Tafuta

2025.10.02 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mabiti wa Mtakatifu Paulo. 2025.10.02 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mabiti wa Mtakatifu Paulo.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Mabinti wa Mtakatifu Paulo:Tukiongozwa na Roho,tukisikilize ubinadamu wa leo

“Kutangaza na kueneza Neno,kutumia maisha yenu kwa ajili ya Injili katika nyayo za Yesu Mwalimu na kutafuta njia,zana na lugha ili kila mtu aweze kumjua na kumfuata Bwana, ndiyo moyo wa utume wenu."Ni katika maneno ya Papa Leo XIV kwa Washiriki wa Mkutano Mkuu wa XII wa Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Paulo,aliokutana nao,Oktoba 2,mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuishi kwa upyaisho na ari kwa kutazama juu na kufikiria kuwa ndani, ndiyo msisitizo wa Baba Mtakati Leo XIV, Alhamis tarehe 2 Oktoba 2025, akikutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa XII wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo. Awali ya wote aliwakaribisha na kuwatakia heri kwa kumpata Mama Mkuu mpya alichaguliwa , na kwamba tusali kwa ajili yake. Alionesha furaha ya kushirikishana nao wakati huu katika fursa ya mkutano huo. Na wakati huo kumsalimu  Mkuu mpya kama ilivyo hata shukrani kwa yule aliyemaliza muda wake na kuwakaribisha kila mmoja wao. Papa alieleza wanavyotoka katika mabara yote matano, na hii inadhihirisha umoja wa Kanisa. Utume wao, ulioenea katika nchi nyingi ulimwenguni, na ushuhuda wanaotoa katika mazingira tofauti zaidi pia unathibitisha kile ambacho Roho Mtakatifu ametimiza, kuanzia na ufahamu wa kinabii wa mwanzilishi wao, Mwenyeheri James Alberion, uliotekelezwa bila woga na mwanzilishi mwenza, Mtumishi wa Mungu  Thecla Merlo.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@VATICAN MEDIA)
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@Vatican Media)

Kutangaza na kueneza Neno, kutumia maisha yao kwa ajili ya Injili katika nyayo za Yesu Mwalimu na kutafuta njia, zana na lugha ili kila mtu aweze kumjua na kumfuata Bwana: huu ndio moyo wa utume wao. Wanakabiliwa na changamoto za wakati wetu, wanahitaji kujipyaisha na kutiwa nguvu tena, ili shauku ya kiinjili inayowatia moyo waweze kupata usemi wake bora zaidi. Papa alisema hii “Si kwa bahati kwamba mada waliyochagua ya Mkutano Mkuu wao  ni "Tukiongozwa na Roho, tukisikilize ubinadamu wa leo, tunawasilisha Injili ya matumaini." Hakika, Papa alisisitza kuwa “wakati wa utangazaji wa Injili unabakia kuwa kiini cha utume, na ni kweli vile vile kwamba si suala la kuwasilisha habari za jumla au ukweli wa kufikirika, bali ni kuingia katika historia halisi, ya kukumbatia maombi na mahangaiko yaliyoibuliwa na maisha halisi, ya kuzungumza lugha za wanawake na wanaume wa wakati wetu.”

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@Vatican Media)

Ishi kwa upyaisho na ari:kutazana juu na kufikiria kuwa ndani

Papa Leo XIV alipenda kuwahimiza kuishi kwa upyaisho wa ari ya kitume kwa tabia mbili muhimu: kutazama juu na kujifikiria kuwa ndani. Akidadavua  alisema kuwa: “Kutazama juu, ili kuweza kuongozwa na Roho Mtakatifu." Wito wao na utume wao unatoka kwa Bwana, tusisahau hili,"  Papa alihimiza. Kwa hiyo, kujitolea kwetu binafsi, karama tunazoshiriki, ari yetu ya kitume, na zana tunazotumia kamwe zisituelekeze katika udanganyifu na dhana ya kujitosheleza. Ni Roho ambaye ndiye mhusika mkuu wa utume wetu; ni Roho ambaye hutusukuma mbele, akizidisha talanta zetu, akiturudisha katika kazi zetu, akiichangamsha mioyo yetu wakati furaha ya Injili inapoa, akiangaza hatua zetu na kutupatia utambuzi wa ubunifu, ili tuweze kufungua njia mpya kwa mawasiliano ya imani.”

