Tafuta

Papa Leo XIV,Jubilei ya Waliowekwa wakfu:kuimarisha na kutakasa imani,kukuza ukarimu na uhuru katika upendo

Katika mahubiri ya Papa Leo XIV katika Misa iliyoadhimishwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa fursa ya Jubilei ya Maisha ya Wakfu,alisisitiza mambo matatu kutoka katika Injili ya Luka:"kuomba,kutafuta na kubisha.Watu waliowekwa wakfu ni ishara ya kinabii ya huruma kwa sababu nadhiri zao za Kiinjili ni kujiacha kama watoto mikononi mwa Baba.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV ameongoza Ibada ya Misa Takatifu Alhamisi asubuhi tarehe 9 Oktoba 2025 kwa makumi ya maelfu ya washiriki katika Jubilei ya Maisha ya Wakfu, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro chini ya jua kali la  mwezi Oktoba. Hawa walikuwa ni Wanaume na wanawake watawa wa asili tofauti, tabaka za kijamii, lugha, na rangi, wanaojishughulisha na nyanja mbalimbali za utume, lakini pia wakiunganishwa na kusudi moja la  kumfuata Kristo katika njia ya Ushauri wa Kiinjili, wanakusanyika siku hizi jijini Roma kutoka nchi mia moja kwa ajili ya muungano katika Mwaka Mtakatifu wa Jubilei 2025.

Misa ya Jubilie ya Watawa
Misa ya Jubilie ya Watawa   (@Vatican Media)

Na Adhimisho la Ekaristi Takatifu pamoja na Baba Mtakatifu linawakilisha kilele cha mpango mzima ulioendelezwa na Jimbo Kuu la Roma na Baraza la Kipapa la  Maisha ya Wakfu na Vyama vya  Kitume (DIVCSVA), pamoja na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji linalohusika na uandaaji wa  Jubilei ya Matumaini.  Hawa, kila mmoja akiwa na historia yake ya kibinafsi baada ya kuvuka Milango Takatifu na kupokea sakramenti ya upatanisho wa kimsingi, walijikuta leo hii wakisikiliza kwa ukimya mahubiri ya Papa Leo XIV, tangu mtu aliyewekwa wakfu, kama wao katika Shirika la  Mtakatifu Agostino mnamo 29 Agosti 1981.

Jubilie ya Watawa
Jubilie ya Watawa   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo alianza kusema “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, na mlango utafunguliwa” (Lk 11:9). Kwa maneno haya, Yesu anatualika kumgeukia Baba kwa ajili ya mahitaji yetu yote.  Haya pia ni maneno tunayosikiliza wanapokusanyika kutoka sehemu zote za dunia kuadhimisha Jubilei ya Maisha ya Kuwekwa wakfu. Kama wanaume na wanawake watawa, watawa wa ndani, washiriki wa taasisi za kilimwengu na Ordo virginum, Wakaa pweke,  na wale wa "taasisi mpya," kwa ujumla wote wamefika Roma kufanya Hija ya Jubile ya pamoja.

Jubilei ya Watawa
Jubilei ya Watawa   (@Vatican Media)

Papa alisema kuwa wamefika kuyakabidhi maisha yao  kwa huruma  ile ile ambayo, kwa njia ya nadhiri zao za kitawa walijitolea mara moja kutoa ushuhuda, kwa sababu kuishi kulingana na nadhiri zao  “kunamaanisha kujitoa wenyewe kama watoto mikononi mwa Baba.” Kwa njia hiyo "Kuomba," "kutafuta" na "kubisha." Maneno haya ya maombi, yaliyotajwa na mwinjili Luka, ni mitazamo ambayo wanaifahamu, Papa alisema: “Kupitia kuishi mashauri ya kiinjili wamezoea kuomba bila kudai, daima kuwa wanyenyekevu kwa tendo la Mungu.”  Si kwa bahati kwamba Mtaguso wa Pili wa Vatican unazungumza juu ya nadhiri kama njia muhimu ya "kupata matunda mengi zaidi kutoka kwa neema ya ubatizo" (Lumen Gentium, 44).

