Tafuta

"Leo kutoka Chicago,"makala kuhusu asili ya Papa Leo nchini Marekani,itatolewa Novemba 10

Katika fursa ya kuadhimisha kumbukumbu ya miezi sita ya upapa wake,Jumatatu saa 12.00,jioni,utarayarishaji wa makala kuhusu Papa utachapishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika lugha tatu(Kiingereza,Kiitaliano,na Kihispania)kwenye chaneli za Vatican News.

Vatican News

Katika hafla ya maadhimisho ya miezi sita ya kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV, Vatican Radio – Vatican News inachapisha "Leo kutoka Chicago," makala inayofuatilia historia, asili ya familia, masomo, na wito wa  Kiagostinian  wa Robert Francis Prevost katika nchi yake ya asili: Marekani. Safari inaanza na utoto wake huko Dolton, kupitia kumbukumbu za kaka zake Louis na John, na inaendelea kupitia shule na vyuo vikuu, Jumuiya na parokia, pamoja na sauti za kaka zake, walimu, wanafunzi wenzake, na marafiki wa muda mrefu.

"Leo kutoka Chicago" inafuata makala ya "León de Perú," iliyotolewa mwezi Juni iliyopita, kuhusu miaka ya utume wa Papa katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Ni toleo la Kurugenzi ya Uhariri ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kwa ushirikiano na Jimbo Kuu la Chicago na Utume wa Unjilishaji Mpya wa Mpanzi (Apostolado El Sembrador Nueva Evangelización (ESNE). Lilitayarishwa na waandishi wa habari Deborah Castellano-Lubov, Salvatore Cernuzio, na Felipe Herrera-Espaliat, huku likihaririwa na Jaime Vizcaíno Haro.

Saa 12:00 jioni (saa za Roma-ikiwa ni saa 2 za Usiku Afrika Mashariki na Kati) Jumatatu, tarehe 10 Novemba 2025, makala hiyo itachapishwa kwenye chaneli ya YouTube ya Vatican News kwa lugha tatu (Kiingereza, Kiitaliano, na Kihispania) na kusambazwa kupitia vyombo vingine vya habari vya kimataifa.

"Leo kutoka Chicago" itaoneshwa katika siku zijazo katika miji kadhaa ya Italia wakati wa mikutano ya hadhara iliyotangazwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ajili ya wasifu wa Papa Leo, hasa huko Vicenza na Cremona itakayofanyika (Novemba 21), Trento (Novemba 25), Verona (Desemba 1), Genova (Desemba 5), ​​na Cagliari (Desemba 15).

Leo kutoka Peru: makala kuhusu Papa Leo XIV

 

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui

 

08 Novemba 2025, 13:57