Tafuta

2025.10.02 Rappresentanti della "Confederacion Medica Latinoiberoamericana y del Caribe" 2025.10.02 Rappresentanti della "Confederacion Medica Latinoiberoamericana y del Caribe"   (@VATICAN MEDIA)

Papa:uhusiano na mgonjwa ni muhimu na AI haiwezi chukua nafasi ya daktari!

Papa Leo XIV akitana na wanachama wa Shirikisho la Madaktari wa Amerika na Caribbean(CONFEMEL)alibainisha jinsi mazungumzo na uwepo wa kimwili ni msingi katika uhusiano kati ya wale wanaotoa huduma na wanaopokea.Alitoa mfano wa Mwenyeheri José Gregorio Hernández wa Venezuela,daktari wa maskini,atakayetangazwa Mtakatifu Oktoba 19,kama mfano wa kuigwa..

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, alhamisi tarehe 2 Oktoba 2025, alikutana mjini Vatican na Shirikisho la Madaktari wa Kilatini-Ibero-Amerika na Caribbean (CONFEMEL. Katika hotuba yake alianza na   ishara ya Msalaba kama kawaida na kuwakaribisha mjini Vatican kwa furaha.  Papa alisema kuwa Shirikisho lao  linawakilisha zaidi ya madaktari milioni mbili wanaofanya kazi kuleta huduma bora za afya katika kila kona ya nchi zao. Kwa hiyo aliwashukuru kwa kazi hiyo bila kuchoka. Kwa kutazama, Liturujia ya Siku amebainisha kwamba: “Leo tarehe 2 Oktoba, Kanisa linaadhimisha Siku kuu ya Malaika Walinzi Watakatifu. Ukumbusho huu unaweza kutusaidia kutafakari uhusiano wa daktari na mgonjwa, ambao unategemea mawasiliano ya kibinafsi na utunzaji, mtu anaweza kusema kama malaika wanaotulinda na kutulinda katika safari ya maisha.”

Shrikisho la Madaktari bara la Amerika Kusini
Shrikisho la Madaktari bara la Amerika Kusini   (@VATICAN MEDIA)

Mada hii pia Papa aliongeza kuwa,  ilivyomkumbusha maneno ya Mtakatifu Agostino, ambamo alimtaja Kristo kama tabibu na dawa.” “Yeye ni tabibu kwa sababu yeye ni Neno, na dawa kwa sababu yeye ni Neno aliyefanyika mwili(Mahubiri 374, 23). Kwa hakika, Papa Leo aliongeza,  “Neno” na “Mwili” ni mambo ya msingi; mazungumzo, mawasiliano, na mgusano wa kimwili lazima viwepo kila wakati katika uhusiano wa matibabu, zaidi ya zana na vifaa vinavyotumiwa kutibu magonjwa.” Tunaposoma katika Injili, Papa aliongeza “ Yesu aliwaponya wagonjwa kadhaa. Tunaweza kutaja kisa cha mtu mwenye ukoma ambaye, kama Injili ya Mtakatifu Marko inavyotuambia, alipiga magoti “Yesu akamwambia, “ Ukitaka, waweza kunitakasa!” Akamwonea huruma, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka; Takasika!' Mara ule ukoma ukamwacha, na yule mtu akapona” (Mk 1:40-42).

Hii sio ishara ya mitambo; Papa alisisitiza kwamba “uhusiano wa kibinafsi ulianzishwa kati ya mwenye ukoma na Yesu: yule ambaye hangeweza kuguswa alipata afya na wokovu katika kubembelezwa kwa Yesu. Vile vile, kuna madaktari wengi waliojitolea maisha yao kwa ustawi wa wagonjwa wao. Leo  Papa alipenda kumkumbuka Mwenyeheri José Gregorio Hernández, mmoja wa madaktari mashuhuri nchini Venezuela mwanzoni mwa karne ya 20.” Huyo ni Mwenyeheri atakayetangazwa tarehe 19 Oktoba kuwa Mtakatifu, kwa njia hiyo Papa alisisitiza kuwa anamwona: “ kuwa mfano mzuri kwao, kwa vile aliunganisha ujuzi wake wa juu wa matibabu na kujitolea kwake kwa wale walio na mahitaji zaidi, ambayo ilimpatia kuitwa jina la "daktari wa maskini."

Shirikisho la Madaktari wa Amerika Kusini
Shirikisho la Madaktari wa Amerika Kusini   (@VATICAN MEDIA)

Kwa kuzingatia tafakari hizo, Papa Leo  aliwaalika wote “kuendelea kuchunguza umuhimu wa uhusiano wa daktari na mgonjwa. Uhusiano kati ya watu wawili, na miili yao na nafsi zao za ndani, na historia yao.” Imani hii pia aliongeza Papa, “inatusaidia kutoa nuru  juu ya nafasi ya akili Unde (AI)  katika dawa: inaweza na lazima iwe msaada mkubwa katika kuboresha huduma za matibu, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya daktari, kwa sababu wao,  kama Papa Benedikto XVI alivyosema, "ni 'hifadhi ya upendo,' ambao wanaleta utulivu na matumaini kwa wanaoteseka" (Benedikto  XVI, Malaika wa Bwan, Julai 1, 2012). Mfumo wa mitambo hauwezi kamwe kuchukua nafasi ya ishara ya ukaribu au neno la faraja. Baba Mtakatifu Leo alisema kuwa  changamoto kubwa na za kusisimua zinawangoja, ambazo lazima zikabiliwe kwa matumaini.

Wawakilishi wa Shirikisho la Madaktari wa Amerika Kusini
Wawakilishi wa Shirikisho la Madaktari wa Amerika Kusini   (@VATICAN MEDIA)

Mwishoni mwa mkutano huo Papa aliwaombea  “Kristo Yesu, tumaini letu”(1 Tim 1:1) na Bikira Maria, Afya ya Wagonjwa, awasindikize wote katika hija hii tunayoifanya sisi sote kuelekea nyumba ya Baba. Mungu awabariki nyote. Asante. Lakini kabla ya kuwaga, Papa Leo aliongeza kusema: “Na kwa hivyo tunahitimisha kwa kuomba baraka za Bwana juu yenu na wenzenu  wote. Kama nilivyosema, uhusiano huo, fursa hiyo ya maisha na matumaini kwamba ninyi pia kwa kutoa kwa wagonjwa wenu wote na wagonjwa wengine wote ni muhimu sana."

02 Oktoba 2025, 17:01