Jubilei ya Watawa
Jubilei ya Watawa   (@Vatican Media)

Kuomba, kiukweli, ni kutambua, kupitia umaskini, kwamba kila kitu ni zawadi kutoka kwa Bwana na kutoa shukrani kwa ajili yake.“Kutafuta” ni kujifungua mwenyewe, kwa njia ya utii, ili kugundua kila siku njia tunayopaswa kuchukua katika safari ya kuelekea utakatifu, kufuata mipango ya Mungu.  “Kubisha” ni kuomba na kutoa zawadi ambazo tumepokea kwa kaka  na dada zetu kwa moyo safi, tukijitahidi kupenda kila mtu kwa heshima na ukarimu. Tunaweza kusoma maneno ambayo Mungu alimwambia nabii Malaki katika somo la kwanza katika nuru ileile. Anawataja wakaaji wa Yerusalemu kuwa “mali yangu ya pekee” (Mal 3:17) na anamwambia nabii hivi: “Nitawahurumia kama vile wazazi wanavyowahurumia watoto wao.”  Maneno haya yanatukumbusha upendo ambao Bwana alitupenda kwanza kwa kutuita. Ni fursa, hasa kwao, kutafakari juu ya zawadi ya bure ya wito wao kutoka asili ya shirika la kila mmoja wao, hadi leo na kutoka hatua za kwanza za safari yao ya kibinafsi hadi sasa.

Jubiliei ya Watawa
Jubiliei ya Watawa   (@Vatican Media)

Papa akianza kudadavua alisema “Kwanza kabisa, sote tuko hapa kwa sababu Mungu amependa, na ametuchagua tangu mwanzo kabisa. “Kuomba,” “kutafuta,” na “kubisha” pia kunamaanisha kutafakari maisha yetu wenyewe, tukileta akilini na moyoni kile ambacho Bwana amefanikisha kwa miaka mingi kwa kuzidisha talanta, kuimarisha na kutakasa imani, na kukuza ukarimu na uhuru katika upendo. Wakati mwingine hii imefikiwa katika hali ya furaha, na wakati mwingine kwa njia ambazo ni ngumu zaidi kuelewa, labda hata kupitia msalaba wa ajabu wa mateso. Wakati wote, hata hivyo, tunajikuta katika kukumbatia wema huo wa kibaba unaoonesha kile anachofanya ndani yetu na kupitia kwetu, kwa manufaa ya Kanisa (taz. Lumen Gentium, 43).

Jubilie ya Watawa
Jubilie ya Watawa   (@Vatican Media)

Hii inatuleta kwenye tafakari ya pili: Mungu kama utimilifu na maana ya maisha yetu. “Kwao na  kwetu,  Bwana ndiye kila kitu. Yeye ni kila kitu kwa njia tofauti: kama Muumba na chanzo cha kuwepo, kama upendo unaoita na changamoto, kama nguvu inayotusukuma na kututia moyo kutoa. Bila yeye, hakuna kitu kilichopo, hakuna kitu cha maana, hakuna kitu cha thamani,” Papa alisisitiza. “Kuomba,” “kutafuta,” na “kubisha” kwao, katika sala na maishani, kunahusiana sana na ukweli huu. Katika suala hili, Mtakatifu Agostino anaelezea uwepo wa Mungu katika maisha yake mwenyewe kwa kutumia taswira nzuri. Anazungumza juu ya nuru isiyofungwa na anga, sauti isiyofifia, chakula kisichopungua kwa kula, na njaa ambayo haishibiki, na anahitimisha: "Hiki ndicho ninachopenda ninapompenda Mungu wangu" (Mtakatifu Agostin, Maungamo, 10.6.8).

Papa Leo XIV alisema kuwa haya ni maneno ya mtu wa ajabu, lakini yanahusiana na uzoefu wetu wenyewe. Yanafunua hamu ya kutokuwa na mwisho ambayo hukaa ndani ya mioyo ya wanaume na wanawake wote. Kwa sababu hii, Kanisa linawakabidhi jukumu la kuwa mashahidi hai wa ukuu wa Mungu katika maisha yenu. Kwa kujinyima kila kitu, wanasaidia kaka na dada wanaokutana nao kusitawisha urafiki huu wenyewe. Baada ya yote, historia inatufundisha kwamba uzoefu halisi wa Mungu daima huleta umiminiko wa ukarimu wa upendo.  Hivi ndivyo ilivyokuwa katika maisha ya waanzilishi wao, wanaume na wanawake ambao walikuwa katika upendo na Bwana na kwa hiyo tayari kuwa "vitu vyote kwa watu wote" (1 Kor 9:22), bila ubaguzi, katika njia na hali tofauti zaidi.

