Papa kwa Vikosi vya Ulinzi Vatican:huduma inayofanyika nyuma ya pazia ni muhimu sana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa maashimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya Kikosi cha Maaskari wa Mji wa Vatican, ikiwa ni fursa ya kuadhsimisha Siku kuu ya Mtakatifu Mlizi na msimamizi wao Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, iliyofanyika Dominika jioni tarehe 6 Oktoba 2025 mbele ya Groto ya Lourdes katika Bustani za Vatican, alisisiztiza juu ya, majukumu ya viongozi wa Vatican kuwa si taaluma tu, bali ni huduma kwa manufaa ya Kanisa, kwa sababu kazi yao ya kila siku inatoa ushuhuda wa Injili.
Baba Mtakatifu Leo XIV akianza mahubiri, alisema kuwa kwa mujibu wa mapokeo mazuri, amekuwa na fursa ya kusherehekea Ekaristi pamoja nao kwenye siku kuu ya mlinzi wao Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu. Wamekusanya kwenye madhabahu ya Bwana, chini ya macho ya Mama ya Bikira Safi. “Ombi letu la kwanza kabisa ni la kusikiliza Neno la Mungu, ambalo linatupatia ujumbe wenye nguvu na wazi siku hizi. Hakika, Mtume Paulo anatuhimiza hivi: “Usione haya kumshuhudia Bwana wetu” (2 Tim 1:8).”
Papa aliendelea kusema kuwa “ Ni ushuhuda wa Yesu unaotoa maana kwa kile tunachofanya: vinginevyo tuna hatari ya kuwa Wakristo wavuvi wa uvuguvugu, na wasio na moyo wa bidii kwa ajili ya Injili. Kwa kukumbuka tukio la kiapo kilichopita, “ ka vikosi vya ulinzi vya Vatican, si taaluma tu: ni huduma kwa manufaa ya Kanisa. Hakika, kazi yenu ya kila siku pia inatoa ushuhuda kwa Injili.” Kwa njia hiyo “kamwe msione aibu kwa mfano mnaoweza kuweka. Mara nyingi na mnajua hili kutokana na uzoefu—uwepo wenu wa busara na ujasiri mnaweza kueleza mtindo wa kiinjili, si kwa maneno, lakini hata kwa kutazama kwa uangalifu, kwa ishara ya kujali ambayo inalinda kila mtu karibu nayi,” Papa alieleza. Papa alisema “Ili kupinga jaribu la tabia na uvivu, Mtakatifu Paulo mwenyewe anatuhimiza kuwa : "Nawakumbusha kufufua zawadi ya Mungu iliyo ndani yenu [...]. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na kiasi"( 2 Tim 1: 6-7 ).” Kwa hakika hizi ni fadhila za Mkristo mwema, na kwa hivyo pia vikosi vya Ulinzi vya Vatina: mna nguvu kutoka kwa sheria, lakini sio kutawala; mna upendo kwa watu wa hali ya chini, lakini si kutaka kuwapendeza wenye mamlaka; busara katika utendaji, lakini si kwa kuogopa majukumu yako mwenyewe.”
Huu ndio mpango ambapo Papa Leo XIV alipenda kuwakabidhi hasa hao vijana wa kiume ambao walikula kiapo siku moja kabla ya Dominika(4 Oktoba 2025.) Papa alisema kuwa ahadi hiyo haikuwa kiapo rahisi kurudiwa, bali kitendo cha uhuru na kujitolea. Walithibitisha hadharani “ndiyo,” mbele ya Mungu na Kanisa. Waliahidi uaminifu kwa Papa na kwa huduma inayohusisha maisha yao, katika kujitolea kwa kazi yao ya kila siku. Papa aliwashukuru kwa ujasiri na utayari walioonesha katika kutumikia Kiti Kitakatifu! Ili kudumu katika kuchagua mema na haki, ambayo inatimiza wajibu wako kama sheria, na tujifanyie ombi tulilosikia katika Injili, wakati mitume wanamwomba Yesu: "Tuongezee imani!" (Luka 17:5 ). Naam, Bwana: kaa upande wetu, uongoze mioyo yetu, utufanye mashahidi wa Neno lako! Imani yetu, yaani, uhusiano wetu na Wewe, ukue daima, katikati ya furaha na majaribu ya maisha. Ni Wewe Mwenyewe, Bwana, unayeilisha kwa neema ya Roho wako Mtakatifu, ili izae matunda ndani yetu kwa njia ya matendo mema.
Papa alisema “Hebu basi tuseme maneno haya kwa matumaini ya wale wanaojua kuwa wanapendwa na Mungu, na kwa hiyo wanatamani kuishi kulingana na mapenzi yake. Wakati siku za taabu na kutokuelewana zinakuja, tutapata katika neema ya Bwana faraja na uaminifu unaotutegemeza. “Wapendwa, huduma yenu hufanyika kimsingi "nyuma ya pazia." Haionekani mara chache, lakini inafanya kazi sana. Ni kazi inayojenga usalama, utaratibu, na heshima: ifanyeni pamoja, kama timu, kwa kuelewana na wale ambao wamefanya kazi huko kwa muda mrefu zaidi. Ni huduma inayolinda sio tu maeneo na watu, bali inaakisi utume, utume wa Kanisa. Kwa hiyo, muishi utume huu huu, ambao ni utangazaji wa Injili, kwa sare yenu na, zaidi ya yote, kwa ubinadamu wenu.
Shukrani za Papa pia ziliwandea familia zao : wake zao watoto wao, baba zao na mama zao. "Ndiyo" yao pia inaungwa mkono na "ndiyo" yao ya kimya. Bila wao, huduma yao itakuwa dhaifu zaidi. Bwana awabariki, awalinde, na awajaze amani. Bikira Maria awe kielelezo cha imani na kujitolea kwao na Mtakatifu Mikaeli, Malaika Mkuu anayepiga vita maovu kwa jina la Mungu, awalinde wao na familia zao daima. “Kwa moyo wa unyenyekevu na uaminifu mtaweza kuwa mashahidi wa amani katika Nchi ndogo sana, ambayo ina upeo wa Ulimwengu.”
Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here