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa mabinti wa Mtakatifu Paulo
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@Vatican Media)

Kwa upande wa tabia ya pili ambayo Papa aliyowahimiza ni ile ya kujifikiria kuwa ndani ya hali, yaani mtazamo wa kuzama ndani, kwa sababu kutazama juu sio kutoroka, lakini, kinyume chake, kunapaswa kutusaidia kuwa na unyenyekevu sawa na Kristo, ambaye alijivua kwa ajili yetu, akashuka katika mwili wetu, alijishusha ili kuingia katika kina cha wanadamu waliojeruhiwa na kuleta huko upendo wa Baba” (taz. Fl 2:5-11). Papa Leo  alibanisha kwa njia hiyo, kwamba kwa kuongozwa na Roho, wao pia wameitwa kujitumbukiza katika historia, kwa usahihi katika kusikiliza ubinadamu wa leo hii; ni suala la kukaa katika tamaduni za leo hii  na kujifanya mwili katika maisha halisi ya watu wanaokutana nao. Uwepo wao, tangazo la Neno, njia wanazotumia, hasa uchapishaji wanaohamasisha kwa kujitolea kama hivyo, yote haya “lazima yawe tumbo la uzazi la ukarimu kwa mateso na matumaini ya wanawake na wanaume ambao wametumwa kwao.

"Mnatoa huduma kwa Kanisa na ulimwengu,uchapishaji wa kijitali, maduka ya vitabu..."

Papa Leo alisisitiza  kwa kujikita na shuhuli zao za utume wa kimisionari watawa hawa alisema kuwa: “Mnatoa huduma muhimu kwa Kanisa na Ulimwengu, kufanya kazi katika uchapishaji, ulimwengu wa kidijitali, kusimamia maduka ya vitabu, mipango  ya radio na televisheni, na uhuishaji wa Biblia.” Papa aliongeza kueleza  jinsi anavyojua  kwamba “jitihada za kutekeleza shughuli hizi nyingi wakati mwingine ni nzito, hasa kwa sababu hali ngumu za leo hii zinahitaji mafunzo ya kitaaluma ya hali ya juu, ambayo, kwa bahati mbaya, wakati mwingine hupambana  na rasilimali ndogo, za kibinafsi na za nyenzo.” Lakini pamoja na hayo, Papa aliongeza kusema “ wasikate tamaa!” Kwa hivyo, aliwaalika “kutafakari jinsi ya kuweka karama hai, hata kama hii inahitaji uchaguzi wa ujasiri na changamoto.” Kwa hakika, “kuna haja ya utambuzi makini wa kazi zinazohusiana na utume, wa jinsi zinavyotekelezwa, na haja ya kuzifanya upya kwa maono yenye usawaziko, yenye kuunganisha utajiri wa historia ya zamani na rasilimali na karama za sasa za kila mmoja, katika muungano wenye kuzaa matunda kati ya vizazi mbalimbali.”

Papa Leo na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo
Papa Leo na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV alisisitiza tena kwamba “Ushirika unaotokana na mtazamo huu hakika utawasaidia kushinda hatari ya kugawanya maisha na utume. Hakika, Papa alibainisha kwamba wao walizaliwa ili kuwasiliana na Neno, lakini mawasiliano haya, yanayopitishwa katika mazingira ya kichungaji, lazima pia yawe mtindo wa maisha ya jumuiya.  “Ni lazima tuhakikishe kwamba hakuna utengano kati ya kile tunachohubiri na maisha yetu ya kila siku. Ni kwa njia hii tu ndipo mtakuwa waaminifu kwa njia ya uadilifu inayotamaniwa na mwanzilishi wenu kwa Familia nzima ya Paulo: Njia, Kweli, na Uzima, Akili, Mapendo, na Moyo. Na kisha pendekezo hili la kuunganisha, ambalo linaonekana kuwa la kinabii katika ulimwengu uliogawanyika, litakuwa thabiti na la kuaminika."

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mabinti wa Mtakatifu Paulo   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo alipenda kuwakumbusha juu ya faraja waliyopokea kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko miaka michache iliyopita: katika majira haya ya baridi ya kiutamaduni na kikanisa tunayopitia, kwamba "msiogope kujihatarisha na kuendelea na safari "kwa mtazamo wa kutafakari na uliojaa huruma kwa wanaume na wanawake wa wakati wetu, wenye njaa ya Habari Njema ya Injili."(rej. Hotuba kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa XI Oktoba 2019). Kutazama kwa bidii ya Mtakatifu Paulo, kwa furaha yake isiyochoka katika kumtangaza Kristo hata katikati ya shida na mateso (taz. 2Kor 6:4-10). Ancheni muongozwe na  Roho na kuwasikiliza wanadamu. Kwa kila mtu, hasa walio hatarini zaidi, pelekeni tumaini linalotoka juu na, kama Padre Alberone alivyosema, kukuza furaha ya "kupanua kazi ya Mungu kwa wakati na nafasi."  Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alibainisha navyosali kwa ajili yao katika siku kuu ya Malaika Walinzi, akiomba kwa Maombezi ya Maria Malkia wa Mitume na kwa moyo wote amewabariki.

Papa na Mabinti wa Mtakatifu Paulo
02 Oktoba 2025, 10:42