Tafuta

Papa Leo XIV kwa Kikosi cha Ulinzi cha Uswiss:Huduma kwa Kristo katika kuwajali wanaohitaji

Papa Leo XIV akishiriki katika sherehe za kuapishwa kwa kikosi kipya cha Ulinzi wa Kipapa cha Uswiss,alisisitiza kuelewa umuhimu wa nidhamu na kujisadaka.Ni katika hafla iliyofanyika jioni,Oktoba 4 katika Uwanja wa Mtakatifu Damas wa Jumba la Kitume.Papa alisifu thamani ya ushuhuda wao katika Ulimwengu wa leo hii,njia ya kuishi imani inayozungumza na vijana wote kuhusu thamani ya kujisadaka,kutumikia na kufikiria wengine.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Uwanja wa Mtakatifu  Damas unaozunguka Jumba la Kitume  Vatican ulipambwa kwa sherehe kwa bendera za kila Mkoa wa Uswiss katika fursa ya kuapishwa kwa Askari wapya 27 wa Walinzi wa Uswiss. Ilikuwa tukio maalum jioni ya tarehe 4 Oktoba 2025 kwa sababu ya ushiriki wa  Baba Mtakatifu leo XIV, tukio ambalo halikuwahi kutokea tangu wakati wa Upapa wa Papa Paulo VI.

Hafla ya kiapo cha walinzi wa Kiswiss
Hafla ya kiapo cha walinzi wa Kiswiss   (@Vatican Media)

Rais wa Uswiss, pamoja na Mapadre na maafisa wa kiraia na kijeshi, na familia, marafiki, wafadhili, na walinzi wa zamani, wote walikuwepo wakati ambao ni muhimu sana katika kazi ya Walinzi wa Uswiss, wanaodhamana ya kumlinda Baba Mtakatifu.

Hafla ya kiapo cha walinzi wa Kiswiss
Hafla ya kiapo cha walinzi wa Kiswiss   (@Vatican Media)

Kwa mujibu wa Padre wa Kiroho wa Walinzi wa Uswiss wakati wa kufafanua tukio hilo alisema “Tunajivunia ninyi na tunashukuru kwamba mmeitikia mwito wa utumishi huu wenye heshima, ambao sasa mnaapa kutekeleza kwa uangalifu na kwa uaminifu.”

Wakati wa kiapo
Wakati wa kiapo   (@Vatican Media)
Kikoso cha Kiswiss
Kikoso cha Kiswiss   (@Vatican Media)

Kiapo kwa lugha yao

Nyimbo za Vatican na Uswiss zilipigwa. Mmoja baada ya mwingine, walioitwa na sajenti, wale wahitimu walikaribia bendera ya Kikosi. Katika tukio la kuapa, walikuwa wakifika mbele na kushika Bendera huku wakisema: “Naapa kumtumikia kwa uaminifu, na kwa heshima Papa Mkuu Leo XIV na warithi wake halali, na kujitolea kwao kwa nguvu zangu zote, hata kutoa maisha yangu ikibidi kwa ajili ya utetezi wao. Pia ninachukua majukumu haya kwa Baraza la  Makardinali wakati wa Kiti kilicho wazi. Zaidi ya hayo, ninaahidi heshima, uaminifu, na utii kwa Kamanda na wakuu wangu wengine. Naapa. Basi Mwenyezi Mungu na walinzi wetu watakatifu nisaidie mimi.”

Mkuu wa Kikosi cha Kiswiss walinzi wa kipapa
Mkuu wa Kikosi cha Kiswiss walinzi wa kipapa   (@Vatican Media)

Sherehe hiyo ilichukua zaidi ya saa moja na kuhitimishwa kwa tamasha fupi lililofanywa na bendi ya Walinzi wa Uswiss. Kisha ilitiwa muhuri kwa maneno ya shukrani kutoka kwa Papa, ambaye alionesha shukrani zake “zaidi ya yote, kwa Mungu kwa zawadi ya uhai na imani.” Baba Mtakatifu kwa kuliita tukio hilo zuri, aliwasalimu waliohudhuria: makardinali, maaskofu wakuu, maaskofu, rais wa Shirikisho la Uswiss, na familia za Walinzi wa Uswiss ambao walikula kiapo hicho kwa njia ya pekee sana.”

Kikosi cha Ulinzi cha Kiswiss
Kikosi cha Ulinzi cha Kiswiss   (@Vatican Media)
Kikos cha Uswiss
Kikos cha Uswiss   (@Vatican Media)

Papa alisema : “Kwa ninyi nyote mliofanya kiapo hiki: ni shuhuda muhimu sana katika ulimwengu wa leo. Mnatuonesha thamani ya nidhamu, sadaka ya kuishi imani kwa njia ambayo inazungumza kiukweli na vijana, juu ya thamani ya kutoa uhai wa mtu, kuwatumikia, na kufikiria wengine. Niwakushukuru kwa niaba yangu na kwa niaba ya Kiti kitakatifu kwa huduma yenu."

Wakati wa kula kiapo
Wakati wa kula kiapo   (@VATICAN MEDIA)
Wakati wa kula kiapo
Wakati wa kula kiapo   (@Vatican Media)
Kiapo cha Wanajeshi wa Kiswiss

Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here

05 Oktoba 2025, 10:20