Papa,Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu:Undani,umoja,upendo na furaha!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mambo ya ndani, umoja, upendo, na furaha yalikuwa ni mambo muhimu ambayo Baba Mtakatifu Leo XIV aliyojikita nayo akisisitiza kwamba ni mambo muhimu na dhamira ya waelimishaji katika shule na Vyuo vikuu. Hivi ni vipengele vya mafundisho ya Mtakatifu Agostino ambavyo Papa aliona kuwa msingi wa elimu ya Kikristo. "Ningependa viwe msingi wa safari tunayoweza kufanya pamoja," alisema, akikumbuka uzoefu wake kama mwalimu katika taasisi za elimu za Shirika la Mtakatifu Agostino kwa walimu na maprofesa 15,000 "kutoka ulimwenguni kote na kushiriki katika kila ngazi" waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 31 Oktoba 2025 kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Elimu.
Kabla ya Hotuba yake Papa awali ya yote alizunguka kwenye kigari jeupe katika uwanja mzima ili kuwasalimia mahujaji. Akitumaini kwamba mkutano huo, unaweza kuwa mwanzo wa safari ya pamoja ya ukuaji na utajiri wa pande zote, Baba Mtakatifu Leo XIV alionya kuhusu hatari ya kuharibu jukumu la kijamii na kiutamaduni la waelimishaji, ambalo lingekuwa kuweka rehani mustakabali wao wenyewe, na akaonya kuhusu hatari za Akili Unde, ambayo inaweza kuwatenga zaidi wanafunzi ambao tayari wametengwa. Katika hotuba yake, alisisitiza, kwanza kabisa, kwamba ni shukrani kwa kundi kubwa la karama, mbinu, ufundishaji, na uzoefu na kujitolea kwa sauti nyingi' katika Kanisa, katika majimbo, taasisi za kitawa, vyama na harakati kwamba waelimishaji wanawahakikishia mamilioni ya vijana elimu ya kutosha, wakiweka wema wa mtu katikati ya uenezaji wa maarifa ya kibinadamu na kisayansi.
Kisha alizingatia kila moja ya mambo muhimu yaliyooneshwa kwa walimu, na kuhusu mambo ya ndani, akinukuu, ili kurudia kwamba ni moyoni ndipo Mungu anaposema, kile ambacho Askofu wa Hippo alisema katika Maoni yake kuhusu Barua ya Mtakatifu Yohane: “Sauti ya maneno yetu hugusa masikio, lakini mwalimu wa kweli yuko ndani.” Ni kosa kufikiri kwamba maneno mazuri au madarasa mazuri, maabara, na maktaba yanatosha kufundisha. Hizi ni njia na nafasi za kimwili tu, hakika ni muhimu, lakini Mwalimu yuko ndani. Ukweli hauzunguki kupitia sauti, kuta, na korido, bali katika kukutana kwa kina na watu, ambao bila hiyo pendekezo lolote la kielimu litashindwa. Tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa na skrini na mara nyingi vichujio vya kiteknolojia vya juu juu, ambapo wanafunzi wanahitaji msaada wa kuungana na nafsi zao za ndani. Na si wao tu. Kwa waelimishaji, ambao, mara nyingi wamechoka na kulemewa na kazi za urasimu, wanahatarisha kusahau kwamba moyo huzungumza na moyo, kama Mtakatifu John Henry Newman alivyorudia mara nyingi kusema, Papa alikumbusha mwaliko wa Mtakatifu Agostino wa "kutoangalia nje," kurudi ndani yako mwenyewe, kwa sababu "ukweli uko ndani" yako mwenyewe.
