika ya umma yaeleze uhusiano mzuri na yaweze kufanya kazi kwa ubora wao. Katika enzi hii, iliyojaa mivutano mikubwa, lakini ambayo haijawahi kuachwa na huruma ya Mungu, ninawakabidhi mifano mitatu inayong'aa ya matumaini na haki, ya unyenyekevu na kujitolea kwa Serikali: kumbukumbu ya maisha na vifo vyao ituchochee kwenye uongofu walioupata wenyewe.

Shuhuda kwanza ni Mtumishi wa Mungu Alcide De Gasperi, ambaye mchakato wake wa kutangazwa mwenyeheri unaendelea. Akichanganya imani yake na uwajibikaji unaokuwa wa kisiasa, kiongozi huyu wa serikali alikuwa miongoni mwa baba waanzilishi wa Jamhuri ya Italia. Katika miaka yote iliyojaa vita viwili vya dunia, alifanya kazi kujenga madaraja yaliyopinga mikondo ya itikadi zinazopingana. Upendo wake kwa Mungu, kiukweli, uliendeleza kujitolea kwake kwa nchi yake, ukitufundisha kwamba siasa, diplomasia, na ulinzi wa taifa huwa vyombo vya upendo wa kweli vinapoishi kwa roho ya unyenyekevu.

Taasisi ya Kikatiba Italia waadhimisha Jubilei yao
Taasisi ya Kikatiba Italia waadhimisha Jubilei yao   (@VATICAN MEDIA)

Shuhuda wa pili wa kuiga ni Mtumishi wa Mungu Salvo D'Acquisto, ambaye pia yuko karibu na kutangazwa kuwa mwenyeheri. Sadaka yake ni ya thamani zaidi kuliko nishani ya dhahabu ya ushujaa wa kijeshi inayoheshimu kumbukumbu yake: kwa kutoa maisha yake kwa ajili ya raia wenzake, alitimiza kikamilifu utume wake kama Polisi. Katika wakati wa vita na chuki, ujasiri wake ukawa unabii wa amani iliyojengwa juu ya kujitolea kwa ukarimu zaidi: ni watu kama yeye wanaoangazia matatizo ambayo bado yanawalemea watu wengi leo hii.

Shuhuda wa  tatu ninayemkabidhi ni Mwenye Heri Rosario Livatino, hakimu wa kwanza katika historia kutambuliwa kama shahidi. Kwa kujitolea kwake bila kuyumba kwa haki, alionesha kwamba uhalali sio seti ya sheria, bali ni njia ya maisha, na kwa hivyo njia inayowezekana ya utakatifu. "Sub tutela Dei," yaani “chini ya Ulinzi wa Mungu” aliandika juu ya maelezo yake: sisi pia tunajiweka chini ya ulinzi wa Mungu kwa ujasiri, tukifanya kazi kila siku kama watumishi wa ukweli na wafumaji wa umoja.

Jubilei ya kikatiba ya Italia
Jubilei ya kikatiba ya Italia   (@Vatican Media)

Kiukweli, Serikali hubadilishwa kuwa bora zaidi ikiwa kila mtu anahisi kuwajibika kwa hilo, ikilisha hisia zao za kiraia na wajibu wa kitaasisi kwa maadili ya juu zaidi ya kiroho. Tunakushukuru kwa ushirikiano tunaoweza kufikia katika kazi hii, hebu tuendelee pamoja katika safari hii, tukimsifu Bwana kwa uhakika wa lengo analoandaa kwa ajili ya wote.

Papa aadhimisha misa ya Mihimili ya Kikatiba Italia

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: Just click here

27 Oktoba 2025, 14:40