Tafuta

Picha katika siku ya hafla ya kuapishwa kwa Mfalme Guillaume wa Luxembourg. Picha katika siku ya hafla ya kuapishwa kwa Mfalme Guillaume wa Luxembourg.  (ANSA)

Papa Leo XIV atuma salamu kwa Mfalme wa Luxembourg

"Ili kukuza,maisha yaliyojengwa juu ya kuheshimu maadili ya Kikristo ambayo yameunda utambulisho wa Luxembourg na hivyo kukuza utaftaji bila kuchoka wa faida ya wote.Kushiriki furaha kunaambatana na matakwa ya dhati ya amani kwa mustakabali wa nchi.”Ndiyo Matashi mema yaliyomo kwenye telegramu ya Papa aliyomtumia Mrithi wa Ufalme wa Luxembourg wakati wa kutawazwa kwake.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV, alituma salamu zake za matashi mema kutoka moyoni kupitia telegram kwa Mfalme  Guillaume wa Luxembourg kwenye hafla ya sherehe kwa heshima ya kutawazwa kwake kwenye kiti cha kifalme huko Luxembourg.

Kukuza heshima kwa maadili ya Kikristo na manufaa ya wote

Papa aliandika kwamba, "katika fursa ya maadhimisho ya Heshima ya Kutawazwa Mfalme katika Kiti  kikuu cha Luxembourg, nimefurahi kutoa salamu zangu za dhati kabisa. Kwa hivyo ninajiunga na shangwe ya nchi nzima yenye tamaduni  ya kale na ya kifahari, iliyokita mizizi katika historia.” Papa Leo XIV aidha alibainisha kwamba, “Ukuu  wa Kifalme, kwa upande wake, uchangie katika kukuza maisha yanayotokana na kuheshimu maadili ya Kikristo ambayo yameunda utambulisho wa Luxembourg na hivyo kukuza ufufutaji usiochoka wa manufaa ya wote.”

“Katika siku hii ya furaha, - Papa aliongeza “ninatoa kwa Mtukufu usemi wa kujali kwangu kwa moyo mkunjufu, ukiambatana na matashi  yangu ya dhati ya amani kwa mustakabali wa nchi yako.” Kwa kuhitimisha Papa anaadika, “Nikiwaombeeni ulinzi wa mbinguni wa Mama wa Mungu, ninawapa Baraka yangu ya Kitume, ambayo kwa hiari yangu ninawapa wakazi wote wa Ufalme wa Luxembourg.”

Kardinali Hollerich ataongoza Misa katika Kanisa Kuu,Dominika Oktoba 5

Guillaume wa Luxembourg, mwenye umri wa miaka 43, anamrithi babake, Henri, kama mkuu wa Grand Duchy, ambaye alijiuzulu baada ya miaka 25 ya utawala. Atavishwa taji na kula kiapo cha Katiba mbele ya manaibu 60 wa Baraza la Manaibu. Sherehe hiyo itahudhuriwa na wawakilishi wa kifalme wa Uholanzi na Ubelgiji. Mwishoni mwa Juma hili,  Kiongozi Mkuu atafanya ziara yake ya kiutamadubi  nchini, ambayo itahitimishwa kwa Ibada ya Dominika  itakaoadhimishwa na Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Luxembourg, katika Kanisa Kuu la Katoliki la Notre-Dame de Luxembourg.

Luxembourg, nchi yenye wakazi 700,000, ni demokrasia ya bunge huku Grand Duke akiwa mkuu wa nchi. Guillaume atakuwa Grand Duke wa saba tangu 1890, mwaka ambao ufalme wa kisasa ulianzishwa katika kile ambacho kwa sasa ni duchy kuu ya mwisho ulimwenguni.

Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here

03 Oktoba 2025, 14:30