Papa Leo aliwaalika kutazama elimu kama njia ambayo walimu na wanafunzi hutembea pamoja, kwa ufahamu wa kutotafuta bure lakini, wakati huo huo, kulazimika kutafuta tena baada ya kupata." Kwa sababu ni juhudi hii ya unyenyekevu na ya pamoja tu, inayochukuliwa kama “Mpango wa kielimu katika mazingira ya shule, inaweza kuwaleta wanafunzi na walimu karibu na ukweli." Kuhusu umoja, Papa Leo alirudi kwenye kauli mbiu yake, ya 'Illo uno unum,' usemi wa Mtakatifu Agostino uliochukuliwa kutoka kwa Ufafanuzi wa Zaburi 127:3, "ambao unatukumbusha kwamba ni katika Kristo pekee ndipo tunapata umoja wa kweli, kama washiriki walioungana na Kichwa na kama wasafiri wenza katika safari ya kujifunza endelevu maishani." Ni kipimo cha 'pamoja,' kinachopatikana kila wakati katika maandishi ya Baba wa Kanisa, ambacho Papa alikiona kuwa cha msingi katika mazingira ya kielimu, kama changamoto ya 'kugawanya' na kama kichocheo cha ukuaji." Hivyo ni uamuzi "wa kufufua na kusasisha mpango wa Papa Francisko wa Mkataba wa Kielimu wa Kimataifa.
Kuhusu upendo, Papa alikumbuka "Mstari wa Mtakatifu Agostino tena kwamba 'Kumpenda Mungu ndiyo amri ya kwanza, kumpenda jirani ndiyo ya kwanza ambayo lazima itekelezwe, ili kila mtu aweze kutafakari jinsi ya kushiriki na kushughulikia mahitaji ya dharura zaidi, kujenga madaraja ya mazungumzo na amani, hata ndani ya jamii za kufundisha, kushinda dhana za awali au maono machache, kuwa wazi katika michakato ya kujifunza pamoja, na kwenda kukidhi na kujibu mahitaji ya walio hatarini zaidi, maskini, na waliotengwa." Kushiriki maarifa hakutoshi kufundisha bali upendo unahitajika. Hapo ndipo utakapowanufaisha tu wale wanaoupokea, maarifa yenyewe na zaidi ya yote kwa ajili ya upendo unaoutoa. Kufundisha hakuwezi kamwe kutenganishwa na upendo, na ugumu wa sasa katika jamii zetu ni kwamba hatuthamini tena mchango mkubwa ambao walimu na waelimishaji hutoa kwa jamii.
Papa ametoa onyo kuwa lakini tuwe waangalifu kwani: kuharibu jukumu la kijamii na kitamaduni la waelimishaji kunaweka rehani mustakabali wetu wenyewe, na mgogoro katika uenezaji wa maarifa huleta mgogoro wa matumaini. Papa Leo alibainisha kwamba, walimu wanahimizwa kuelimisha kwa "tabasamu" na "kuamsha tabasamu katika kina cha roho za wanafunzi wao." Papa alitazama ukweli wa kisasa na mazingira ya kielimu ya sasa na, akiwa na wasiwasi kuhusu ukuaji wa dalili za udhaifu wa ndani ulioenea, katika rika zote alihimiza kwamba zisifumbiwe macho kwa vilio hivi vya kimya kimya vya kuomba msaada na kujitahidi kutambua sababu zake kuu.
Na kuhusu Akili Unde (AI) Papa alitoa onyo kwamba “kwa maarifa yake baridi na sanifu ya kiufundi, inaweza kuwatenga zaidi wanafunzi waliotengwa tayari, ikiwapa udanganyifu wa kutowahitaji wengine au, mbaya zaidi, hisia ya kutostahili. Hii ndiyo sababu Baba Mtakatkfu alisisitiza umuhimu wa kazi ambayo walimu wameitwa na ametumia kifungu cha maneno kutoka kwa Mtakatifu Agostino kuakisi pendekezo la mwisho la furaha. Hata hivyo, jukumu la waelimishaji alisema ni kujitolea kwa mwanadamu, na furaha yenyewe ya mchakato wa elimu ni ya kibinadamu kabisa, ambao ni mwali unaounganisha roho pamoja kutengeneza mingi.
