Papa Leo XIV kwa Shirika la Columbus:Shukrani kwa upendo kwa walio wa mwisho
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika hotuba yake Baba Mtakatifu Leo XIV akikutana na Wajumbe wa Bodi ya Kurugenzi ya Shirika la Kijeshi la Columbus Jumatatu tarehe 6 Oktoba 2025 mjini Vatican alionesha furaha ya kukutana nao pamoja na famili zao ambazo zimewasindika katika muktadha wa hija ya Jubilei ya Matumaini. Jinsi gani ilivyo muhimu neno lenyewe matumaini, kama wao wamefika Roma katika Mwaka Mtakatifu ili kutembelea kaburi la Mitume, kuvuka Milango Mitakatifu, na kuimarishwa katika imani yao. Moja ya kazi za sanaa za Vatican ambazo kwa uhakika wakati wa wakuvuka Mlango Mtakatifu na kuingia katika Basilika ni kazi nzuri sana ya Gian Lorenzao Bernini ambayo leo hii inag’aa kwa uzuri wake wote wa asili mara baada ya kukarabatiwa kwa mara ya kwanza kuisha katika historia yake. Eneo nyingine la Basilika, na uzuri wa shaba wa Bernini ambayo inalinda Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ulikarabaitiwa katika kipindi kile kile.
![]()
Papa na Bodi ya Shirika la Kijeshi la Columbus (@Vatican Media)
Kazi hizi nzuri zinasaidia kila mtu kutazama sambamba na nguzo mbli msingi wa imani yetu: Uwepo wa kweli wa Yesu katika Ekaristu na Papa kama Mfuasi wa Petro ambaye anaunganisha na kuongoza Kanisa. Katika muktadha huo, Baba Mtakatifu Leo XIV, amechukua fursa kutoa shukrani kwao, Shirika la Kijeshi la Columbus, kwa ukarimu wao wa kuwezesha mipango hiyo. Hiyo ni ishara ya wazi inayoonekana katika ibada yak ila wakari ya mfuasi wa Kristo. Katika mchakato wa Historia, Shirika liliwezesha kwa namna mbalimbali kazi za upendo wa Papa wa Roma, hata kwa njia ya Mfuko wa ‘Vicarius Christi Fund,’ unaomwezesha kuelezea mshikamano kwa maskini na walio katika mazingira magumu zaidi Ulimwenguni kote.
Baba Mtakatifu kadhalika alieleza kuwa kwa njia ya mipango mingi iliyohamasishwa na Mabaraza mahalia, wao na ndugu zao wa Shirika la kijeshi, wanatafuta zaidi ya hayo kupeleka huruma na upendo wa Bwana katika Jumuiya zao mahalia, hata kwa njia ya jitihada ili kuwezesha maisha matakatifu ya binadamu kwa kila hatua, kusaidia waathirika wa vita na majanga ya asili na kusadia miito ya kikuhani. Kwa njia ya matendo hata na kama jinsi ilivyo sala zao na sadaka zao za kila siku kwa ajili ya wema wa Watu wa Mungu, Baba Mtakatifu ametoa shukrani kubwa ya utambuzi.
![]()
Papa na Shirika la kijeshi (@Vatican Media)
Kwa kuhitimisha amewatakia matunda mema ya hija yao na kusali ili wakati wao wa kuwa katika Mji wa Milele wa Roma waweze kumwilishwa imani, uwathibitishie katika matumaini na kujifunza zaidi upendo wao kwa Kanisa. Wanaweza kwa namna moja kuongeza nguvu ili kuendelea kwa mshangao mkuu wa utume ulionzishwa na Mwanzishilishi wao adhimu. Na katika hisia hizi, aliwakabidhi wote kwa maombezi ya Mama Yetu Maria, Mama wa Kanisa na Mwenyeheri Michael McGivney, na kuwapatia baraka kwa moyo wote kwa kila mmoja wao na familia zao na wapendwa wao.
Asante sana kusoma makala hii, ikiwa unakata kubaki na masasisho zaidi, tunakualika kujiandikisha hapa: Just click here
