Papa:ajibu maswali:mpango wa Trump kwa Gaza,tumaini kwamba Hamas wanakubali
Na Gabriella Ceraso – Castel Gandolfo.
Baba Mtakatifu Leo XIV alijibu maswali, usiku wa Jumanne tarehe 30 Septemba 2025, kwa waandishi wa habari ambao waliokuwa wakimsubiri katika lango la Villa Barberini, kama ilivyotokea kwa mwezi mzima kila Jumanne jioni. Tunatumaini watakubali; hadi sasa inaonekana kama pendekezo la kweli," alisema Papa Leo XIV, akitoa maoni yake kuhusu mpango wa vipengele ishirini vya amani huko Gaza vilivyowasilishwa kwenye Ikulu ya White House, Marekani kwa kupendekeza Rais wa Marekani Donald Trump kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israel Bwana Benjamin Netanyahu. Ni muhimu kwamba kuna kusitisha mapigano na kutolewa kwa mateka, aliongeza: "Kuna mambo ya kuvutia sana." Na kubainisha kwamba: "Tunatumaini Hamas itakubali ndani ya muda uliokubaliwa."
Kuheshimu watu
Kuhusu Flotilla inayokaribia Gaza kutoa misaada ya kibinadamu, ambayo mvutano unaendelea, Papa alisisitiza hali ngumu sana, akielezea kwamba "kuna nia ya wazi ya kukabiliana na dharura ya kweli ya kibinadamu." Matumaini ya Papa ni kwamba "hakutakuwa na vurugu na kwamba watu wataheshimiwa."
Tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya amani
Kisha linakuja suala la mkutano ulioitishwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth, huku majenerali wote wakiwa tayari kwa vita, wakiwemo tayari kutumia silaha za nyuklia. "Njia hii ya kuzungumza," Papa alitoa maoni, "inatia wasiwasi" kwa sababu inaonesha jinsi mvutano unavyoongezeka. Kuhusu uamuzi wa Rais Trump wa Marekani kubadilisha jina la Idara kutoka "Ulinzi" hadi "Vita," Papa Leo XIV alisema: "Hebu tutumaini kwani ni njia ya kuzungumza tu inayotakiwa." Kwa hakika inaashiria mtindo wa serikali ambao "hutumia nguvu kutekeleza shinikizo. Tuwe na tumaini kwamba itafanya kazi, lakini kwamba hakuna vita; tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya amani."
Hakuna kuingilia Kesi ya Vatican
Alipoulizwa maoni kuhusu kesi inayoendelea ya Vatican kuhusu usimamizi wa fedha za Kiti Kitakatifu, Papa hakufafanua, lakini alieleza kwamba "kesi lazima isonge mbele" na kwamba "hana nia ya kuingilia ." Aliwaachia majaji na mawakili wa utetezi kufikia hitimisho lao.
Kutazama Mafundisho ya Kanisa
Kwa lugha ya Kiingereza, aliulizwa Papa maoni yake juu ya kutunukiwa tuzo kwa Dick Durbin, seneta wa Kidemokrasia anayeunga mkono utoaji mimba, na Kardinali Blaise Cupich, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Chicago. "Sina taarifa za kutosha kuhusu kesi husika. Nadhani," alisema Papa Leo XIV, "ni muhimu sana kutazama kazi ya jumla ambayo seneta amefanya wakati, ikiwa sijakosea, miaka 40 iliyopita ya utumishi wa Seneti ya Marekani." Papa alishikilia kwamba anafahamu matatizo na mivutano, lakini ni "muhimu kutazama masuala mengi yanayohusiana na Mafundisho ya Kanisa."
Kadhali Papa alisema kwamba kusema "mimi ninapinga utoaji mimba" lakini "napendelea hukumu ya kifo" si kweli, kutetea maisha, sawa na "kukubaliana na unyanyasaji wa kinyama wa wahamiaji nchini Marekani" sivyo. "Haya ni masuala magumu sana," Papa alisema. "Sijui ikiwa kuna mtu yeyote ana ukweli wote juu yao, lakini ningeuliza, kwanza kabisa, kwamba kuwe na kuheshimiana zaidi na kwamba tujitahidi pamoja, kama wanadamu , katika hali hii, kama raia wa Marekani au raia wa Mkoa wa Illinois, na kama Wakatoliki, kusema: 'Kiukweli tunahitaji kuangalia kwa karibu maswali haya yote ya kimaadili na kutafuta njia ya mbele kama Kanisa.' Mafundisho ya Kanisa juu ya kila moja ya masuala haya yako wazi sana."
Kurudi Vatican
Hivyo Papa aliondoka Castel Gandolfo kwa gari muda wa saa 2:30 usiku, masaa ya Ulaya ambapo aliwasili jana jioni, Jumatatu, Septemba 29, na ambapo atarejea Mosi Oktoba alasiri baada ya Katekesi, kukutana katika Kituo cha Mariapolis cha Harakati ya Wafocolari pamoja na viongozi wa kidini zaidi ya 400 walioalikwa kwenye tukio la kimataifa: "Kuinua Matumaini kwa Haki ya Hali ya Tabianchi.” Katika kuadhimisha miaka kumi ya waraka wa Papa Francisko Laudato si', Papa Leo ataongoza "Sherehe ya Matumaini" mbele ya wataalam wa hali ya hewa, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, na taasisi kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