Jubilie ya watawa
Jubilie ya watawa   (@Vatican Media)

Ni kweli kwamba leo, kama ilivyokuwa katika siku za Malaki, wengine husema, “Ni bure kumtumikia Mungu” ( Malaki 3:14 ). Njia hii ya kufikiri husababisha kupooza kweli kwa nafsi. Tunaishia kuridhika na maisha yanayojumuisha matukio ya muda mfupi, mahusiano ya juu juu na ya vipindi, na mitindo ya kupita kiasi - mambo ambayo yanaacha pengo mioyoni mwetu. Hili silo tunalohitaji ili kuwa na furaha ya kweli.  Badala yake, tunahitaji uzoefu thabiti, wa kudumu na wenye afya wa upendo. Kupitia mfano wa maisha yao ya kuwekwa wakfu, wanaweza kufananishwa na miti inayositawi iliyoimbwa juu  yake katika kiitikio cha zaburi(rej. Zab 1:3), ikieneza “hewa safi” ya upendo wa kweli ulimwenguni kote.

Papa alisema anavyopenda  kuzingatia kipengele kimoja cha mwisho cha utume wao: Tulimsikia Bwana akiwaambia wakaaji wa Yerusalemu, “Jua la haki litazuka, lenye kuponya katika mbawa zake,” (Mal 4:2) akiwaalika kutumaini utimizo wa hatima yao zaidi ya wakati uliopo.”  Hii ni rejea kwa mwelekeo wa eskatolojia wa maisha ya Kikristo, ambayo inatualika tujishughulishe na ulimwengu, wakati huo huo tukijitahidi daima kuelekea umilele. Ni mwaliko kwao kurefusha "kuomba," "kutafuta," na "kubisha" kwa maisha yao kupitia maombi hadi upeo wa milele unaovuka uhalisi wa ulimwengu huu.  Kuwaelekeza Dominika hiyo bila machweo wakati “wanadamu wote wataingia katika... pumziko la Mungu,(Misale ya Roma, Dibaji ya Dominika katika Kipindi cha Kawaida X).

Jubilie ya watawa kike na kiume
Jubilie ya watawa kike na kiume   (@Vatican Media)

Katika suala hili, Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vaticam unawakabidhi kazi mahususi unaposema kwamba watu waliowekwa wakfu wanaitwa kwa namna ya pekee kutoa ushuhuda wa “mali zijazo” (taz. Lumen Gentium, 44). Kwa njia hiyo, Papa kwa kuhitimisha aliwaeleza  kaka na dada, kwamba  Bwana, ambaye wamewapatia  kila kitu, kwamba  amekutuza kwa uzuri na utajiri kama huu, na alipenda Papa kuwahimiza kutunza na kukuza kile walichopokea.  Kadhalika Papa alipenda  tukumbuke maneno ya Mtakatifu Paulo VI ambaye aliwaandikia watawa: “Shika, usahili wa ‘walio wadogo zaidi’ wa Injili. Naomba mfanikiwe kugundua jambo hili upya katika uhusiano wa ndani na wa karibu zaidi na Kristo na katika mawasiliano yenu ya moja kwa moja na ndugu zenu. Kisha mtapata uzoefu kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu shangwe ya furaha ya wale wanaoingizwa katika siri za ufalme.  Msitafute kuhesabiwa miongoni mwa ‘waliosoma na wajanja’... Siri hizo zimefichwa kwa hawa. Muwe maskini kweli kweli, wapole, wenye shauku ya utakatifu, wenye huruma na wasafi wa moyo. Muwe miongoni mwa wale watakaoleta duniani amani ya Mungu” (Mtakatifu  Paulo VI, Wosia wa Kitume wa  Evangelica Testificatio, 29 Juni 1971, 54).

Asante sana kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho, tunakualika kujiandikisha hapa ili kupata habari za kila siku: cliccando qui

 

09 Oktoba 2025, 14:51