Tafuta

Barua ya Papa Leo XIV ya Mto Proprio: Barua ya Papa Leo XIV ya Mto Proprio: 

Papa Leo XIV aandika Barua ya motu proprio mpya kuhusu uwekezaji wa Kiti Kitakatifu

Katika Barua mpya ya Kitume ya motu proprio iliyotolewa,Papa Leo XIV anatoa mwongozo mpyakuhusu shughuli za uwekezaji wa kifedha wa Kiti Kitakatifu.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa Waraka mpya wa Kitume wa "motu proprio" Jumatatu tarehe 6 Oktoba 2025 kuthibitisha mapendekezo maalum yaliyoidhinishwa na Baraza la Uchumi kuhusu shughuli za uwekezaji wa kifedha wa Kiti Kitakatifu. Motu proprio mpya, yenye kichwa: "Coniuncta cura", inaakisi kanuni ya "wajibu wa ushirikiano katika jumuiya" kama inavyohitaji ujumuishaji wa masharti mbalimbali ambayo yamejitokeza baada ya muda, pamoja na ufafanuzi wa wazi wa "majukumu na mienendo ya taasisi mbalimbali za Kiti kitakatifu, "kuwezesha kila mtu kuungana katika ushirikiano wa pamoja."

Imetolewa baada ya tathmini ya kina ya mapendekezo ya Baraza na mashauriano na wataalamu, ambapo Barua mpya ya Kitume inafuta maandishi ya awali "kuhusu usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kifedha na taslimu za Kiti Kitakatifu na za taasisi zinazohusiana na Kiti kitakatifu,"iliyoandikwa tarehe 23 Agosti 2022(rej.dated August 23, 2022.) Hati iliyofutwa ilibainisha kwamba “Taasisi ya Kazi za Dini (IOR) ambayo wakati mwingine hujulikana kama (Benki ya Vatican) ilikuwa na uwezo wa kipekee juu ya usimamizi wa mali na ilikuwa msimamizi wa mali zote zinazohamishika za Kiti Kitakatifu na taasisi zinazohusiana nayo. Kwa hiyo iliweka bayana kwamba taasisi zote za Kiti Kitakatifu ambazo zinamiliki mali za kifedha na taasisi za fedha isipokuwa IOR, na lazima zihamishie kwenye Benki ya Vatican haraka iwezekanavyo.”

Katika Barua mpya ya kitume ya motu Proprio ijulikanayo "Coniuncta cura"  inabainisha kwamba "shughuli za uwekezaji wa kifedha za Kiti Kitakatifu, ambazo zimejitolea kwa matumizi yake yenyewe na kutekelezwa kwa mujibu wa kifungu 219 cha Katiba ya Kitume ya Praedicate Evangelium, lazima ifuate masharti yaliyoanzishwa na Kamati ya Uwekezaji, kwa kuzingatia Sera ya Uwekezaji iliyoidhinishwa." Pia inabainisha kwamba shughuli za uwekezaji wa kifedha za Kiti Kitakatifu kwa ujumla zinafanywa na Utawala wa Urithi wa Mali za Kiti Kitakatifu  (APSA) kupitia Taasisi ya Kazi za Dini,(IOR), "isipokuwa mashirika yenye uwezo, kama ilivyoanzishwa na sheria za Kamati ya Uwekezaji, inaona kuwa inafaa zaidi au inafaa kutumia usuluhishi wa kifedha ulioanzishwa katika nchi zingine."

Katika Barua mpya ya Kitume ya Motu proprio itaanza kutumika Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025, siku ya kutangazwa kwake rasmi kwa kuchapishwa katika gazeti la Osservatore Romano.

Papa na Motu Proprio

Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kusasishwa zaidi, jiandikishe katika makala za kila siku kwa kubonyeza hapa: Just click here

06 Oktoba 2025, 18:08